Kanibwagia mtoto mlangoni, sasa ndoa yangu imeshikiliwa na kamba nyepesi mno

Kanibwagia mtoto mlangoni, sasa ndoa yangu imeshikiliwa na kamba nyepesi mno

cliff jerfeson

New Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
2
Reaction score
1
Wadau habari zenu,

Msichana mmoja nilie zaa nae mwaka 2011 katika mazingira ambayo nayajutia hadi Leo, amekuja nyumbani kwangu siku ya jumapili mchana kweupe na kumbwaga mtoto mlangoni na kutoa maneno makali na kuondoka huku mke wangu akiwa haamini kinachotokea mbele yake.


Historia ya tatizo:-

Mwaka 2011 tulienda safari ya kikazi Mtwara, tulikua wawili mimi na huyu mzazi mwenzangu wote tukiwa wafanyakazi wa kampuni moja.Tulikaa kule kwa wiki tatu. Tulipofika kule akaja na mpango wa kunirubuni kwamba tutumie chumba kimoja cha hotel chenye vitanda viwili double ili tuchukue ile hela ya kile chumba kingine tugawane

Na akashauri tukachukue guest ya kawaida tu ya shiling 15,000 badala ya ile ya 40,000 inayotambuliwa na kampuni
Kwa mantiki hiyo tutaondoka na hela nzuri mwisho wa hiyo project. Akasema huwa wanafanya hivyo sana kila waendapo mikoani wanapokua wasichana kwa wasichana, sasa safari hii tumechanganywa jinsia tofauti ila haina shida ilimradi tu kila mtu analala kitanda chake.Kwa injili hiyo nikawa nimekubali mpango huo maana kwa kweli mshahara wetu ni mdogo mno hivyo hizo ndio dili za kupiga hela.

Sijui ni shetani gani alietuingia na sijui tulianzaje anzaje ila nachokumbuka ni kuwa siku ya pili tu ya arrangement hiyo nilistuka usiku wa manane na kumuona mwenzangu night dress yote ipo kiunoni akiwa ametawanya miguu na makalio yote yapo nje yakiwa yamesitiriwa na kufuli ya kamba tu iliyopita katikati ya ikweta. Nilikua najiamini sana kutokana na dini niliyokua nimeishika vilivyo lakini cha ajabu sikuweza kuhimiri jaribu hilo, nilijikuta namrukia huyo binti kitandani kwake na kumvua kufuli kama nafukuzwa vile ambapo alinipokea kwa mikono miwili na kwa bahati mbaya tukafahamiana
Tuliendelea kufahamiana wiki tatu zote za project

Ndipo tukiwa Dar akaja kuniambia ni mjamzito mwezi mmoja baadae, nikamwambia mimi ni mume wa mtu atafute utaratibu mwingine, akaniambia hamna tabu atasafiri kwenda Arusha kwa boyfriend wake akamwonjeshe halafu amsakizie akasema kwa Wachaga wanavyopenda watoto asingeruka, ila akaniambia kwa option hiyo mimi sina changu hapo na nisije kudai mtoto mbele ya safari nikakubali pia. Nilikubali kupoteza damu yangu kwa sababu nilijiuliza ntamwambia nini mke wangu siku akijua nina mtoto pembeni niliempata baada ya ndoa?

Hofu hii imetokana na ukweli kwamba mke wangu alinikuta kanisani nikiwa na mazingira magumu sana, akanipenda na akaamua kunisitiri, sikua hata na mahari ya kupeleka kwao, yeye wife ndo alinipa mahari ya kupeleka kwa wazee wake.Hata gharama za ndoa na harusi ni yeye ndo alinipa, alianza kazi siku nyingi na ana biashara kadhaa hivyo yupo vizuri.Baada ya ndoa alinitafutia kazi kwa magumashi na kufosi sana, sikua na vigezo stahiki, nilikua na cheti cha form six ambacho nilifanya vibaya, nilipata principle pass moja maana mzee wangu ndo alikua amefariki wiki hiyo ya mitihani ya mwisho, mke wangu alinilipia kozi jioni ya diploma nilishamaliza, ndo wife akakipeleka cheti kwa baba yake mkubwa ambae ndie hr wangu na kuchomekwa kwa file langu

