Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Imagine wewe ni laiser/Msuya/Mchome/Sumaye halafu unasikia mtu analeta mada ya Nothern zone huku akifikiri ukiongelea Nothern zone unaongelea Moshi/Wachaga.

Kuna baadhi ya watu mnawakuza sana wachaga kila zinapoletwa mada za Nothern zone ilihali ni sehemu tu ya watu wa kaskazini.

Ukiongelea kaskazini unaanzia Tanga kama sikosei(Nirekebishwe kama sipo sahihi) mpaka babati kwenye mbuga za wanyama huko. Umasaini kwa kina laiser, Endasaki kwa kina sumaye, upareni kwa kina Mndeme, n.k

A blessed region.

Kuna watu mnawafanya watu wa maeneo mengine wafikiri Kaskazini ni uchagani. Wachaga ni sehemu tu ya ardhi ya Kaskazini na wamejikita zaidi kwenye biashara ndogondogo,za kati na wengine biashara kubwa.

Wapo pia omba omba, walevi, wezi, vibaka na matapeli kutoka moshi kilimanjaro.

Ukiongelea matajiri wa kaskazini watu watapeleka mawazo yao kwa wachaga lakini ukienda umasaini utakutana na matajiri wakubwa sana wenye ranch za ng'ombe na tenda za kulisha jeshi miaka na miaka hutawasikia,

Hanang kuna watu wana mashamba ya Alizeti ekari za kutosha, mahrvest combiner na matrekta makubwa na magodown makubwa ila hutawasikia.

Ukienda mererani kuna mabilionea wa kimasai, walikuwepo kina msuya(RIP), n.k n.k

Sasa mchaga mwenye duka la kileo, guest house, nyumba ya kupangisha na prado mchaga hapo Arusha mjini ndo atatolewa mfano wa matajiri wa kaskazini.

Wachaga kama walivyo makabila wengine ni watu safi sikatai, wachapa kazi na wengi wao wanapenda biashara. Ila kufikiri nothern zone ni Moshi kwa wachaga ni kupotoshwa, Uchagani ni sehemu tu ya Nothern zone.

KANDA YENYE MCHANGO MKUBWA SANA KWENYE UCHUMI WA TANZANIA.
Yaani katika upuuzi ambao naushangaa ni huu sasa asiejua kuwa kanda ya kaskazini yanatoka hayo makabila ni nani?

Labda kama unazungumzia wakenya huko sawa ila hakuna Mtanzania asiejua makabila yanayotokea kaskazini kusema tu kuwa eti watanzania wanajua kabila linalotokea kaskazini ni wachaga tu basi utaKuwa unaanza kudata, sababu hakuna asiewajua wamasai, wapare, wameru mpaka wabarbaig sababu tunaishi nao hata huku tulipo.

Labda uje na mada nyingine ila hii perception endeleeni kujidanganya
 
Hahaha ok mkuu🤣🤣

Je voundrais que vous nous en dire plus a ce

Sasa unaonaje hii hoja ukiiandika kwa kifaransa maana umeishi nao ili wasioamini wathibitishe uhalali wa hoja yako.
Hahahahaaaaa bahati mbaya JF hamna jukwaa la Wafaransa.... Nitakuwa najiongelesha tu kama twitter
 
yaani katika upuuzi ambao naushangaa ni huu sasa asiejua kuwa kanda ya kaskazini yanatoka hayo makabila ni nani? labda kama unazungumzia wakenya huko sawa ila hakuna mtanzania asiejua makabila yanayotokea kaskazini kusema tu kuwa eti watanzania wanajua kabila linalotokea kaskazini ni wachaga tu basi utaiuwa unaanza kudata, sababu hakuna asiewajua wamasai, wapare, wameru mpaka wabarbaig sababu tunaishi nao hata huku tulipo. labda uje na mada nyingine ila hii perception endeleeni kujidanganya

Yaweza kuwa ni ujinga kweli ila si uongo....
Kuna Watanzania wamekulia Dar es Salaam hata hawajui kaskazini ni wapi achilia mbali makabila yaliyopo huko. Wao wanajua huko kaskazini kuna wachaga.

