Kamwaga atembelea Ubalozi wa Cuba kuhakiki bei ya Gesi

WanaJF pigeni simu fasta huko cuba ili jumatano tuwe na majibu kwani Gesi sh ngapi?
 
Kulikuwa hakuna sababu ya kulinganisha Bei ya Cuba na Tanzania huko ni kutoana kwenye reli na kuacha kuongelea issue ya Maana..., Na Issue ya maana ni hii Kwanini tunahamasisha kutumia fedha za kigeni katika Kupikia badala ya Nishati ambayo tunayo ?!! Gesi Sio yetu na tunanunua na ukisema tushushe bei ni kutumia Kodi zetu ili kutajirisha wengine....

Mjadala kuhusu gesi ya cuba lazima uanze na litereture review ...msomi unataka kuikimbia hoja?
 
Mjadala kuhusu bei ya gesi ya majumbani nchini Cuba umeendelea kuchukua sura mpya baada ya kurushiana maneno kati ya mwanahabari na mchambuzi wa siasa Ezekiel Kamwaga na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole.

Agosti 29, 2025, Polepole kupitia mitandao ya kijamii alidai kuwa bei ya mtungi wa gesi wa kilogramu 20 nchini Cuba ni Shilingi 2,000 za Kitanzania, akilinganisha na bei ya mtungi wa kilogramu 15 nchini Tanzania inayofikia kati ya Shilingi 56,000 hadi 60,000.

Hata hivyo, Agosti 30, Kamwaga alipinga kauli hiyo wakati akichangia mjadala ulioandaliwa na Jukwaa la Wachambuzi na PPPC, akisema kuwa bei ya mtungi wa gesi wa kilogramu 10 nchini Cuba ni kati ya Shilingi 100,000 hadi 300,000 za Kitanzania.

Hali ilichukua mkondo mpya Agosti 31 baada ya Polepole kumshutumu Kamwaga kwa kutumia Google kama chanzo chake cha taarifa, akieleza kushangazwa na uhalali wa takwimu hizo.

Septemba 1, 2025 Kamwaga amefika katika Ubalozi wa Cuba jijini Dar es Salaam kujiridhisha kuhusu bei halisi ya gesi nchini humo.

“Nimeamua kuja hapa kwenye Ubalozi wa Cuba kwa sababu hapa kuna watu waliowahi kuishi Cuba, wengine wamewahi kununua mitungi ya gesi kule. Angalau nikichanganya taarifa za mtandao na hizi za hawa watu ninaweza kupata kitu kizuri. Nikitoka hapa sasa ninaweza kuchakata taarifa nilizopata leo na zile za mtandaoni ili tuendeshe mjadala halisi. Kesho nitazungumza kuhusu hilo baada ya kuchakata taarifa nilizopata,” amesema Kamwaga.

Unadhani mzani wa hoja katika mjadala huu utaegemea upande upi kati ya upande wa Polepole na ule wa Kamwaga?
View attachment 3461747
Kwanini asiende kuhakiki kuhusu wahuni kukiteka chama hajataka kulifuatilia hilo kaamua kufuatilia jambo lisilo na tija
 
Tafsiri ya hiki anachokifanya sasa huyu Ezekiel Kumwaga (Mwandishi wa habari) ni kuwa amekubali kuwa ile taarifa yake ya mwanzo kumpinga Balozi Humphrey Polepole ilikuwa ni uongo, ni taarifa ambazo si za kweli, za kuokoteza mitandaoni tu na zisizo na uthibitisho...

Mimi nilimshangaa sana Ezekiel Kumwaga, kwamba anabishana na mtu ambaye ndo katoka juzi tu kule Cuba akiwa ameishi miaka mingi na ametumia nishati hii maisha yake yote huko...

Sasa anawatafuta wengine walioishi Cuba, lakini haamini taarifa za huyu anayeishi huko Cuba hata sasa...!!

Na inashangaza kidogo kwa sababu hili sio la ajabu hata kidogo kwa serikali ambazo zinajali watu. Kwa sababu ni kweli kuwa, bei halisi ya gesi sokoni inaweza kuwa juu sana, lakini serikali ikaweka subsides ili wananchi wapate bidhaa hiyo hiyo kwa bei rahisi/ya chini...

Na Ezekiel Kumwaga anashindwa kuelewa kuwa, Cuba is socialist State ambao uchumi wao ni wa kijamaa kwelikweli kama ilivyo Vietnam, North Korea, China nk
 
Back
Top Bottom