Yule binti niliezaa nae nilikua nimeshasahau suala lake siku nyingi, nilijua alishambambika yule Mchaga wake siku nyingi maana binti mwenyewe aliacha kazi mda sana, hatukuwahi kuwa na mawasiliano hadi alipoibuka January mwaka huyu akinitisha nimtumie hela la sivyo atamleta mtoto, nikimuuliza kuhusu Mchaga ananiuliza mtoto ni Wa Mchaga au wako?
Nikawa simuelewi kwa kweli

Sijui amepajuaje kwangu, nimestukia tu huyu hapa na mtoto siku ya jumapili iliyopita Muda ya saa nane mchana, kagonga Getimsichana wa kazi kaenda kufungua, almanusura nizimie kwa mshtuko, mzazi mwenzangu akiwa na mtoto mkononi akafika na kumbwaga mlangoni ni mtoto wa miaka mitatu kwenda minne, akaanza kunipaka mbele ya mke wangu na kudai ameniletea nilee mimi na wife na akaondoka zake.

Mke wangu alianza kulia na kuniambia maneno makali sana, akaniambia nibebe mzigo wangu niondoke nao. Nikampigia simu yule binti nikambeleza tuonane usiku huo huo maana tayari ilishafika usiku hapo, nilizunguka na mtoto hadi alipokubali tuonane saa nne usiku baada ya kumwambia nina laki 3 mfukoni aje achukue, akaja nikampa hiyo laki 3 akamchukua mtoto akaondoka huku akinimbia "" usinichezee mimi"" .Tangu siku hiyo wife ananitazama tu hanisalimii wala nn, wala hatuongei kabisa. Nimemlilia na kumshika miguuni lakini hakunijali.

Sasa sijajua kama ndoa bado ipo kwa hali hii. Yeyote mwenye suluhisho nahitaji msaada wa haraka, akina na mama humu ndani nifanye nn katika hali kama hii ili huyu mwenzenu aweze kunisamehe.Yaani amefura hata kumuongelesha naogopa, hata ile nafasi ya kujitetea ameshindwa kunipa. Au niondoke tu pale nyumbani na mabegi yangu nikaanze moja?

Your help is highly needed

Wenu mtiifu

Mimi na mke wangu tuna watoto wawili
 
Aisee kuolewa kubaya sana hakuna namna nyingine mpigie magoti mmeo umwombe msamaha mwambie ukweli maana kweli itakuweka huru. Endapo atakutimua usife moyo anza maisha mapya
 
Aisee kuolewa kubaya sana hakuna namna nyingine mpigie magoti mmeo umwombe msamaha mwambie ukweli maana kweli itakuweka huru. Endapo atakutimua usife moyo anza maisha mapya
Mke wake ndo kamkosea mkuu
 
Muombe samahan... Ikiwezekana hata andika barua au email..

Kama akiwa kimya jaribu mda mnapolala kuongea lililopo moyon mwako bila kujali anakisikiliza au kasinzia. Kama ukiona hali haibadiliki basi hebu washirikishe wazee walio karibu nanyi hasa hasa waambie wazazi/walezi wako wakupe ushauri haf mtafte na huyo mjomba wa mkeo aliekuajiri mweleze akusaidie. Kama suluhisho likikosa bada hapo ndio waweza kufukiri kuhama nyumbani had mkeo atapokuhitaji.
*ila usiache kuhudumia wanao hata ukitka kwa mkeo, na pia huyo mtt wa nje anza kujenga mazngira ya ukaribu ili huyo mama asikutishe tishe. Kubali responsibility yako hata mkeo atapokusamehe
 
The truth shall always set you free. Iwapo ungekuwa mkweli kwa mkeo toka huyo so called binti aanze kukutishia hio january; usingekumbwa na fedheha hii na wala usingemuumiza mkeo kwa kiasi hicho!!
 
Suluhisho hapo nikumuomba radhi sana nakupiga magoti ila kwa nature ya wwanawake walivyo jua na wewe lazima utakuja ulee mimba ambayo siyo yako...

Anzisha maongezi wewe...
 
You must be a MAN. Yule mtoto ni wako, ulikosea sana kumwachia maana pale unapokaa ndiyo kwao. Kwa nini unaiacha damu yako ikakae utumwani kwakuwa unamwogopa wife. Kosa kubwa. Mweleze mkeo kama anataka uendelee na huyo mwanamke basi mtoto akae huko maana utatakiwa kupeleka matumizi. Endapo anataka uachane kabisa na huyo mwanamke basi mtoto aje na wewe kata mawasiliano kule. Na amlee.
 