Wapo wengine hawajui Kuwa wambulu na wachaga wote ni kanda ya kaskazini.

Kwasababu ww unafahamu au wengi wanafahamu haimaanishi kuwa wote wanafahamu.
 
Unaposema Wamasai, ni kabila. Lakini wachaga si kabila. Nyerere ndio alilazimisha wachaga liwe kabila ( Putin na Ukrein). Wachaga ni taifa. Labda twende na muelekeo huo ndio tutajua kwanini Kaskazini ni wachaga.
 
Unaposema Wamasai, ni kabila. Lakini wachaga si kabila. Nyerere ndio alilazimisha wachaga liwe kabila ( Putin na Ukrein). Wachaga ni taifa. Labda twende na muelekeo huo ndio tutajua kwanini Kaskazini ni wachaga.
Acha upotoshaji, Kaskazini si wachagga tu..
Na kama suala la Kanda, ndio kabisa..hata Tanga ni kaskazini

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Labda tu niongezee kitu kimoja ama viwili kwa wale wasioelewa juu ya hawa jamaa zetu wachaga
I. Ni watu wa kupiga kelele za kujivuna
Kwa taarifa yako mfano hapa Arusha Kuna matajiri ambao sio wachaga ila wamenyamaza kimya
Natoa mfano namba moja Mzee anaitwa Bajuta huyu ni Muiraq (Mmang'ati
Huyu ndio Tajiri Arusha nenda TRA , Bank kuu, au Au uliza Serikali itakueleza
Marehemu Jiwe mwenyewe alimshindwa.

Domell ...Huyu ni Mang'ati mwingine

Laizer ...Huyu Masai ni hatari bado

Lowasa.. Former prime minister

Mzee Mbise ... Bado hakuna mchaga aliyewekeza hata kwa kiwango Cha Mzee Mbise huyu mwenye Mahotel ya Meru House, Arusha center inn, Arusha Tourist inn, logdes kama sarafina , Meru deluxe, nk
Magorofa mengine huko Tengeru nk...

Kuna Masai wanapesa balaa kwenye industry ya Tanzanite


Wachaga wako organized kwa kukopeshana

So wanaenda kama teamwork kwenye level yao flani tu

Hawa kina Aquiline Hotel , rich Hotel ukiwajumlisha pamoja unapata hotel moja ya SG Resort ya marehemu bilionea Msuya Hadi Leo

Tatizo mchaga akipata kidogo anapiga kelele sana Kuna watu wametulia wanahela balaa

Ndio maana Magufuli aliwapitia sana sababu ya makelele yao na bado akakuta hawana chochote

Walishindwa hata kumsaidia Lema ( Elerai construction) bilioni Saba alikuwa anadaiwa Hadi akaenda jela

Hawa ni mdomo tu hawana lolote
 
Umeongea kishabiki sana mim nimezaliwa Moshi Ila sipendi kujitambulisha kama nimetokea kule kwa sababu wachaga ni wabaguzi kama wewe siko proud kujitambulisha nimezaliwa Moshi kwa sababu wachaga wanaamin hata ukizaliwa Moshi as long wewe sio mchaga basi wewe kwenu sio Moshi
Huwezi kuwa proud kwa kuwa huna sifa za kuwa mchaga. Kuzaliwa Moshi au kama mama yako aliolewa Moshi akiwa ameshakuzaa na mwanaume mwingine hakuna namna unaweza kuwa Mchaga... Wewe ni Chasaka..
 
Sijawah kutaman kuwa mchaga na hakuna sehemu niliyosema nataman kuwa mchaga, mim nimekaa na wachaga sijawahi ona huo uspecial unaongelea point ni kwamba wachaga ni wabaguzi kama walivyo wazungu wanabagua waaafrika, tofauti ni kwamba ni mwafrika anayebagua waafrika wenzake na Hana uspecial wowote
Wewe huoni kwa kuwaonea kwako wivu hadi unawaita wabaguzi ndio uspecial wenyewe?
 
