TANZIA Kanali Fabian Massawe, aliyekuwa RC Kagera afariki dunia

R.I.P namkumbuka alivoendesha oparetion za kupambana na majambazi wa mapori ya Burigi na Kimisi, akaleta ahueni ya matukio ya utekaji na ujambazi uliokuwa ukiendelea huko.
R.I.P Massawe.
Hakuwa na dharau. Nakumbuka siku moja tulikuwa naye tukipokea msaada kutoka Balozi wa Belgium.
 
Nishawahi kutana nae miaka ya nyuma akiwa Rc. Kwetu. Mtu peace sana. Apumzike kwa amani.
 
Raha ya milele umpe Eee Bwana. Apumzike kwa amani
 
Pumzika kwa amani Mzee wetu

NB: huyu mbona hatukanwi na kuombewa mabaya na BAVICHA?
 
Tukio ninalomkumbukia mimi ni hili, shule yetu ikiwa inazinduliwa akaalikwa Kanali awe mgeni rasmi, akafika pale, shughuli zinaendelea, kila mmoja anafurahia kua eneo lile. Mkuu wa shule alikua mwenyekiti wa CHANETA kwahiyo Kanali kuwepo haikua big deal, kwa influence yake hadi ITV na Channel Ten walikuepo.

Basi bwana shughuli inaendelea pale ghafla tunasikia mvumo, wazia ile zzzZZZzzz, muda huo Kanali anatoa mawili matatu.

Ebwana kumbe ni nyuki. Walivamia lile tukio ikawa mshikemshike kila mtu anatafuta pa kukimbilia. Watu wengine miyeyusho wanakimbilia madarasani.

Madarasa ambayo madirisha ni nondo.

Kanali kayeya, kila mtu kashika lwake.

Baada ya pale sikumsikia tena mpaka leo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…