kitoto wa vitoto
JF-Expert Member
- Jul 28, 2019
- 375
- 410
- Thread starter
- #101
Nilianza na 300,000/nilifungua genge la mazaga ya nyumban
- Je ni biashara gani?
- Mtaji ulikuwa kiasi gani?, ambapo ukaanza na faida ya 5k , kisha ikawaa faida ni 12k kwa siku.
- Je hilo eneo ulilofungulia biashara hakuna wengine wenye biashara kama yako? Kma wapo wengine je nini cha ziada ulifanya ili kuwavutia wateja?
Tofauti Yao na Mimi nilikuwa natafuta bidhaa kwenye msambazaji wa kwanza mara nyingi bidhaa ik8shapitia mikono mingi ya dalali Huwa Bei juu sana
Kwa hiyo nilikuwa naagiza nyanya Tenga Zima namuomba huyo anichangabyie mbichi kias ili niweze kuuza hata siku tatu bila nynya kuharibika
Pia nilikuwa nafungua mapema na kufunga usiku sana
Kitu kama parachichi nilikuwa naenda kusaka mwenyewe shambani au masoko ya matunda Kisha nauza Bei ndogo
Ila bidhaa ni nzuri na Bei ndogo
Mboga za majani nilikuwa nafuata kwenye bustani nanunua kabustan kazima navuna mwenyewe
ukilinganisha na jirani yangu
Pia nilikuwa na meza ya kuuza matunda yaliyokatwa
Kwa kila sahani buku
Matunda yanayovutia
NB
Kazi ya kuuza genge nilimpa msichana mmoja akawa anauza kama kawaida nikitoka job Mimi nakuja kumpokea yéye anaenda kupumzika ili kesho awahi kufungua.