Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Kanda ya Kaskazini si Moshi kwa wachaga tu

Serengeti iko katkati ya Arusha na mara But sehemu kubwa ya Serengeti iko mkoa wa Mara ambayo n Lake zone ....
Hata kama Serengeti ingekuwa ipo Mara na si katikati ya Arusha na Mara bado ingeendelea kuwa Kaskazini, Arusha ipo Kaskazini Mashariki mwa Tanzania na Mara ipo Kaskazini Magharibi mwa Tanzania. Kama si geographical feature (Ziwa Victoria) hiyo mikoa inayoitwa ya Kanda ya Ziwa ingekuwa inatambulishwa kama Mikoa ya Kanda ya Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.

Sema tu ni kwa bahati mbaya sana kwamba ukisema Kanda ya Kaskazini basi moja kwa moja watu wanajua kuwa unazungumzia Kaskazini Mashariki inayojumuisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Tena wengine Tanga haiwajii kichwani.

Wachaga ni kabila la pili kwa ukubwa Tanzania na lina wingi wa historia pengine ndo maana ukizungumza Kaskazini linakuwa ndilo kabila linawajia watu kichwani. Lakini pia kuna Wamasai ambao pia ni kabila maarufu sana si tu Tanzania bali Afrika pia na duniani (kwa wale watu wachache wanaofuatilia historia ya Afrika), ndilo kabila linafuata kwa kuwajia watu kichwani pindi Kaskazini izungumziwapo. Ukimuambia mtu unatoka Kaskazini atakuambia "Wewe ni Mchaga eeh?" Ukimkatalia atakuuliza ni Masai? Yote hayo yanatokana na ukubwa wa historia ya makabila hayo.

Lakini Kaskazini ina Makabila mengine;

Wachaga
Wamasai
Waarusha (Wamasai koko)
Wameru
Wapare
Wasonjo
n.k

Kuhusu umiliki wa Uchumi hapana shaka kabisa kwamba uchumi wa Kaskazini unamilikiwa na Wachaga pengine wakifuatwa na Wamasai kama tukilinganisha kwa uwiano.

Ni kanda ambayo watu wake ni Wajamaa sana tena kuwazidi hata Wasukuma wanaosifika kwa Ukarimu.

Ujamaa wao pamoja na kwamba haushii tu kwa wao peke yao bali na kwa wengine pia wanaokutana nao ndo jambo ambalo linawafanya waonekana ni watu wa kujaliana wenyewe.
 
Upo sahihi, ila naona kama ni sahihi zaidi kuwakilisha KLM na si Kaskazini yote.

Kuhusu kutapakaa wapo pia mpaka pwani na DSM si Arusha na sehemu nyingine za kaskazini tu, wafanyabiashara wengi ni watu kutoka uchagani. Mchango wao ktk biashara unajulikana ila uwakilishi wa kaskazini ni kuovarate na overate yoyote inawapa sifa mbaya pia maana unabeba mabaya yote ya tabia za kanda ya Kaskazini pia na si sifa nzuri tu.

SASA HIVI IKITOKA TAARIFA YA MWIZI YOYOTE KUTOKA NOTHERN ZONE AKILI INAKUJA MCHAGA HATA KAMA SI KWELI.

NA MSAADA WOWOTE ANAYEHITAJI MTU WA KASKAZINI MCHAGA NJE YA JAMII YAKE HITIMISHO NI HUYO NI MCHAGA ANA NDUGU ZAKE NI MATAJIRI WANA MADUKA WAKATI WAPO WACHAGA WAMEJICHOKEA TU.
 
Chasaka = mtu asiyekuwa Mchagga.
Hata baadhi ya makabila/mataifa mengine yanatofautisha pia wenyeji na wageni.
Mf:
Wasukuma, wanasema "makabila" - mtu wa mataifa/wakuja
Wahaya, wanasema "nyama(hanga)
  • mtu wa mataifa(hanga), wakuja
  • Ha-goyim, gentile, alien - Wayahudi.
Shukran
 
Wanyakyusa tunawaita "wajanga" akiwa mmoja ni "mjanga"
Chasaka = mtu asiyekuwa Mchagga.
Hata baadhi ya makabila/mataifa mengine yanatofautisha pia wenyeji na wageni.
Mf:
Wasukuma, wanasema "makabila" - mtu wa mataifa/wakuja
Wahaya, wanasema "nyama(hanga)
  • mtu wa mataifa(hanga), wakuja
  • Ha-goyim, gentile, alien - Wayahudi.
 
Kwanza ujue kuna 1. Kabila kubwa 2. Kabila Maarufu na 3. Kabila linaloheshimika.

Ukienda kanda ya ziwa utakuta Wasukuma ndio kabila maarufu na pia kabila kubwa. Ila kwa kanda hiyo kabila linaloheshimika ninaweza kusema ni Wahaya.

Kwa kanda ya Kaskazini Kabila maarufu ni Wamasai, Kabila kubwa (kwa idadi ya watu) ni Wairaq na Kabila linaloheshimika ni Wachaga.

