Kamwe tusiaminishane upuuzi wa Wahuni! Nchi inajengwa na sisi

Tz kama tukiwa na utu na uafilifu hata kidogo tu tungekuwa mbali sana
 
Kwani hao wengine waliwezaje kujitegemea na sisi tunashindwaje?
China waliweza huko malasiya waliweza je sisi na umli huu mpaka lini?
Mnadekezwa na miaka yote hii y uhuru bila kuchukua hatua?
Kilichobaki ni nyie kuombwa malinda basi.
 
watanzania wako tayari kukamuliwa kujenga nchi yao?, Watanzania wako tayari kufanya kazi kwa bidii kujenga nchi yao.?

Kuijenga Tanzania kwa sasa na ije ijetegemee, unahitaji watu wachape kazi kuanzia sasa non stop mpaka miaka 100 ijayo....na manufaa yataonekana kwa vitukuu huko sio sasa..
 
Wanakopa kufanyia nini je ulishawahi kuwaona tanzania wanataka mkopo?
Acheni upumbavu wenu.
Mtu anakopa kwenda kwenye sayari na tena anajikopesha mwenyewe, kisha wewe ujilinganinshe nae wakati unakopa kujenga choo?
Acheni upumbavu wa akili.
Huko serikali zai hawakopi kununua chakula ila kwa kufanyia ziada tu.
Tumia akili.
 
Kwani hao wengine waliwezaje kujitegemea na sisi tunashindwaje?
China waliweza huko malasiya waliweza je sisi na umli huu mpaka lini?
Mnadekezwa na miaka yote hii y uhuru bila kuchukua hatua?
Kilichobaki ni nyie kuombwa malinda basi.

Shida ni hiyo safari ya miaka mingi kuelekea kujitegemea ya milima na mabonde, Watanzania wataiweza kusubiri maendeleo kwa vitukuu..?

China na hiyo Malyasia hazikujengwa overnight, ni miaka mingi ya mateso na uvumilivu..
 
Mkuu Tanzania sio tunalalamika, tunapenda matokeo mkuu! Lets see impact uone kama kuna mtu atalalamika.

Kwa akili ya viongozi wetu hawa ya kufisadi na kujilimbikizia mali bila kuboresha welfare ya watu hamna mtu atafurahia kulipa kodi. Serikali inakomalia tozo halafu badala maisha yawe mepesi yanazidi kuwa mabovu.

Tozo zichajiwe ila tuone unafuu flani wa maisha then waseme kodi na tozo zenu ndio zinafanya wepesi ndio maana huduma ya hospitali kwa wajawazito ni nafuu...Tozo zenu mazolipa ndio maana shida ya pembejeo za kilimo hakuna tena..tozo mnazolipa ndio maana sasa hakuna shida ya maji wala umeme na gharama za kufungiwa huduma ni nafuu mno.

Sasa we matozo mnalipishwa na makodi ya REA ila bado kupata huduma ni kichefu chefu yani vita nikuvute ya ajabu. Mkopo wa madarasa, tozo za madarasa tutafika kweli. Ajira hamna za kutosha na bado tunakomalia kujenga madarasa tuendelee kujaza majobless mitaani badala ya kufikiria suluhu ya kuwapunguza.
 
Magufuli aliyekuwa muumini wa kujitegemea ndie anaeongoza kwakukopa pesa nyingi kwa kipindi kifupi,kakopa 29trln kwa miaka mitano tu record ambayo haijawahi kufikiwa na watangulizi wake.

Ila wakati Magufuli anajua kabisa anakopa,wananchi alikua anatudanganya kwamba ni makusanyo ya ndani na anachukia mabeberu.

Na ieleweke kwamba huyu anaeonekana hapendi kujitegemea ndie aliyeweka record ya juu ya makusanyo TRA kwa mwezi kuliko watangulizi wake.

Kinachomgarimu mama ni kusema ukweli kwamba tunakopa,mnapenda kudanganywa.

Hemu tueleze Magufuli ametekeleza dhana yakunitegemea kivipi?na kivipi mama hatekelezi dhana yakujitegemea?
 
Mkopo siyo pesa yako. Ingekuwa pesa yako utaikopaje? Hiyo ni pesa ya watu wengine ndo maana unadaiwa.
Sasa utasemaje mkopo Ni msaada wakati unalipa. Mkopo Ni strategy ya ya kiuchumi. Ungekuwa umesoma finance ungeona ujinga wako lakini ndo hivyo Tena. Kuna kitu kinaitwa debt financing versus equity financing . Debt financing is more profitable than equity financing. Google ujielemishe vinginevyo itabaki na ujinga huohuo.
 
Badili jina tafadhali, hizi nondo siyo za jitu jinga,ila za jitu lililo elimika
 
Kwa hiyo ukiwa umenuna unamwaga kiingereza cha tuisheni?😝😝😝😝😝
 
Achaneni na kuabudu mtu/watu/kikundi.
Tukiwaambia kuwa katiba mpya ndio mwarobaini wa upumbavu kama huu unaoendelea,mnaleta "uchama" mkiamini kuwa katiba mpya itawatilia kitumbua chenu "mchanga".
Mimi ni mfuasi wa sera ya kujitegemea pia. Lakini tunajitegemea kwenye nini na nini? Tunaweza kweli kujitosheleza kimahitaji yetu bila kukopa au bila misaada!!?
Kama tunakopa au tunasaidiwa,tunakopa kwa ajili ya nini na wapi, kwa masharti yapi, na kwa uwazi upi!!??
Je,tunao utaratibu mzuri wa kuamua kuhusu mikopo na misaada au ni mtu mmoja tu anaamua!!??
Je,tuna utaratibu mzuri wa usimamizi wa pesa za umma (kodi,tozo,misaada,mikopo) ili kuhakikisha inatumika vyema!!??
 
Shida ni hiyo safari ya miaka mingi kuelekea kujitegemea ya milima na mabonde, Watanzania wataiweza kusubiri maendeleo kwa vitukuu..?

China na hiyo Malyasia hazikujengwa overnight, ni miaka mingi ya mateso na uvumilivu..
Kwani sisi tunashindwa?
 
Haya maneno ungemwambia magufuli wakati anakopa kujenga SGR kipande cha Dar - Moro ningekuona wa maana sana otherwise na wewe nakuona kama JoBo tu

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Utengeneze na ARV zako acha kubugia za msaada.
 
Mkopo siyo pesa yako. Ingekuwa pesa yako utaikopaje? Hiyo ni pesa ya watu wengine ndo maana unadaiwa.
Nikiwa nimekaa hapa nikiota moto, imenijia akilini kuwa maadui wetu wa maendeleo TZ ni watatu tu.

β€’ Uchawa ProMax wa Viongozi na Vijana wa UVCCM
β€’ Kipaumbele Ni kwenye Next Election na sio Next Generation
β€’ Presence of many Clueless Citizens

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani alikopa trillion 29
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…