Kamwe tusiaminishane upuuzi wa Wahuni! Nchi inajengwa na sisi

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Inawezekana kabisa washauri na actors mbalimbali ndani ya Serikali kwa sasa ni waamini wa mikopo. They might have good sweeter arguments for now.

Lakini wazalendo wa kweli tutabaki na msimamo wetu.

Ni upuuzi kutegemea walami kutuneemesha watanzania. Hii ni fallacy.

Jingalao atasimama daima kwenye Sera za kujitegemea na sio upuuzi mwingine.

Nilisimama kipindi cha JK, Magufuli na sasa Samia.

I will never change on this.
Nipo tayari tozo iongezwe kama inahitajika lakini si mikopo ya kuhuni!!!

Maendeleo yataletwa na jasho la watanzania and not otherwise tusidanganye,tusidanganywe na kamwe tusichekelee misimamo mibovu.

Nchi hii itajengwa,italindwa na kustawishwa na watanzania.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Jasho la watanzania limeshindwa kuleta maendeleo miaka 60 uhuru, itawezaje leo? Tatizo siyo kujitegemea tatizo ni ujamaa na kujitegemea ndiyo sera zilizofeli.

Mnataka elimu ya bure, mnataka matibabu ya bure, mnataka miundo mbinu ijengwe, mnataka ajira serikalini, mnataka viinua mgongo na pensheni mkistaafu, mnataka majeshi makubwa, polisi wengi, mnataka serikali iwafanyie kila kitu, mnataka big government.

Halafu mnazaliana kiholela kama sungura. Mtajitegemea vipi kwa hali hiyo?
 
Na fedha hazijawahi kuwa ndio chanzo cha maendeleo.

Tunachopata tunapokopa ni fedha tu.
Na kukopa ni pale inapolazimu.
Sio kukopa kopa kopa kopa tuuuu.
 
Tozo iongezeke bila transparency hapana!

Tozo iwe kama mfumo wa Forex tuweze kuona kilichokusanywa daily in realtime.
Kwenye web ya BOT kama ambavyo zile bei za USD, GBP, CAD zinavyodisplay kwenye web za benki zingine.
 
Jasho la watanzania limeshindwa kuleta maendeleo miaka 60 uhuru, itawezaje leo? Tatizo siyo kujitegemea tatizo ni ujamaa na kujitegemea ndiyo sera zilizofeli. Mnataka elimu ya bure, mnataka matibabu ya bure, mnataka miundo mbinu ijengwe, mnataka ajira serikalini, mnataka viinua mgongo na pensheni mkistaafu, mnataka majeshi makubwa, polisi wengi, mnataka serikali iwafanyie kila kitu, mnataka big government. Halafu mnazaliana kiholela kama sungura. Mtajitegemea vipi kwa hali hiyo?
We jamaa upewe wizara tu unaweza kutufikisha mbali.

Hawa wanafiki hawa address real problems tulizonazo. Wanajikita kwenye maneno tu uzalendo uchwara.
 
In conclusion. Nasikitika kukwambia huna akili Mana mkopo siyo msaada Ni pesa yako ileile.
 
Jasho la watanzania limeshindwa kuleta maendeleo miaka 60 uhuru, itawezaje leo? Tatizo siyo kujitegemea tatizo ni ujamaa na kujitegemea ndiyo sera zilizofeli. Mnataka elimu ya bure, mnataka matibabu ya bure, mnataka miundo mbinu ijengwe, mnataka ajira serikalini, mnataka viinua mgongo na pensheni mkistaafu, mnataka majeshi makubwa, polisi wengi, mnataka serikali iwafanyie kila kitu, mnataka big government. Halafu mnazaliana kiholela kama sungura. Mtajitegemea vipi kwa hali hiyo?

Bado una vijana wengi kwenye umachinga na upiga debe ambao hawalipi kodi, bidhaa wanazouza ni magumashi na nyingi ni za magendo.

Lakini bado wanataka umeme 27000, elimu bure, huduma za afya bure, ruzuku ya pembejeo, wanataka wauze pembezoni mwa barabara ili wenye frame wafunge tukose na kodi zao.

Wanachafua miji wanataka ifanyiwe usafi lakini hela ya kodi wanayotoa haiendani na mahitaji wanayolalamika kuyakosa.
 
Moja ya matatizo makubwa tuliyonayo ktk nchi yetu ni kukosa nidhamu katika mapato na matumizi ya pesa zetu.

Hatuna nidhamu wala utaratibu mzuri ktk ukusanyaji wa mapato yetu: kodi wanalipa wachache, wengi wanakwepa, rushwa kwenye ukusanyaji mapato, nk. Kagame anaposena anaweza kuiendesha nchi kwa kutumia bandari peke yake, simply anatupa challenge kutuambia we can do better, and we have to do better!

Hatuna nidhamu pia kwenye matumizi: pesa nyingi inaibwa, miradi hewa, ufisadi wa kutisha, matumizi yasiyoendana na ubora wa huduma/miradi, nk.

Tukijenga nidhamu ktk hayo tunaweza kabisa kupiga hatua kubwa za maendeleo bila kutegemea mikopo mikubwa inayoweza kuweka rehani usalama wa taifa letu.
 
Jasho la watanzania limeshindwa kuleta maendeleo miaka 60 uhuru, itawezaje leo? Tatizo siyo kujitegemea tatizo ni ujamaa na kujitegemea ndiyo sera zilizofeli. Mnataka elimu ya bure, mnataka matibabu ya bure, mnataka miundo mbinu ijengwe, mnataka ajira serikalini, mnataka viinua mgongo na pensheni mkistaafu, mnataka majeshi makubwa, polisi wengi, mnataka serikali iwafanyie kila kitu, mnataka big government. Halafu mnazaliana kiholela kama sungura. Mtajitegemea vipi kwa hali hiyo?
Ccm imefika mwisho
 
Ninachojua ni kuwa sukuma gang inazidi kudhoofishwa
 
Jasho la watanzania limeshindwa kuleta maendeleo miaka 60 uhuru, itawezaje leo? Tatizo siyo kujitegemea tatizo ni ujamaa na kujitegemea ndiyo sera zilizofeli. Mnataka elimu ya bure, mnataka matibabu ya bure, mnataka miundo mbinu ijengwe, mnataka ajira serikalini, mnataka viinua mgongo na pensheni mkistaafu, mnataka majeshi makubwa, polisi wengi, mnataka serikali iwafanyie kila kitu, mnataka big government. Halafu mnazaliana kiholela kama sungura. Mtajitegemea vipi kwa hali hiyo?
Lete ushauri wako mbadala basi mkuu
 
Back
Top Bottom