(JAPO WACHAGA SIO KABILA)
Wachaga wanaheshimika kwa kuwa ndio Jamii ambayo iko "organized" kuliko jamii ingine yeyote Tanzania.

Umeuliza kwa nini inaonekana "WACHAGA" wanaibeba kaskazini?

Jibu rahisi tu ni kuwa kwa upende wa Kaskazini ni maeneo wanayoishi "WACHAGA" peke yake ambayo yalikuwa na maendeleo ya hali ya juu hususani sehemu za vijijini. Kwa leo hii ukiambiwa kuwa Hospitali ya KCMC iko ndani ya Wilaya ya Moshi Vijijini tena Tarafa ya URU utakataa kwa nguvu zako zote.

Karibia kama siyo theluthi ya shule zote za sekondari za Tanzania zinapatikana Kilimanjaro maeneo wanayoishi Wachaga. Ni nadra sana kutembea zaidi ya Km 5 bila kukuta Shule ya sekondari kwa maeneo haya.

Hali ni tofauti kwa maeneo ya upareni.... Utakuta shule kwa wastani wa kila baada ya km 15 hadi 20 kwa maeneo ya kijijini na kwa mjini walau km 7 mpaka 10. Kama mtu anajua umbali wa Shule ya sekondari Vunta mpaka ya Kirangare atasema nasema ukweli.

Maeneo wanayoishi wachaga yana taasisi kubwa hata vijijini na sehemu kubwa imefanywa kwa juhudi za wananchi wenyewe. Kuna mahospitali makubwa yaliyoanzishwa zamani sana kama vile Kibosho Hospital, Kibong'oto (maarufu kwa kifua kikuu), Machame Hospital.... Adhani ina miaka kama 110 au zaidi.... Hospitali ya Kilema... Ilianzishwa miaka ya mwishoni mwa karne ya 19 (1890s)..,Hospitali ya Marangu.... Hospitali ya Huruma iliyopo Rombo.

Sitaongelea barabara za lami zinazoelekea Sanya Juu, Masama, Machame, Kibosho Umbwe, Mbokomu, Kibosho Mweka, Kibosho Kirima, marangu hadi Kilema (kwa sasa inazunguka mpaka kwa Lazari)... Kwenda Kirua Vunjo kupitia Kongo, barabara ya kupandisha Uchira, Old Moshi hadi ilipokuwa shule ya Kolila zamani, marangu mtoni hadi marangu gate, rombo kupitia Mwika.... Naona nikiendelea nitawaabisha tu watani.

Unaachaje kubebwa na mtu mwenye Chuo kikuu cha KCMC, MWENGE, SIMUKO, Chuo cha Wanyamapori Mweka (Tanzania vipo 2 tu na hiki ndio kilikuwa pekee kwa Afrika mpaka miaka ya 2000) Marangu TTC, Mandaka TTC, Singachini TTC, vyuo vya uuguzi KCMC, Machame, Kibosho nk.

Naona niache kutaja shule kama Umbwe, Lyamungo, Kibosho Girls, Machame Girls, Weruweru, St. JAMES' seminary (1925), Uru seminary.... Maua Seminary au basi Ashira Girls... Wengine wakati wanakazana kupokea mahari WACHAGA walikuwa wakijenga shule kwa ajili ya watoto wao wa kike... Unaachaje kusema wanabeba Kaskazini?

Turudi kwenye maendeleo binafsi... Wewe binafsi kama kweli hauna chuki na wachaga utakubali kuwa ndio Jamii pekee kwa TANZANIA NZIMA na sio Kaskazini tu ambapo hauwezi kukuta nyumba ambayo haijaezekwa kwa bati yata kama ni kule kibosho "Ntudu" au Mahoma - Old Moshi.

Pia ndio sehemu ambayo watu hawajisaidii machakani au kwenye choo cha shule kama wapare.... Utakuwa shahidi yangu kama unamjua mchaga kuwa hata kama anaishi sehemu ya mbali na Kilimanjaro utamjua kwa haraka bila kuambiwa kwa kuona nyumba yake tu kwani itakuwa tofauti na ya wenyeji... (standing out). Na "mchaga" asipokuwepo sehemu basi jua wazi hiyo sehemu hakuna maendeleo. Wengi ni "ULTIMATE OPPORTUNISTS".

Kwa mumalizia jibu hili fupi hebu niambie kama huko Kaskazini ni Wapare (Wasu), Wairaq au Wamasai wapi huwa wana"flock" kurudi nybani kwa likizo (VACATION) kama wazungu wengine wafanyavyo kipindi cha majira ya joto?

Sio wapare huwa wanajifanya kuwa na wao ni kina Mangi wanafuata Wachaga kurudi Moshi na wanaishia Hedaru kisha wanarejea maana hawajajenga kwao?

Tuanze na majibu haya kwanza.
 
