Kanali Martini Mkisi kweli maisha ni gwaride

Myala ni full colonel halafu nilikuwa sijui kuwa yuko peace sana maana kuna dogo katoka RTS juzi kati ananisimulia kuwa Myala nae ni mnaa
Labda wasio mjua ,,madogo waliojenga ukuta ,chamwino,na ukonga walitumuliwa pale RTS mpaka huruma ilihali walipewa zawadi ya ajira na raisi kisa unfit ambao umetokana na kazi ngumu walizofanya
 
Ukitaka heshima sababu ya umri wako subira tukivua gwanda na tukikitana uraiani .huko tutazungumza Kama raia wa kawaida

Ukiona afisa analeta ujuaji Hadi kitaa Tena bila gwanda ujue kichaa tu huyo anataka misifa ya kijinga Ila wengi wao wanajielewa .

Ila Sasa ukiwa ndani ya viunga vya jeshi Ni kutii amri bila kuuliza kuhusu umri wako Ni 10th option ,[emoji3]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa bhana nitasemaje sasa na elimu sina nimeishia lasaba....
 
Unasemaje mtu chini ya meja Hana madhara

Unaikumbuka kisa cha akina kapteni hanspope

Ukishakuwa afisa una amri mengine yote yatategemea

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivyo vyeo kama Captain kwanza nani anakujua? Kepteni jina linatisha kwa ambao hata jeshi hawalijui

Vigogo jeshini ni Makanali kwenda juu
 
Mambo ya wanasiasa hayo

Ndio tatizo la mifumo ya huku dunia ya tatu, Vyeo anatakiwa kupewa mtu kutokana na uzoefu pamoja na umahiri binafsi na si nje ya hapo na sio kwa sababu amiri jeshi mkuu anapenda iwe vile

Jk watu walimchukia sana licha ya kulijua jeshi alikuwa akipandisha vizuri tu wanasema anahonga vyeo ili asipinduliwe
 
Afande saameja tuliza munkar

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mi naweza kumzingua kama analeta dharau halafu nitajibiaga mbele
 
Wanazingua sana

Wastaarabu wapo utakuta ye hana mna wa kukimbizana na askari au juniors yupo camp unakuta yuko bize na mawasiliano ya mambo yake hana mambo ya kijinga jinga yakunyanyasa wa chini Siku nyingine asubuhi kasaini huyoo anasepa inategemea na CO yukoje au hayupo

Ila wanaa unakuta anataka anyenyekewe kama Mungu wakati shida nao wanazo unakuta meja anakuja kukopa kwa Pte mshahara ukiisha kabla
 
Sijui uelezwe mara ngapi , na inakuwaje uwe unalalamikia sana cheo cha Mbuge kuliko wengine walioteuliwa kwa njia hizo hizo. Vipi unamfahamu binafsi au mliwahi kutambiana huuko nyuma mkiwa ngazi moja na sasa yeye ameruka mbali sana ambako hutafika au jamaaa yako hatafika? Halafu nimekusoma post zako nyingi hapa kwenye topic hii ni za hisia kuliko facts. Siku moja ulisema kuwa Nyerere alipandisha maofisa kwa upendeleo lakini hukutoa ushahidi wowote. Mimi ninajua kuwa wakati Nyerere anaondoka kulikuwa na majenerali wasiofika 10 ambapo karibu wote walikuwa wamepigana Uganda isipokuwa Hashim Mbita na Sarakikya tu. Ila uliweka blanket statement kuwa alipandisha watu kwa upendeleo bila kuwa na ushahidi wowote. Vyeo vya chini kuanzia 2nd Lt had Lt.Col siyo uteule wa rais bali yeye ni rubber stamp tu; uteuzi wake ni kuanzia Col kwenda juu. Kwa hiyo katika hao majenerali alioacha pamoja na mabrigedia kama 25 hivi ambao wengi wao walikuwa wamepigana vitani Uganda au Musumbiji au Zimbabwe au walikuwa na madakatari hukutoa ushahidi wa wapi Nyerere alipendelea. Sasa hivi unasema kuwa Kikwete hakupandisha watu wakati kuna mwaka 2013 Kikwete alipandisha majenerali zaidi ya 30 kwa wakati mmoja, na kati ya hao wengine pia walikuwa wamekwenda haraka namna hiyo hiyo hiyo ya Mbuge.

