Kwanza ujue kuna 1. Kabila kubwa 2. Kabila Maarufu na 3. Kabila linaloheshimika.
Ukienda kanda ya ziwa utakuta Wasukuma ndio kabila maarufu na pia kabila kubwa. Ila kwa kanda hiyo kabila linaloheshimika ninaweza kusema ni Wahaya.
Kwa kanda ya Kaskazini Kabila maarufu ni Wamasai, Kabila kubwa (kwa idadi ya watu) ni Wairaq na Kabila linaloheshimika ni Wachaga.
(JAPO WACHAGA SIO KABILA)
Wachaga wanaheshimika kwa kuwa ndio Jamii ambayo iko "organized" kuliko jamii ingine yeyote Tanzania.
Umeuliza kwa nini inaonekana "WACHAGA" wanaibeba kaskazini?
Jibu rahisi tu ni kuwa kwa upende wa Kaskazini ni maeneo wanayoishi "WACHAGA" peke yake ambayo yalikuwa na maendeleo ya hali ya juu hususani sehemu za vijijini. Kwa leo hii ukiambiwa kuwa Hospitali ya KCMC iko ndani ya Wilaya ya Moshi Vijijini tena Tarafa ya URU utakataa kwa nguvu zako zote.
Karibia kama siyo theluthi ya shule zote za sekondari za Tanzania zinapatikana Kilimanjaro maeneo wanayoishi Wachaga. Ni nadra sana kutembea zaidi ya Km 5 bila kukuta Shule ya sekondari kwa maeneo haya.
Hali ni tofauti kwa maeneo ya upareni.... Utakuta shule kwa wastani wa kila baada ya km 15 hadi 20 kwa maeneo ya kijijini na kwa mjini walau km 7 mpaka 10. Kama mtu anajua umbali wa Shule ya sekondari Vunta mpaka ya Kirangare atasema nasema ukweli.
Maeneo wanayoishi wachaga yana taasisi kubwa hata vijijini na sehemu kubwa imefanywa kwa juhudi za wananchi wenyewe. Kuna mahospitali makubwa yaliyoanzishwa zamani sana kama vile Kibosho Hospital, Kibong'oto (maarufu kwa kifua kikuu), Machame Hospital.... Adhani ina miaka kama 110 au zaidi.... Hospitali ya Kilema... Ilianzishwa miaka ya mwishoni mwa karne ya 19 (1890s)..,Hospitali ya Marangu.... Hospitali ya Huruma iliyopo Rombo.
Sitaongelea barabara za lami zinazoelekea Sanya Juu, Masama, Machame, Kibosho Umbwe, Mbokomu, Kibosho Mweka, Kibosho Kirima, marangu hadi Kilema (kwa sasa inazunguka mpaka kwa Lazari)... Kwenda Kirua Vunjo kupitia Kongo, barabara ya kupandisha Uchira, Old Moshi hadi ilipokuwa shule ya Kolila zamani, marangu mtoni hadi marangu gate, rombo kupitia Mwika.... Naona nikiendelea nitawaabisha tu watani.
Unaachaje kubebwa na mtu mwenye Chuo kikuu cha KCMC, MWENGE, SIMUKO, Chuo cha Wanyamapori Mweka (Tanzania vipo 2 tu na hiki ndio kilikuwa pekee kwa Afrika mpaka miaka ya 2000) Marangu TTC, Mandaka TTC, Singachini TTC, vyuo vya uuguzi KCMC, Machame, Kibosho nk.
Naona niache kutaja shule kama Umbwe, Lyamungo, Kibosho Girls, Machame Girls, Weruweru, St. JAMES' seminary (1925), Uru seminary.... Maua Seminary au basi Ashira Girls... Wengine wakati wanakazana kupokea mahari WACHAGA walikuwa wakijenga shule kwa ajili ya watoto wao wa kike... Unaachaje kusema wanabeba Kaskazini?
Turudi kwenye maendeleo binafsi... Wewe binafsi kama kweli hauna chuki na wachaga utakubali kuwa ndio Jamii pekee kwa TANZANIA NZIMA na sio Kaskazini tu ambapo hauwezi kukuta nyumba ambayo haijaezekwa kwa bati yata kama ni kule kibosho "Ntudu" au Mahoma - Old Moshi.
Pia ndio sehemu ambayo watu hawajisaidii machakani au kwenye choo cha shule kama wapare.... Utakuwa shahidi yangu kama unamjua mchaga kuwa hata kama anaishi sehemu ya mbali na Kilimanjaro utamjua kwa haraka bila kuambiwa kwa kuona nyumba yake tu kwani itakuwa tofauti na ya wenyeji... (standing out). Na "mchaga" asipokuwepo sehemu basi jua wazi hiyo sehemu hakuna maendeleo. Wengi ni "ULTIMATE OPPORTUNISTS".
Kwa mumalizia jibu hili fupi hebu niambie kama huko Kaskazini ni Wapare (Wasu), Wairaq au Wamasai wapi huwa wana"flock" kurudi nybani kwa likizo (VACATION) kama wazungu wengine wafanyavyo kipindi cha majira ya joto?
Sio wapare huwa wanajifanya kuwa na wao ni kina Mangi wanafuata Wachaga kurudi Moshi na wanaishia Hedaru kisha wanarejea maana hawajajenga kwao?
Tuanze na majibu haya kwanza.