Kamzalisha watoto wawili ila anadai siyo "type yake"

Kamzalisha watoto wawili ila anadai siyo "type yake"

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,708
Reaction score
35,719
Poleni na majukumu wadau,

Story ipo hivii,,
Mtaani kwetu huku Sutimbi, kuna jamaa flani ni mchizi wangu kiaina maana tumefahamiana Bar miaka kadhaa iliyopita (tumwite Masudi) na mara nyingi tunakutana baada ya saa za kazi na weekends.

Jamaa anafanya kazi shirika flani la kimataifa linamlipa viruzi maana ana nyumba (Japo haijaisha) anatembelea gari ya shirika japo ana ya kwake.

Kuna binti hapa mtaani anajishughulisha na Biashara ndogondogo, binti akajichanganya kwa Masudi na kubeba ujauzito, Masudi akadai kategewa hio mimba. Kwa kuwa Masudi hakuwa na lengo la kuishi nae akampotezea hali iliyopelekea biashara ya huyu binti kuyumba kimaisha na akawa anashindwa kulipa kodi ya chumba anachoishi na frem ya biashara ikabidi auze vifaa vya biashara na kulipa kodi ya miezi 3 sehemu nyingine sio mbali saaana na alipoishi awali.

Tukamshauri Masudi amhudumie mdada maana ile mimba ni yake, jamaa kwa shingo upande akaanza kumhudumia na kumhamisha ile nyumba na kumpangia chumba na sebule sehemu nyingine ila hakuwa naye karibu kiviiile ataenda kumwangalia binti hadi asikie anaumwa na si vinginevyo.

Muda ukaenda binti akajifungua mtoto mzuri saaana w kiume amefanana na Masudi, jamaa akaongeza huduma kwa binti.

Mtoto alivyokuwa jamaa akamfungulia tena abiashara yake ya awali na kumuongezea mtaji ili ajikimu kimaisha na akawa anatoa pesa za matumizi.

Binti ni mchakarikaji sana na mzuri wa sura hana skendo mtaani ana heshima nzuri maana tumemjua toka 2014. Tukamshauri Masudi kwanini asiishi na huyu mdada??? Aisee alituwashia moto akatutenga kama mwezi hivi haonani na sisi, wazazi wake pia aligombana nao kwa kushauriwa amuoe huyo binti akidai kwamba sio type yake hana vigezo vya mwanamke anayetaka kuishi nae.

Kuna siku tumetoka Mbudya kuogelea tukarudi usiku tupo tukaka kaa Water World hadi saa6 usiku tupo matingasi balaa tukafika anapoishi mzazi mwenzake jamaa akasema analala pale, sisi tukasepa Masudi akafanya yake bidada akadaka tena ujauzito mwaka jana kajifungua mtoto mrembo saaana wakike.

Masudi anadai demu wake huwa anamtega ndio mana kila akikutana nae anashika mimba ila watoto wakizaliwa wanamuumbua kwa kufanana nae saana. Yaani ikitokea tupo sehemu Shemeji akaja yaani jamaa atapoteza mood hadi demu aondoke yupo tayari kumpa hela aende akanywe sehemu nyingine au yeye ahame kijiwe.

Sasa ana watoto wawili na huyo mwanamke amemnunulia fanicha za ndani ila hataki kuishi nae yeye anaishi kwenye nyumba yake peke yake na bidada na wanawe wanaishi alipowapangia anadai atamnunulia kiwanja na kumjengea nyumba aishi na watoto wake ila yeye bado anatafuta "soul mate" mwenye vigezo anayovitafuta.

Najua kila mtu huwa anapenda kupata mtu mwenye sifa anazotaka iwe mwanamke au mwanaume baadhi ya vigezo ni kama:
  1. Height
  2. Rangi
  3. Elimu
  4. Uwezo wa kifedha
  5. asiyetumia vilevi vyovyote
  6. anayejitambua
  7. mcheshi'
  8. mwenye mapenzi ya kweli
  9. Mcha Mungu
  10. Dini
  11. Kabila
  12. Muonekano/Mtanashati
  13. NK

Wadau nisaidieni namna ya kumshauri huyu rafiki yetu hajawahi kutueleza hivyo vigezo anayovitaka

Ushawahi kupendwa na mtu ambaye huvutiwi kuishi nae?

NB: TO MOST MEN SEX IS NOT EQUAL TO LOVE

Nawasilisha.
 
So unataka tufanye nini...kila mtu apambane na hali yake...kuowa ni maamuzi ya mtu binafsi...kama imekutach sana nenda kamuowe wewe...
Naoaje Demu wa jamaa yangu?? mbona una matusi ya rejareja
 
Nami sijahoji kuwa humfahamu au lah, ni kweli unamfamu.... na vigezo vya Masudi [kama unavifahamu pia] je huyo manzi anaingia..?
Mkuu mbona unauliza maswali yenye majibu??? nimesema "hajawahi kutuambia vigezo vyake"
 
Masoud hajakua na kuyajua maisha. Hugo dada mshauri awe mvumilivu huyu Masoud ndiyo mume wake ingawa atakuja baada ya kutendwa na soul mate.
Sawa mkuu, ngoja tusubiri wanasema "wakati ni mwalimu mzuri"
 
Back
Top Bottom