Kama una tatizo na Mbuge binafsi, nakushauri uwe unasali sala hii mara kwa mara:

" Eeh Mwenyezi Mungu, nakuomba unipe utulivu wa moyo kuweza kukubaliana na nisiyoweza kubadili, unipe ushujaa wa kubadili ninayoweza, na unipe busara ya kujua tofauti kati ya ninayoweza kubadili na nisiyoweza"

Sali sana ili uondokane na malalamiko haya ambayo hayakupeleki popote na hayabadili chochote kuhusu Mbuge zaidi ya kuendelea kukuumiza moyo tu.
 
Naona Kama inakuuma sana [emoji3][emoji3][emoji123]

Usilie kamanda ...ngangamara[emoji1787][emoji1787][emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kisa kakupinga ndo maana unaona inamuuma. Tangu nisome historia ya kijeshi sijwahi kuona kamanda yeyote wa miaka 30+ na early 40 akifanya maajabu kama hana experience. Ukisoma list ya WW2 mfano, Wehrmacht (jeshi la Nazi) lilikuwa na majenerali na Field Marshall wenye uzoefu na WW1 na umri wao miaka 40+ na 50+ uko. Kina Goeling, Heinz Gudelian, Desert Fox, Rundstedt, Kesselring na wengine wengi sana hawakuwa matoto madogo. Walikuwa watu wenye experience zao na hata Adolf Hitler alipigana WW1.

Britain walikuwa na PM wao mzembemzembe ambaye hakuwahi shiriki vita, nchi ilimshinda ikabidi wamchague Winston Churchill ambaye alishiriki WW1. Ukitaka kuona vita inataka experience, Churchill alipomaliza vita tu alishindwa uchaguzi mkuu kwakuwa hakuwa anajua chochote kuhusu uchumi wala maendeleo, still anarank top 3 ya PMs bora kwa Waingereza. Bado majenerali wao kina Montgomery hawakuwa watoto.

France hawa ndo mfano wa jeshi la kisiasa, walichaguliwa kipuuzi kabisa na Ujerumani ilipovamia wakakimbia mapigano. Majenerali walikuwa wapuuzi tu, mpaka badae msaada wa Mwingereza kina de Gaulle ndo wakaja kuipigania nchi. Hawa hawakuwa wa kisiasa wala watoto.

USA wao hawakuwa na experience na vita kumbuka WW1 hawakuhusika. Majenerali wao kina Omar Bradley na McArthur waliteseka kwanza ingawa tech iliwabeba mno, sana.

Kwa Warusi, huyo Stalin alifanya purges miaka ya 1930s akaondoa viongozi muhimu walioshiriki WW1 akaweka wale wa ndio mzee. Kilichotokea mwanzoni kwa vita tunakijua, Germany ilikuwa inawapiga kama watoto. Baadae ndo watu wenye experience zao na umri mkubwa kina Georgy Zhukov na Konstantin Rokossovsky walikuja kuwa game changer.
Uliona majenerali wa Japan, kina Admiral Yamamoto na Admiral Yamaguchi. Hawakuwa watoto wa kubebwa, walikuwa watu wenye experience sana.

Wewe ushawahi ona wapi majenerali wasio na uzoefu wanafanikiwa kwa kawaida. Kule Nigeria watoto ndo walikuwa wanawaza mapinduzi na ilipotokea Biafra ndo wakaonekana maandazi kabisa. Walikuwa wanapigwa na vijeshi vya kurecruit kutoka kirabuni.
 
Bye bye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…