Kangi angalau alijaribu kuwadhibiti ST, huyu Simbachawene hamna kitu labda mengine!

Waache kununua V8 vx ili waache fujo kutanua barabarani kuleta usumbufu usio na tija yeyote, umefika mda Magari ya Serikali yote yawe aina moja tu Rava4 old model zinawatosha waache kutumia mabilioni ya walipa kodi kujinunulia magari ya gharama I hali Hosptal hazina huduma za kutosha kuna upungufu wa madawati madarasa barabara mbovu mitaani zinahitaji ukarabati mkubwa
 
Kama wewe ni mtumiaji na msafiri utakubaliana na mimi kwamba wavunjaji wakubwa wa Sheria za barabarani ni Serikali, magari ya ST hayafwati Sheria zozote, hayasimami kwenye taa...
Lugola atapelekwa mahakamani lini? Magu tuambie. Longo longo hatutaki
 
Barabarani hasa huko jijini Dsm magari ya Serikali yana vurugu kubwa mno barabarani kuliko hata bodaboda na daladala
Inawezekana sababu wanakuwa wanaharaka ya utekelezaji majukumu ,au huwezi jua kama wametoroka Dodoma!!
 
Juz kuna gari ya naibu waziri sijui alikua wa nini yule alinipita maeneo ya mafinga yani alikua speed kias kwamba hata sikufanikiwa kumaliza kuisoma ile namba plate akawa kashapotea kwenye upeo wa macho yangu

Namuonya yule dereva na boss wake, kama wataendelea kutembea kwa mwendo ule basi wajue kabisa hawataiona awamu ya sita.
 
Mwaka juzi kama sikosei ST ziliua sana kisa mwendo kasi, mojawapo ni ajali ya TIC iliyoondoka na rafiki yangu.
 
Unateseka unapoona ST Inakupita kwenye kibao cha 50 Pole na wewe kaombe udereva serikalini...kifupi hao ni watendaji wa serikali hawezi kuwa ameitwa na KM kwa jambo muhimu aendelee kuobserve 50km Pole jikaze.
 
Kifupi magari yenye namba za kibalozi ya kinga ya kuwa treated tofauti unaumia kuanzia mataa ya serena hadi palm Beach wanakula katikati.
 
ila hayo magari ma VX na ma V8 ukiyapanda alafu ukaenda mwendo wa kama ist au vitz, inakua ni matumizi mabaya ya resource za taifa. Hayo raha yake ni mwendo ndio yananoga. Hata ungekua wewe unemuamlisha dereva akanyage!
 
Kangi alifanikiwa sana kwa hilo na kwa kukata mauno
 
Tena ST na polisi, utawakuta sana pale Sokoine AVENUE DAR wakipanda kuelekea ST Joseph then Stesheni halafu central police
 
Hilo swali gani? Kwani Simbachawene hafiki humu jukwaani kuu JF? Kama hafiki JF lazima atakuwa waziri asijejua majukumu yake
Kwa namna yoyote ile uzi wowote upandishwao hapa unakuwa na kusudi la kuelimisha, kuburudisha, kuhabarisha, kutahadharisha. Ingawa nyuzi nyingine upandishaa hapa kwa nia ya kupotosha, kufitinisha, na mambo mengine kama hayo!
 
Inawezekana sababu wanakuwa wanaharaka ya utekelezaji majukumu ,au huwezi jua kama wametoroka Dodoma!!
Hakuna lolote, mara nyingi unakuta wanawahi supu. Kuna siku natoka Mbeya kuna STL moja ilipita kwenye 50 speed kali na overtaking za kipuuzi, kufika Kitonga nikawakuta wamegonga lori kwa nyuma, gari inafuka moshi na kuna mwanaume (nadhani driver) wanampepea na wengine wameshika tama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…