Amesema kwenye Ukristo, he is just being specific. Na kaelezea experience yake kama nawewe una experience ya urithi ulioona kwa Wahindu au Budha ukiwa Nyarugusu sema.
Thread ina utoto gani. Mbona maelezo yake mafupi yanaleta maana na ujumbe na yana mantiki.
Kwanza hapa anazungumzia mazingira ya Ulaya ambapo unakuta mtu ana mtoto mmoja au wawili kwa kutaka. Mtoto wa kike akiolewa baba mkwe anaweza mrithisha mtoto wake au familia au akaweka mkwe wake custodian wa estate. Mifano ipo mingi sana.
Ila bongo baba mkwe awe mfanyabiashara na mkwe wake mfanyabiashara, ila baba mkwe alibahatika kupata binti pekee. Unakuta bora agawe mali kwa ndugu ambao hawajui lolote kwenye uendeshaji wa biashara kuliko ampe mkwe wake (assume binti yake alifariki ila aliacha watoto).
Wazungu wanagawa mali kuangalia legacy, kazi waliyosotea miaka na miaka je itabaki kuwa hai. Huku kwetu wanagawa mali tu kama kumfaidi mfiwa. Mtu anafariki akiwa bilionea ila baada ya miaka mitatu biashara zinakufa.
Nchi nyingine hakuna guarantee ya nani anapewa urithi, hata museum, charity organization, state, binamu, mpwa, mtoto wa kambo wanaweza pewa urithi mkubwa au sawa na mtoto wa kuzaliwa.