Kampuni za simu zaiangukia Serikali tozo ya miamala. TPSF yataka benki zisiachwe

Kampuni za simu zaiangukia Serikali tozo ya miamala. TPSF yataka benki zisiachwe

Hapo kampuni za simu zinajaribu kuepuka mdororo utakaowakumba kwa kukimbiwa na wateja!

Unakumbuka kipindi cha JPM Jiwe jinsi mabenki walikimbiwa kwa watu kuhamisha pesa zao?

Dawa ni chukua chako mapema na ujipangie mwenyewe jinsi ya kukitumia!!
Watu wanatoa tu miamala ya kuweka haipo
 
Mimi sijafanya muamala wowote tangu tozo za kizalendo pori zilivyoanza na sio kawaida yangu
Wajiandae kisaikolojia
Watu wakiamua wanaweza mbona hawa wa mitandao watakubali wenyewe
Nimeweka msimamo sitatumia tigo pesa wala mpesa.
Hela yangu naweka benki, mtu akiwa na shida namwambia atafute akaunt ya benki naenda kwa wakala namtumia hataki aache.

Wananchi tumezidi kuigopa serikali kwa kuhofia kupigwa na polisi n.k sasa kwenye hili hakuna wa kupigwa wala kuulizwa, tuwanyooshe kimya kimya
 
Hizi ni kelele za kitambo tuu kama mafuta afu mtatulia tuliii.

Yaani nchi ambayo unamwambia mwananchi adai risiti hafanyi afu umuwekee kodi mbadala ndio awe analia Lia? Sitegemei Serikali kusalimu amri kwa upuuzi.

Hayo makampuni yanatuibia Sana eti nao wanalia.Afu wauza magaseti wanatafuta habari za kuuzia magaseti hakuna chochote
Niliposoma "magaseti" nikatosheka na kiwango chako cha uelewa.
 
Serikali inakosea wananchi, inayakosea hata makampuni ya simu.

Haiwezekani dukani kwangu mchele nauza kilo alf 2, we unakuja unanambia niuze alf 3, ili we uchukue hiyo alf 1. Unaniumizia wateja...

Huko ni kukimbiziana wateja, na kuharibiana biashara.
 
Nchi yenyewe ni maskini, mnaanzisha na kujenga miradi mingi mikubwa kwa pamoja, sijui mlitegemea miujiza bila mipango makini ya wapi mtapata pesa bila kuumiza wananchi... hata nchi zile zile zilizoendelea zenye uwezo, mambo haya ya miradi mikubwa, hujaribu kufanya 'projects stagerring planning' kwa stages za implementation, na sio kwa mihemko ya kisiasa na matokeo yake ndo haya yanayoendelea....
 
Kampuni za simu wameinvest sana mpaka hii system ya pesa kwenye simu kua apo ilipo .....

Then wapo kishetria na wanalipa kodi kama inavyotakiwa....:

Sasa anatokea bongo lala anaweka ela nyingi kuliko ni hlkuaribu uwekezaji
Wewe umewahi toa au kutuma pesa then ukakuta makato ya serikali yamezidi wanayopata kampuni za simu? Pumbavu zao wa me invest kutuibia?
 
Wewe umewahi toa au kutuma pesa then ukakuta makato ya serikali yamezidi wanayopata kampuni za simu? Pumbavu zao wa me invest kutuibia?
Samahan ndugu nataka kufaham ,kwa mfano ktk hiz huduma za kifedha kivip kampun za sim zinaiba au ilitakiwa iweje ili waonekane wasiibe ,maana kwa uwelewa wang mm ni kwamba kabla ya aya makato ya serikal mfano elf 10 walikua kampun za cm zilikua zinakata elf 1 mia nne ela iyo inagawanyika kama mara nne hiv wa kwanza wao wenyewe ,pil wakala apa wakala analipwa mara mbil yan mfano umekatwa elf 1 mia nne mteja wakala watakupa labda mia 3 alaf apo apo ukituma wakala elf 10 kumbuka ukituma mteja hakatwi watakulpa tena wakala kama mia 2 hiv ,fungu la tatu linaenda serikalin,lakn sasa iv elf kum iyo iyo utakatwa kwanza elf 1 mia 400 ya mtandao alaf utakatwa utakatwa 320 ya serikal ,kumbuka ktk iyo elf 1 mia 400 kuna kodi ya serikal ,sasa apo mwiz nan apo nimezungumzia kutoa tu bado kuituma iyo elf 10
 
Tuchangie Maendeleo mkuu , kodi inayokusanywa haiwezi kutosheleza kujenga miradi mkibuwa inayoendelea.
Atukatai kulipa kodi mkuu ila kodi iwe kwa kiasi na kuzingatia uwezo wa walipaj, tozo imekua kubwa mno na haivumiliki....