Ok mkuu, ila Kilimanjaro ni sawa kuwakilishwa na wachaga ila si kaskani yote.
Hata sisi hatutaki kuwakilisha watu... Tumejikuta tu tuko kanda moja... Ni kama tu Simba wanavyojikuta Ligi moja na Yanga... Sio level yao ila ndio hamna namna...
 
Hata sisi hatutaki kuwakilisha watu... Tumejikuta tu tuko kanda moja... Ni kama tu Simba wanavyojikuta Ligi moja na Yanga... Sio level yao ila ndio hamna namna...
Hahaha.
 
Mkuu usiondoe ukali wa maneno.... CHASAKA maana yake ni mtu wa porini huko.
Chasaka = mtu asiyekuwa Mchagga.
Hata baadhi ya makabila/mataifa mengine yanatofautisha pia wenyeji na wageni.
Mf:
Wasukuma, wanasema "makabila" - mtu wa mataifa/wakuja
Wahaya, wanasema "nyama(hanga)
  • mtu wa mataifa(hanga), wakuja
  • Ha-goyim, gentile, alien - Wayahudi.
 
Ipo Mkoa wa Mara

Kila kanda inabebwa na kabila moja

Kanda ya ziwa wasukuma
Kusini Wamakonde
Nyanda za juu kusini Wanyakyusa

Acha wivu
Kwani katika kanda ya kaskazini wachaga wamechukua asilimia ngapi hadi wabebe kanda nzima
 
Kaskazini inabebwa na wachaga?
Sawa...
Tunajua kanda ya ziwa wasukuma ni wengi, same to makabila mengi kila kanda ndo maana sasa population ya wachaga kanda ya kaskazini ina idadi kubwa kiasi gani kugemeralise kuwa wachaga waiwakilishe kaskazini na wamasai woote wa Arusha? Kilimanjaro sawa ila si Kaskazini.
SINA WIVU NA WACHAGA.
Ndo hapo sasa, labda waseme wamasai kuliko wachaga
 
Ndo hapo sasa, labda waseme wamasai kuliko wachaga
Na hii ya kupenda kuwa wawakilishi wa kaskazini yote si nzuri kabisa kwa hii jamii maana hubebi mazuri tu hata mabaya.

Sijajua wanapendea nn hii sifa.

Wangejikita klm.
 
Na hii ya kupenda kuwa wawakilishi wa kaskazini yote si nzuri kabisa kwa hii jamii maana hubebi mazuri tu hata mabaya. Sijajua wanapendea nn hii sifa. Wangejikita klm.
Mtani usiteseke sana.... Kwa huko nje ya nchi wanajua tu Tanzania kuna Wachaga na Wamasai.... Tunawabeba hata nchi kama nchi.

Ukifika Finland au Ufaransa ukisema umetoka Tanzania utaulizwa Mchaga? Hamna mtu anamjua Mfipa au Myao au sijui Mnyantunzu au Mbarbeig huko Ulaya.

Sijataja Waha maana wataanza ubishi hapa
 
RIPOTI ya hali ya ukeketaji nchini inaonesha kuwa Mkoa wa Manyara ni kidedea kwa kukeketa wasichana nchini.

Taarifa hiyo imetolewa na Msimamizi Mkuu wa vipindi wa Redio hiyo, Emmanuel Likuda wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukeketaji kwa Mikoa ya Kanda ya Kati iliyoandaliwa na Redio ya C-FM ya Jijini hapa jana.

Kwa mujibu wa Tanzania Demographic and Health Survey and Malaria (TDHS) ya 2015-2016, Mikoa inayoongoza kwa ukeketaji ni Manyara (58%), Dodoma (47%), Arusha (41%), Mara (32%), na Singida (31%)

Kampeni hiyo imepewa jina nisitiri nina haki ya kutimiza ndoto zangu,usinikekete,usinipe mimba utotoni ambapo balozi wa kampeni hizo ni Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Diana Exavery maarufu kwa jina la Malaika.

Alisema ripoti hiyo imefafanua kuwa ukeketaji hufanywa kwa asilimia 86 na mangariba au wakeketaji wa jadi na asilimia 25 hukeketwa katika umri wa miaka 13 na zaidi

Haya basi kuanzia sasa hawa wabebe Kanda ya Kaskazini
 
Kuna Kanda ya Kaskazini Kiserekali halafu kuna ya Moyoni.
 
Mtani usiteseke sana.... Kwa huko nje ya nchi wanajua tu Tanzania kuna Wachaga na Wamasai.... Tunawabeba hata nchi kama nchi. Ukifika Finland au Ufaransa ukisema umetoka Tanzania utaulizwa Mchaga? Hamna mtu anamjua Mfipa au Myao au sijui Mnyantunzu au Mbarbeig huko Ulaya. Sijataja Waha maana wataanza ubishi hapa

Hahaha ok mkuu🤣🤣

Je voundrais que vous nous en dire plus a ce

Sasa unaonaje hii hoja ukiiandika kwa kifaransa maana umeishi nao ili wasioamini wathibitishe uhalali wa hoja yako.
 
Back
Top Bottom