Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Waaai

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2021
Posts
1,293
Reaction score
2,642
Imagine wewe ni laiser/Msuya/Mchome/Sumaye halafu unasikia mtu analeta mada ya Nothern zone huku akifikiri ukiongelea Nothern zone unaongelea Moshi/Wachaga.

Kuna baadhi ya watu mnawakuza sana wachaga kila zinapoletwa mada za Nothern zone ilihali ni sehemu tu ya watu wa kaskazini.

Ukiongelea kaskazini unaanzia Tanga kama sikosei(Nirekebishwe kama sipo sahihi) mpaka babati kwenye mbuga za wanyama huko. Umasaini kwa kina laiser, Endasaki kwa kina sumaye, upareni kwa kina Mndeme, n.k

A blessed region.

Kuna watu mnawafanya watu wa maeneo mengine wafikiri Kaskazini ni uchagani. Wachaga ni sehemu tu ya ardhi ya Kaskazini na wamejikita zaidi kwenye biashara ndogondogo,za kati na wengine biashara kubwa.

Wapo pia omba omba, walevi, wezi, vibaka na matapeli kutoka moshi kilimanjaro.

Ukiongelea matajiri wa kaskazini watu watapeleka mawazo yao kwa wachaga lakini ukienda umasaini utakutana na matajiri wakubwa sana wenye ranch za ng'ombe na tenda za kulisha jeshi miaka na miaka hutawasikia,

Hanang kuna watu wana mashamba ya Alizeti ekari za kutosha, mahrvest combiner na matrekta makubwa na magodown makubwa ila hutawasikia.

Ukienda mererani kuna mabilionea wa kimasai, walikuwepo kina msuya(RIP), n.k n.k

Sasa mchaga mwenye duka la kileo, guest house, nyumba ya kupangisha na prado mchaga hapo Arusha mjini ndo atatolewa mfano wa matajiri wa kaskazini.

Wachaga kama walivyo makabila wengine ni watu safi sikatai, wachapa kazi na wengi wao wanapenda biashara. Ila kufikiri nothern zone ni Moshi kwa wachaga ni kupotoshwa, Uchagani ni sehemu tu ya Nothern zone.

KANDA YENYE MCHANGO MKUBWA SANA KWENYE UCHUMI WA TANZANIA.
 
Ishu ni kwamba hata hao kina Mvungi, Msuya, Sabuni, Minja, Mjema, Mnzava na wengine huona fahari sana kutambuliwa kama Wachaga. Wachaga ndio wamefanya kukaonekana kuko "blessed"
Hawa wa aina hii sijawahi kutana nao. Yaani mpare afurahie kuitwa mchaga? Au laiser afurahie kuitwa mangi?
 
Kuna watu hawajui Kuna tofauti kubwa sana kati ya watu wa huku hawajui Kuna wachaga ,wasambaa,wambulu,wapare ( tena mwanga na usangi)wambunghu,waarusha ,wameru,nk wao huona kila MTU ni mchaga
Si ndio. Yaani sijui hii notion imetokanana na nini.
 
Siyo kila eneo inapata umaarufu kwa watu wake wote....huku Wanyantuzu ni balaa mchaga haoni kitu tembea uone.
 
Ishu ni kwamba hata hao kina Mvungi, Msuya, Sabuni, Minja, Mjema, Mnzava na wengine huona fahari sana kutambuliwa kama Wachaga. Wachaga ndio wamefanya kukaonekana kuko "blessed"
Si kweli hata kidogo..Tena wengi huona umewakosea ukiwadhania ni jamii nyingine..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Siyo kila eneo inapata umaarufu kwa watu wake wote....huku Wanyantuzu ni balaa mchaga haoni kitu tembea uone.
Boss unachosema ni kwamba kanda ya kaskazini ni maarufu sababu ya wachaga?

Serengeti, manyara, tarangire, milima ya upareni, mbulumbulu, masai mara, ngorongoro, mapango ya tanga n.k ni maarufu sababu ya uwepo wa wachaga? Kama ndicho ulichomaanisha ww ni mpotoshaji.
 
sina maana hiyo
soma taratibu Mkuu..
 
Si ndio. Yaani sijui hii notion imetokanana na nini.
Acha chuki binafsi ...afu vitu vingi kuhusu northern zone hujui ...Kwenye mada yako umejichanganya hatari..... Mpaka unaomba kurekebishwa kama uko sahihi but lengo lako ni kuwazima wachaga ...poor you ...
 
Boss unachosema ni kwamba kanda ya kaskazini ni maarufu sababu ya wachaga?

Serengeti, manyara, tarangire, milima ya upareni, mbulumbulu, masai mara, ngorongoro, mapango ya tanga n.k ni maarufu sababu ya uwepo wa wachaga? Kama ndicho ulichomaanisha ww ni mpotoshaji.
Mkubwa we kweli kiande nan kakuambia serengeti iko kaskazini .... Acha kukurupuka
Fanya research ndo uje kukosoa wachaga
 
Acha chuki binafsi ...afu vitu vingi kuhusu northern zone hujui ...Kwenye mada yako umejichanganya hatari..... Mpaka unaomba kurekebishwa kama uko sahihi but lengo lako ni kuwazima wachaga ...poor you ...
Hapo nilipoomba nirekebishwe kama nimekosea na hayo niliyokosea hujayarekebisha.

Sina tatizo na wachaga, nina tatizo na upotoshaji kuwa ukizungumzia kaskazini umezungumzia moshi/wachaga. Wachaga ni sehemu tu ya kaskazini.
 
Mkubwa we kweli kiande nan kakuambia serengeti iko kaskazini .... Acha kukurupuka
Fanya research ndo uje kukosoa wachaga
Sema ipo wapi hutapoteza lolote...
 
Back
Top Bottom