Kifupi kaboronga sana jamaa,

Angeongeza kiasi ata kwenye mamia miamala ingekua mingi na angepata tofaut ni apo watu watatumia kwa emegency tu
Hivyo atua hii biashara kwenye kampuni, mawakala wakuu na mawakala...
Muda utaongea.
 
Wewe umewahi toa au kutuma pesa then ukakuta makato ya serikali yamezidi wanayopata kampuni za simu? Pumbavu zao wa me invest kutuibia?
Angalia kwenye kutuma
IMG_20210715_104508_981.jpg
 
Wewe umewahi toa au kutuma pesa then ukakuta makato ya serikali yamezidi wanayopata kampuni za simu? Pumbavu zao wa me invest kutuibia?
Sasa kumbe unabisha kitu usicho kijua

Mfn... Kutuma Laki kampuni inakata 1000 na apo kuna kod ya serikali ndan yake, kuna kamishen ya wakala, kuna operation costs na faida...

Afu kuna jitu likaeka tozo 2530
Kwa iyo jumla ni 3530..

Wanakuibia Nini? Kama unaibiwa si uache kutumia kama watu wanavoacha kueka ela kweye simu
 
Mimi sijafanya muamala wowote tangu tozo za kizalendo pori zilivyoanza na sio kawaida yangu
Wajiandae kisaikolojia
Watu wakiamua wanaweza mbona hawa wa mitandao watakubali wenyewe
Nishalizwa sana Ijumaa ilitumwa 10 sema aliweka na yakutolea jumamosi imetumwa 50 makato ikawa juu yangu nikalambwa 3850 Leo tena imetumwa 15 makato juu yangu 1770☹️
 
Tokea lini kampuni za simu zikawaonea huruma wateja wake?

Mama anaupiga mwingi

Kazi iendelee
lazima walalamike kwasababu watu wakisusia kutuma miamala, kampuni za simu zinapungua mapato sana. walikuwa wanapiga sana pesa kwenye maMPESA huko, sasa watu kama hawatumi tena ndani ya wiki tu hapa wamepoteza mabilioni, bila hata sababu ya msingi. walitakiwa kushirikishwa halafu waweke reasonable rate ambayo haitaleta maumivu. reasonable rate ikiwepo na kwa watu wengi zitakusanywa nyingi. excessive rate ikiwepo watu watakatwa nyingi ila watumiaji watakuwa wachache hivyo utapata kidogo kuliko ile rate ya chini. akili kumkichwa.
 
Atukatai kulipa kodi mkuu ila kodi iwe kwa kiasi na kuzingatia uwezo wa walipaj, tozo imekua kubwa mno na haivumiliki....

Kifupi kaboronga sana jamaa,

Angeongeza kiasi ata kwenye mamia miamala ingekua mingi na angepata tofaut ni apo watu watatumia kwa emegency tu
Hivyo atua hii biashara kwenye kampuni, mawakala wakuu na mawakala...
Muda utaongea.

Nakubaliana na wewe ,tozo muhimu ila waliyoweka ni kubwa!!
 
lazima walalamike kwasababu watu wakisusia kutuma miamala, kampuni za simu zinapungua mapato sana. walikuwa wanapiga sana pesa kwenye maMPESA huko, sasa watu kama hawatumi tena ndani ya wiki tu hapa wamepoteza mabilioni, bila hata sababu ya msingi. walitakiwa kushirikishwa halafu waweke reasonable rate ambayo haitaleta maumivu. reasonable rate ikiwepo na kwa watu wengi zitakusanywa nyingi. excessive rate ikiwepo watu watakatwa nyingi ila watumiaji watakuwa wachache hivyo utapata kidogo kuliko ile rate ya chini. akili kumkichwa.
Yani mwigulu ni Kengee sanaa.. Kweli hesabu gani huwa anapiga sijuii[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hizi ni kelele za kitambo tuu kama mafuta afu mtatulia tuliii.

Yaani nchi ambayo unamwambia mwananchi adai risiti hafanyi afu umuwekee kodi mbadala ndio awe analia Lia? Sitegemei Serikali kusalimu amri kwa upuuzi.

Hayo makampuni yanatuibia Sana eti nao wanalia.Afu wauza magaseti wanatafuta habari za kuuzia magaseti hakuna chochote
Wizi wa makampuni ya simu unaujua wewe tu? Serikali pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama havijui?
 
Back
Top Bottom