Acha upotoshaji, Kaskazini si wachagga tu..
Na kama suala la Kanda, ndio kabisa..hata Tanga ni kaskazini

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
Tanga itoke kabisa kwani hata ule mtihani wa kanda sidhani kama unafanyika sasa wa northern east maana wakifanya na Kilimanjaro lazima mitihani ivuje na inaanzia huko ni muda naona kama kanda ikafutwa

Sasa sijui hapo waliwagawa kwamba tanga haipo kanda iyo au
 
Wewe huoni kwa kuwaonea kwako wivu hadi unawaita wabaguzi ndio uspecial wenyewe?
Ni wabaguzi hawakuwafanyi kuwa special mfano wewe unatabia za kibaguzi hakukufanyi kuwa special, ubaguzi ni ujinga ndo maana kila Mahalia unapigwa vita mfano uko kwenye mikoa mingine mngekua mnatreatiwa vibaya kama mnavyotreat watu ambao sio wachaga Ila wamezaliwa na kukulia Moshi unafikiri ingekuaje na hii ndo sababu Nyerere aliwadis ni wabinafsi sana yule Babu aliona mbali sana kuhusu wachaga na hakukosea
 
Najua wachaga si kabila kama wambulu.
Wewe ni mchaga?

Well kama ndio basi si kila sifa ya kuifurahia unajua kwann hii notion ya kaskazini ni wachaga ni mbaya?

Mtu unahukumiwa just sababu ya notion isiyo na uhalisia.....

Baada ya ufisadi kwenye interview panel ya kujaza nafasi member alipendekeza wa kumwajiri ila ni mkazi wa Arusha, then akatokea board member akasema watu wa kaskazini hao ni wachaga tupu na wezi tu Halafu mwenye tuhuma za wizi na kusimamishwa ni mpare si mchaga ila wote wakazi wa Arusha.


HII SI SAWA. UTAJIKUTA MAMBO YA WIZI YOTE YANAHUSISHWA NA WACHAGA HATA KAMA SI MCHAGA ALIYEFANYA, HII INACHANGIWA NA NOTION KUWA KASKAZINI NI WACHAGA.
Una mangamanga tu huna hoja,watu wenye akili za kimaskini lazma wawapige majungu wapambanaji hiyo ni common
 
Kwanza ujue kuna 1. Kabila kubwa 2. Kabila Maarufu na 3. Kabila linaloheshimika.

Ukienda kanda ya ziwa utakuta Wasukuma ndio kabila maarufu na pia kabila kubwa. Ila kwa kanda hiyo kabila linaloheshimika ninaweza kusema ni Wahaya.

Kwa kanda ya Kaskazini Kabila maarufu ni Wamasai, Kabila kubwa (kwa idadi ya watu) ni Wairaq na Kabila linaloheshimika ni Wachaga.

(JAPO WACHAGA SIO KABILA)
Wachaga wanaheshimika kwa kuwa ndio Jamii ambayo iko "organized" kuliko jamii ingine yeyote Tanzania.

Umeuliza kwa nini inaonekana "WACHAGA" wanaibeba kaskazini?

Jibu rahisi tu ni kuwa kwa upende wa Kaskazini ni maeneo wanayoishi "WACHAGA" peke yake ambayo yalikuwa na maendeleo ya hali ya juu hususani sehemu za vijijini. Kwa leo hii ukiambiwa kuwa Hospitali ya KCMC iko ndani ya Wilaya ya Moshi Vijijini tena Tarafa ya URU utakataa kwa nguvu zako zote.

Karibia kama siyo theluthi ya shule zote za sekondari za Tanzania zinapatikana Kilimanjaro maeneo wanayoishi Wachaga. Ni nadra sana kutembea zaidi ya Km 5 bila kukuta Shule ya sekondari kwa maeneo haya.

