Kamshina wa Uhamiaji Makakala, tafadhali kataza upesi mambo haya yanaofanyika Ofisi za Uhamiaji Kurasini

Kamshina wa Uhamiaji Makakala, tafadhali kataza upesi mambo haya yanaofanyika Ofisi za Uhamiaji Kurasini

Bongo wanaona kuwa na passport ni anasa au ni kwa ajili ya wa watu fulani tu, akili zetu zimelala sana
Na kuwa na passport ni haki ya kila raia. Wanafanya urasimu na hawazitoi bure. 150k sio pesa ndogo.
Na utailipa kila baada ya miaka 10!!

Ujinga mwingine ni endapo umepoteza itakugharimu 500k, kupata nyingine.

Na iki expire wanataka uanze utaratibu upya. longolongo
 
Copy wakati wa passport huwa ni ya nini?
anyway pale Mambo ya Ndani wako straight forward.
Hata hayo mambo yakukaguliwa mabegi sio kihivyo.

Nimeingia pale mara nyingi bila ukaguzi wowote hasa ukienda na gari. Sijawahi kukaguliwa.
Gari linaingilia wapi pale Mambo ya ndani Kama wwe siyo stuff wa pale!? Naomba ufafanuzi kidogo hapo unaposema ukienda na gari!!
 
Sijui kwa kweli, nimewahi kwenda Uhamiaji kurasini Mara moja tu.

Ila mara nyingine zote nimeenda pale Mambo ya Ndani hawana mambo mengi.

Ukiingia pale maingate kuna askari police wanaofungua geti kwa remote.
Ukiingia na Begi utalipitisha kwenye ile scanner yao upande wako wa kulia. Na utaendelea na mambo yako.
Pale mlango wa uhamiaji utajaza lile daftari lao basi.

Kwa kweli hakuna mambo mengi pale.

Ila bado hujanijibu kitu, hizo photocopy kwenye kuchukua/kulipia/kuprocess passport huwa ni kwa ajili ya nini?
Kuna Nyaraka niliiambatanisha katika Fomu ya Ombi ya Pasipoti Mpya ( Electronic ) ndipo nikatakiwa kwenda Nje kutoa Copy ndipo nikakumbana na hili la Copy Moja tu ya Kawaida ( siyo Coloured ) kuwa ni Tsh 500/= kwa Ukurasa ( Page )

Stationery yenyewe inatazamana perpendicular na Geti Kuu la Kuingia UHAMIAJI Kurasini utakikuta Kidada Kimoja kina Nyodo fulani hivi ( japo ana Sura mbaya ) na kuna Kijana Mmoja ana Pua Kubwa na Kichwa Kikubwa pengine ndiyo maana hana Akili na ana Roho Mbaya ile.

Nina hasira nao sana hawa Wapuuzi.
 
Pole sana.

Ila kama uliweza kupata huduma hakuna shida mkuu.

by the way huduma nyingi serikalini ni za hovyo sana.

Niliwahi kwenda pale TRA ilikuwa mida ya saa tatu Asubuhi nimeingia chumba namba 12 wanaposhughulikia mambo ya VAT. ni balaa tupu.

Washkaji wamekusanyika wanaangalia preview ya mechi ya Arsenal, bila kujali kuna mtu pale anayesubiria huduma.

Ni balaa sana
 
watanzania ni watu wa ajabu sana wanapenda sana kutumia shida za watu kujiingizia kipato kisicho halali

mfano hapo kwenye kopi ya tsh 100 wao wanafanya tsh 500 na wanajua watawapata wengi,ujinga huo huo ulikuwepo Police pale ukienda kutafuta loss report

nchi imejaa laana hii watu wanawanyonya watu pesa isiyo halali na ndio mana shida haziishi 😎
Na ndio maana tunasema idara nyingi za serikali wapewe wawekezaji tu!kwa sababu wazawa wengi ni wezi
 
Mkuu hivi wale DP hawawezi kweli kutuendeshea uhamiaji,maana sisi ndio kama hivyo atuwezi kujiendesha,mtu akipata cheo anataka kuwa Mungu mtu na kuwaanyosha watanzania wenzake
Yaani hapa pia kuna TRA , TRC,ATCL,UDART napendekeza hivyo vyote wapewe wawekezaji maana wabongo wameshindwa kabisa hawa huko kote ni mapicha picha tuu , wanawaza wizi na uhujumu pamona na uzembe na uvivu
 
Eti mkuu wa uhamiaji atoe tamko la kupunguza gharama ya kopi kwenye biashara binafsi za Watanzania[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