Dah, pole sana kaka. Ndo maisha. Kuondoka na kuacha familia sio solution. Hta ww ukivaa viatu vyake, utaumia sana. Muache apoe kwanza. Cha muhimu kubali kabisa kwamba umefanya makosa. Tafuta wazee wa busara sana, waongee hilo suala. Wewe kwa kuwa ni mkosaji namba 1, ni ngumu sana kulisolve. Hapo huwezi kutumia ubabe, lazima uwe mpole tu mzee.

Fanya yoooote, lakini mzazi mwenzako akikuletea mtoto, usije ukakubali kukaa na huyo mtoto. Mpeleke hata kwa wazazi wako au hta dada yako akae nae. Kinachoniogopesha hapo ni kwamba, kama mkeo sio muelewa, anaweza akatumia uwepo wa huyo mtoto wa nje ya ndoa wakati yeye akiwa ameshaolewa, kama fimbo ya kukuadhibu. Cha muhimu ni kwamba ongeza mapenzi sana kwa mkeo, huku ukionesha kabisa kabisa kwamba hiyo hali hata wewe inakuumiza.
 
amehama chumba au bado....kama bado wakati wa kulala jaribu kuongea nae na kumwomba msamaha mweleze shetani alikupitia :A S-fire1:
 
Hiki kisa kinaweza kuwa cha kweli naomba umlilie wife wako mpaka akusamehe mwelezee mazingira ilivyokuwa nina uhakika atakusamehe ukiona hataki kukusamehe ondoka hapo nyumbani(kama nyumba amejenga yeye)akipigwa na upweke atakukumbuka.
 
Na inavyoonekana ndoa yako ipo mikononi mwa my wife wako. Yani yeye ndio ana final say kwa vile yeye ndio main bread winner.
Kiongozi wewe endelea kupiga magoti, muombe tu mkeo akusamehe na kukusitiri..
 
Na inavyoonekana ndoa yako ipo mikononi mwa my wife wako. Yani yeye ndio ana final say kwa vile yeye ndio main bread winner.
Kiongozi wewe endelea kupiga magoti, muombe tu mkeo akusamehe na kukusitiri..

Mwanaume ukiolewa na mwanamke ni mbaya sana
 
Kwanza fahamu mambo flani uliyokosea.
1.Kumsingizia shetani, wakati mfanya tendo ni wewe na wala sio shetani.
2.Kumzingizia MUNGU kwamba wewe ni mtu wa dini na imani kali , kumbe ni mzugaji.
3.Kushindwa kuzuia hisia zako kwa mzinzi mwenzio (NB>We are human being having clear concise).
4. Kutomwambia mwenzio 9mke wako harari ) juu ya faulo uliyocheza.
5.Kukubali kuweka makubaliano / aagano na mwanamke (huku ukijua kuwa hawa ni viumbe dhaifu, na pia wasaidiz wetu).
6.Kuwa na wazo la kukimbia mji wakati wewe ndio kichwa cha familia.
7.Kutelekeza damu yako halali kisa kumuogopa mwanadamu mwenzako (mkeo halali) na kusahau kuwa "the blood is
thicker than water".

Chakufanya:
1.Kaa chini ongea na mkeo umueleze kweli ya dhati (black & white) juu ya huyo mtoto.
2.Kaa chini uongee na huyu mzinzi mwenzio ambaye alikuja kukuletea mtoto nyumbani.
3.Usikimbie nyumba kisa damu yako kwani utakuwa umeongeza duku duku zaidi na kujivua uanaume wako.
4.Akishika msimamo wa kumkataa mtoto , tafuta hata utaratibu wa kumpeleka dogo kwa wazee wako na kisha kuwa unatoa matumizi juu kwaju.
The way foward
 
Mpe muda amalizie hasira ila jua basi hakuna uaminifu tena na kama hakuna uaminifu hata love hakuna. Pole hapo ushaitia doa ndoa yako wanawake huwa wanasamehe ila huwa hawasahau mpk anaingia kaburini.
 
Mweleze ukwel mkeo kwa sababu na yy n binadamu pia atakuelewa na wala.usilaximishe akuelewe siku hyo hyo taratibu tu
 
Back
Top Bottom