Kampuni za simu zimepunguza vifurushi vya internet tena

Kampuni za simu zimepunguza vifurushi vya internet tena

Tatizo hamsifii vya kutosha " huduma zao" sasa mnataka wafanyeje! Utadhani yananitoka moyoni.
 
Tulishakubaliana kuwa TANZANIA ni kati ya NCHI 5 zenye unafuu wa gharama ya kujiunga na data
 
Ifahamike kwamba vifurushi hivi havina mfanano Kwa wateja wote.

Yani wanachofanya wakiona wewe ni mteja mzuri wanakupandishia wewe kama wewe,ukiwapiga chini Kwa muda wanakupa tena ofa kabambe.

Binafsi huwa ninacheza na voda na tigo, voda walinikazia nikapiga chini nikaishi na tigo Kwa kifurushi cha 5000 GB 2,dkk 200 Kwa wiki ,wakaniona kiazi wakafika level ya GB 1.2 dkk 150 Kwa 5000,nikapiga chini kurudi voda nikakuta washanilegezea
unachosema ni sahihi mm airtel wamenipandishia kwa kuwa ni mtumiaji mkubwa na nimekuja gundua majuzi baada ya jamaa yangu kujiunga kwa 2000 akapata kifurushi kikubwa mm napata kidogo.acha na mm niwapige chini airtel nashukuru kwa kunifumbua macho.
 
Nilifurahi kwenye heading nikachukia kwenye content
 
Huu mtindo wa kupangia siku za kutumia bando nililolipia kwa pesa yangu Ni wakishamba sana
 
Vodacom na Tigo walikuwa na kifurushi cha @1000tsh dk 100, sms 100 na 1Gb 3days au kwa @1500 tsh kwa 7days.
Sasa hivi voda cha 3days wameweka 800MB na tigo 750MN.
Airtel ndio wameua zaidi in short jionee mwenyewe.
Najua serikali ina mkono au baraka zake hapa.

View attachment 1958946

View attachment 1958947
TTCL wanalipa vizuri, 1000 wiki GB 1.2 dakika 10
5000 mwezi GB 2.2 dakika 20
Screenshot_20211001-121244_Gallery.jpg
Screenshot_20211001-120946_Gallery.jpg
 
Back
Top Bottom