Hali ni tofauti kwa maeneo ya upareni.... Utakuta shule kwa wastani wa kila baada ya km 15 hadi 20 kwa maeneo ya kijijini na kwa mjini walau km 7 mpaka 10. Kama mtu anajua umbali wa Shule ya sekondari Vunta mpaka ya Kirangare atasema nasema ukweli.

Maeneo wanayoishi wachaga yana taasisi kubwa hata vijijini na sehemu kubwa imefanywa kwa juhudi za wananchi wenyewe. Kuna mahospitali makubwa yaliyoanzishwa zamani sana kama vile Kibosho Hospital, Kibong'oto (maarufu kwa kifua kikuu), Machame Hospital.... Adhani ina miaka kama 110 au zaidi.... Hospitali ya Kilema... Ilianzishwa miaka ya mwishoni mwa karne ya 19 (1890s)..,Hospitali ya Marangu.... Hospitali ya Huruma iliyopo Rombo.

Sitaongelea barabara za lami zinazoelekea Sanya Juu, Masama, Machame, Kibosho Umbwe, Mbokomu, Kibosho Mweka, Kibosho Kirima, marangu hadi Kilema (kwa sasa inazunguka mpaka kwa Lazari)... Kwenda Kirua Vunjo kupitia Kongo, barabara ya kupandisha Uchira, Old Moshi hadi ilipokuwa shule ya Kolila zamani, marangu mtoni hadi marangu gate, rombo kupitia Mwika.... Naona nikiendelea nitawaabisha tu watani.

Unaachaje kubebwa na mtu mwenye Chuo kikuu cha KCMC, MWENGE, SIMUKO, Chuo cha Wanyamapori Mweka (Tanzania vipo 2 tu na hiki ndio kilikuwa pekee kwa Afrika mpaka miaka ya 2000) Marangu TTC, Mandaka TTC, Singachini TTC, vyuo vya uuguzi KCMC, Machame, Kibosho nk.

Naona niache kutaja shule kama Umbwe, Lyamungo, Kibosho Girls, Machame Girls, Weruweru, St. JAMES' seminary (1925), Uru seminary.... Maua Seminary au basi Ashira Girls... Wengine wakati wanakazana kupokea mahari WACHAGA walikuwa wakijenga shule kwa ajili ya watoto wao wa kike... Unaachaje kusema wanabeba Kaskazini?

Turudi kwenye maendeleo binafsi... Wewe binafsi kama kweli hauna chuki na wachaga utakubali kuwa ndio Jamii pekee kwa TANZANIA NZIMA na sio Kaskazini tu ambapo hauwezi kukuta nyumba ambayo haijaezekwa kwa bati yata kama ni kule kibosho "Ntudu" au Mahoma - Old Moshi.

Pia ndio sehemu ambayo watu hawajisaidii machakani au kwenye choo cha shule kama wapare.... Utakuwa shahidi yangu kama unamjua mchaga kuwa hata kama anaishi sehemu ya mbali na Kilimanjaro utamjua kwa haraka bila kuambiwa kwa kuona nyumba yake tu kwani itakuwa tofauti na ya wenyeji... (standing out). Na "mchaga" asipokuwepo sehemu basi jua wazi hiyo sehemu hakuna maendeleo. Wengi ni "ULTIMATE OPPORTUNISTS".

Kwa mumalizia jibu hili fupi hebu niambie kama huko Kaskazini ni Wapare (Wasu), Wairaq au Wamasai wapi huwa wana"flock" kurudi nybani kwa likizo (VACATION) kama wazungu wengine wafanyavyo kipindi cha majira ya joto?

Sio wapare huwa wanajifanya kuwa na wao ni kina Mangi wanafuata Wachaga kurudi Moshi na wanaishia Hedaru kisha wanarejea maana hawajajenga kwao?

Tuanze na majibu haya kwanza.
Jibu atakuwa kalipata
 
Back
Top Bottom