Tukio ninalomkumbukia mimi ni hili, shule yetu ikiwa inazinduliwa akaalikwa Kanali awe mgeni rasmi, akafika pale, shughuli zinaendelea, kila mmoja anafurahia kua eneo lile. Mkuu wa shule alikua mwenyekiti wa CHANETA kwahiyo Kanali kuwepo haikua big deal, kwa influence yake hadi ITV na Channel Ten walikuepo.
Basi bwana shughuli inaendelea pale ghafla tunasikia mvumo, wazia ile zzzZZZzzz, muda huo Kanali anatoa mawili matatu.
Ebwana kumbe ni nyuki. Walivamia lile tukio ikawa mshikemshike kila mtu anatafuta pa kukimbilia. Watu wengine miyeyusho wanakimbilia madarasani.
Madarasa ambayo madirisha ni nondo.
Kanali kayeya, kila mtu kashika lwake.
Baada ya pale sikumsikia tena mpaka leo.