Kampuni za kuuza viwanja zinaumiza wananchi, Serikali iingilie kati

Kampuni za kuuza viwanja zinaumiza wananchi, Serikali iingilie kati

Dan Zwangendaba

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Posts
5,814
Reaction score
8,118
Ni jambo la kushangaza unapopita mitandaoni kukutana na matangazo ya kampuni zinajinadi kuuza viwanja vya SQM 200, 300 nk, katika maeneo mbalimbali nje ya Jiji. Tena, mbaya zaidi wanaviuza kwa vipimo vya futi. Hivi kweli tunaruhusu viwanja vya SQM 200 miaka hii? Je, haya makampuni hayana mdhibiti? Waziri wetu mchapakazi, hili limekushinda au?

Aidha, sambamba na hilo sioni sababu ya nchi yetu viwanja kuuzwa bei kubwa kupita kiasi. Kunahitajika kuwa na regulator na bei kikomo katika ardhi, nadhani vinginevyo wananchi wanaumia kununulishwa viwanja kwa bei kubwa sana.
 
Wizara ishaburuzwa hapo hamna wizara toka zamani ni kikundi cha wahuni tuu. Fungu walikuwa wanapata jiulize walishindwa hata kupanga maeneo mpaka nchi ikajengwa kiholela hili mpaka leo wamelishindwa waliweza Dodoma kipindi cha amri za jiwe basi.
 
Naunga mkono hoja,kingine ni huo ULANGUZI wa viwanja, eti square metre 1 =40,000--60,000/=Tsh hasa Maeneo ya Kigamboni ilihali hakuna muendelezo wowote wa kimiundombinu uliofanyika..WIZI tu
Ni uhuni kabisa wananchi wanafanyiwa. Leo hii masikini wanazidishiwa umaskini kwa kuuziwa ardhi bei juu utadhani almasi.
 
Wizara ishaburuzwa hapo hamna wizara toka zamani ni kikundi cha wahuni tuu. Fungu walikuwa wanapata jiulize walishindwa hata kupanga maeneo mpaka nchi ikajengwa kiholela hili mpaka leo wamelishindwa waliweza Dodoma kipindi cha amri za jiwe basi.
WIZARA YA ARDHI ni Sehemu ya hayo MATATIZO na MIGOGORO ya ARDHI NCHINI
 
Serikali imelala.

Ardhi imeshikwa na majambazi hatari sana.
 
Back
Top Bottom