Kamwe usiolewe na mwanaume asiyeweza kukulipia mahari

Kijana ndiye alilazimisha kuoa na wala si wazazi waliomlazimisha.

Kijijini nimeishi.

Mwanaume nitamsaidia mambo yote lakini si kumpa hela ya mahari..ni Bora nisiolewe kama ni hivyo.
Sawa huo ni mtazamo wako ni mzuri na si mzuri.
 
Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.

Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.

Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.

Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.

Kwanini hakufai??

Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?!

Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.

Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.

Na
Winnie Kilemo
Ni ujumbe mzuri.

Mabinti wakumbuke kuwa mahari ni ishara ya upendo kwa anayeolewa.

Kutoa mahari ni utamaduni wa binadamu kuonesha upendo.

Bila mahari ujue hakupendi ila anakutamani tu.
 
Yah huo ni mtazamo wangu na kwangu naona upo sawa bila kujali nani anauchukulia vipi.
Ikitokea uabadili mawazo au umenogewa na penzi ukaamua kumpa mahari nitaomba unijulishe nijue kilicho kufanya uamue hivyo ili nijifunze ai ya kitu kilichokupa msukumo wa kufanya hivyo
 
Siwezi kujioa mkuu
 
Ni ujumbe mzuri.

Mabinti wakumbuke kuwa mahari ni ishara ya upendo kwa anayeolewa.

Kutoa mahari ni utamaduni wa binadamu kuonesha upendo.

Bila mahari ujue hakupendi ila anakutamani tu.
Amen
 
Kumbukumbu la Torati 22:13-21
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹³ Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia,
¹⁴ kisha akamshitaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema, Nimemtwaa mwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama za ubikira;
¹⁵ ndipo babaye yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni;
¹⁶ na baba yake yule kijana awaambie wazee, Mwanamume huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye amchukia;
¹⁷ angalieni, amemwekea mambo ya aibu, asema, Sikuona kwa binti yako alama za ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira. Na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji.
¹⁸ Basi wazee wa mji ule na wamtwae yule mtu mume na kumrudi,
¹⁹ wamtoze shekeli mia za fedha, wampe babaye yule kijana, kwa kuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa Israeli; naye awe mkewe; hana ruhusa ya kumwacha siku zake zote.
²⁰ Lakini likiwa ni kweli neno hili, la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira;
²¹ na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.

Hii ndio sheria ya mahari sasa sijui mpo tayari?
 
Kwani mnataka kuoa bure?
 
Back
Top Bottom