Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
1. Kamwe Marekani haiwezi kuruhusu nchi yoyote duniani iwe na uwezo wa kuunda silaha ambazo mwisho wa siku zikirushwa zinaweza kufika au kutua ndani ya ardhi ya Marekani na hatimae kuleta madhara kwa wamarekani ndani ya marekani. Na ndio maana nchi zilizojaribu kutengeneza silaha za maangamizi hulengwa na kuorodheshwa na marekani kama ni nchi hatari na tishio zaidi kwa usalama wa dunia. Iraq na Iran ni mifano mizuri ya nchi hizo na tunaweza kuzitumia kama mifano kwa sera ya marekani ya kudhibiti nchi hizo kua na silaha za maangamizi.
2. Kamwe Marekani haiwezi kuzichokoza au kuzitisha kijeshi nchi ambazo tayari zina silaha nzito na za kisasa zenye uwezo wa kuifikia ardhi ya Marekani kirahisi na kuathiri watu wake na uchumi wake. Baadhi ya nchi ambazo Marekani haiwezi kuthubutu kuzivamia kijeshi ni pamoja na Russia, North Korea, China n.k.
Nchi nyingine zote ambazo sio kitisho cha kiusalama kwa marekani lakini zina maslahi ya kiuchumi kwa nchi hiyo, zinaweza kuvamiwa wakati wowote na Marekani na hakuna nchi yoyote ulimwenguni inaweza kuzuia hilo kutokea, kutokana na uwezo mkubwa wa kijeshi wa marekani, uwezo mkubwa wa kiuchumi na ushawishi mkubwa wa kisiasa ilionao Marekani duniani kote.
Mungu Ibariki Tanzania.

R.I.P Ayatollah Ali Khamenei
Mungu Ibariki Tanzania.