Hii ndio product ya Vyuo vya hovyo kama SAUT
Kulipuka kichaa ndio huanza hivyo hivyo
Badala ya kwenda kuwaomba wenye photocopy machine wampunguzie bei anaenda kwa kamishina wa uhamiaji

Mwenye namba ya simu ya Hospitali ya vichaa Mirembe ampe mleta mada yaweza msaidia amwambie aongee nao
 
Kulipuka kichaa ndio huanza hivyo hivyo
Badalabya kwenda kuwaomba wenye photocopy machine wampunguzie bei anaenda kwa kamishina wa uhamiaji

Mwenye namba ya simu ya Hospitali ya vichaa Mirembe ampe mleta mada yaweza msaidia amwambie aongee nao
Huko Mirembe Mental Hospital ningeshauri ungeanza Kwanza kuwapeleka Wazazi wako wenye hilo Tatizo Sugu ambalo nawe Umezaliwa nalo.
 
Kulipuka kichaa ndio huanza hivyo hivyo
Badala ya kwenda kuwaomba wenye photocopy machine wampunguzie bei anaenda kwa kamishina wa uhamiaji

Mwenye namba ya simu ya Hospitali ya vichaa Mirembe ampe mleta mada yaweza msaidia amwambie aongee nao
Chuo ambacho sio cho hovyo ni kipi? Naomba usinitajie UDSM tafadhari
 
Chuo ambacho sio cho hovyo ni kipi?
Mkuu huyo yuko UVCCM na bahati nzuri hajui kuwa namjua vyema tu na sasa namtafutia timing ajae vizuri nimuumbue.

Kwa aina ya arguments zake hapa JamiiForums unaona ni Mtu aliyesoma Kweli?

Yuko UVCCM na ni Msafisha Vyoo wao.

Cc: YEHODAYA
 
Chuo ambacho sio cho hovyo ni kipi? Naomba usinitajie UDSM tafadhari
Kaangalie rank za vyuo bora duniani na Africa ambavyo wasomihu vi rank

Nenda Google utapata majibu sio nikujibu mimi .Kazi ya ku rank hufanywa na taasisi za kitaalamu sio.mimi na wewe nenda katizame huko utajua kila chuo kikiwemo.UDSM au SAUT ni cha ngapi duniani au Afrika kwa ubora
 
Mbona humwambii Kazi yako Kubwa hapo UVCCM ni Kusafisha Vyoo vinavyotumiwa na Makada na Mabosi zako?
 
Mkuu huyo yuko UVCCM na bahati nzuri hajui kuwa namjua vyema tu na sasa namtafutia timing ajae vizuri nimuumbue.

Kwa aina ya arguments zake hapa JamiiForums unaona ni Mtu aliyesoma Kweli?

Yuko UVCCM na ni Msafisha Vyoo wao.

Cc: YEHODAYA
Kubali tu kichwani hazimo

Huwezi kwenda kwa kamishina wa uhamiaji na hoja ya eti apunguze bei ya photocopy ya wafanyabiashara binafsi kutoka mia tano hadi 100 au 50

Kubali tu akili zilikuruka ukakumbula Milembe hospitali ulikowahi kulazwa akili ikakutuma kwa kamishina
 
Leo Makada wa CCM na UVCCM hawajachafua Vyoo unavyoviosha ( 24/7 ) ili nikutafutie Tenda ya Kusafisha Vyoo Kwingineko?
 
Yaani hapa pia kuna TRA , TRC,ATCL,UDART napendekeza hivyo vyote wapewe wawekezaji maana wabongo wameshindwa kabisa hawa huko kote ni mapicha picha tuu , wanawaza wizi na uhujumu pamona na uzembe na uvivu
Wabongo ukitaka wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa sana,wwe wawekee Mtu mweupe Kama ndiyo msimamizi Mkuu,hapo Wabongo watapiga kazi sana kwa kumuogopa white skin color!!
 
Wabongo ukitaka wafanye kazi kwa ufanisi mkubwa sana,wwe wawekee Mtu mweupe Kama ndiyo msimamizi Mkuu,hapo Wabongo watapiga kazi sana kwa kumuogopa white skin color!!
Yaan miradi ya uma inatajirisha watu wachache halafu serikali inaambiwa eti mashirika mengi yanajiendesha kwa hasara ushenzi huu! Tuwape wawekezaji tuu kila kitu.

Kusimamia watu ambao kila uchwao wanawaza kubuni mbinu mpya za wizi na sio za ufanisi katika kazi na hasa kwa linchi likubwa kama tanzania hii ni kazi sana sana hata mama tutamlaumu tuu!
 
Ukitaka kujua watanzania wengi ni wajinga,wewe soma komenti ujionee vituko.

Mtoa Mada yupo sahihi.
 
Back
Top Bottom