Kanibwagia mtoto mlangoni, sasa ndoa yangu imeshikiliwa na kamba nyepesi mno

Kanibwagia mtoto mlangoni, sasa ndoa yangu imeshikiliwa na kamba nyepesi mno

Tatizo lenu mnajifanya jeuri huyo dada toka hy januar ungekua unamtumia pesa ya matumiz cjui km yangekukuta hayo btw damu yako ni damu yako ty mwambie mkeo ukweli na endelea kutuma matumiz
 
hiv mme wa mtu unaejitambua na unasema umeshika dini unaanzaje kulala na mwanamke mwingine usiemfahamu chumba kimoja,
sasa hiyo pesa uliyo serve kipindi hicho ulifanyia nn cha maana zaidi ya kukuletea haya matatizo, khaa!

kwanza naona huna maamuz binafsi unapelekwa sana,
Yule mwanamke alikushaur mlale chumba kimoja ukakubili bila hata kufikiria we ni mme wa mtu, pia inaonesha hata mkeo unamuogopa,

Mpe muda hasira zake ziishe, Halafu tafuta mtu wa heshima unae mwamini mueleze yote akaongee na mkeo, na we uonyeshe kujutia kosa.

Huyo mwanao wa katikati ya ndoa chukua peleka kijijini kwa mama yako au bording school na utoe huduma zote

Hili jina nimelipenda
 
Muombee tu msamaha mkeo.
kwa hali aliyokukuta nayo na kwa namna alivyokusaidia lazima tu aumie kwa huo usaliti wako. ukiangalia na mtoto yupo na amemuona na kwa miaka yote umemficha kwa miaka karibia minne.
 
mkuu punguza jaziba, hata bungeni kuna swali la msingi na swali la nyogengeza, kwa hiyo hili ni swali la nyongeza Mgirik
 
Last edited by a moderator:
Kijana una mambo mengi yalokukabili...

1. Umeolewa

2. Una mtoto wa kufikia asiyejulikana kwa 'mumeo'

Hata sijui usaidiwe vipi

Kwa kweli huyu kijana ana mtihani mgumu sana. Maana "mumewe" akimsamehe jamaa atakabidhiwa madaraka mapya ya uhausiboi.

Nauchukia sana umaskini.... source Edoboy Lowasaman.
 
Una shilingi ngapi. ikusaidie.namba yangu......0754 60 45 67..piga kama unashida.....tatizo lako dogo sana na ukichelewa atakutoa ndani maana inaonyesha hapa ameshauriwa na yeye arudishe kisasi.na wewe utakasirika na kuondoka.

Taarifa yoyote ya kuuwawa au kupotea kwa mama mwenye binti wa miaka mitatu ikisikika... You are in trouble. You are warned....
 
Aisee kuolewa kubaya sana hakuna namna nyingine mpigie magoti mmeo umwombe msamaha mwambie ukweli maana kweli itakuweka huru. Endapo atakutimua usife moyo anza maisha mapya
Hahaha
 
The truth shall always set you free. Iwapo ungekuwa mkweli kwa mkeo toka huyo so called binti aanze kukutishia hio january; usingekumbwa na fedheha hii na wala usingemuumiza mkeo kwa kiasi hicho!!
 
Wadau habari zenu,

Msichana mmoja nilie zaa nae mwaka 2011 katika mazingira ambayo nayajutia hadi Leo, amekuja nyumbani kwangu siku ya jumapili mchana kweupe na kumbwaga mtoto mlangoni na kutoa maneno makali na kuondoka huku mke wangu akiwa haamini kinachotokea mbele yake.


Historia ya tatizo:-

Mwaka 2011 tulienda safari ya kikazi Mtwara, tulikua wawili mimi na huyu mzazi mwenzangu wote tukiwa wafanyakazi wa kampuni moja.Tulikaa kule kwa wiki tatu. Tulipofika kule akaja na mpango wa kunirubuni kwamba tutumie chumba kimoja cha hotel chenye vitanda viwili double ili tuchukue ile hela ya kile chumba kingine tugawane

Na akashauri tukachukue guest ya kawaida tu ya shiling 15,000 badala ya ile ya 40,000 inayotambuliwa na kampuni
Kwa mantiki hiyo tutaondoka na hela nzuri mwisho wa hiyo project. Akasema huwa wanafanya hivyo sana kila waendapo mikoani wanapokua wasichana kwa wasichana, sasa safari hii tumechanganywa jinsia tofauti ila haina shida ilimradi tu kila mtu analala kitanda chake.Kwa injili hiyo nikawa nimekubali mpango huo maana kwa kweli mshahara wetu ni mdogo mno hivyo hizo ndio dili za kupiga hela.

Sijui ni shetani gani alietuingia na sijui tulianzaje anzaje ila nachokumbuka ni kuwa siku ya pili tu ya arrangement hiyo nilistuka usiku wa manane na kumuona mwenzangu night dress yote ipo kiunoni akiwa ametawanya miguu na makalio yote yapo nje yakiwa yamesitiriwa na kufuli ya kamba tu iliyopita katikati ya ikweta. Nilikua najiamini sana kutokana na dini niliyokua nimeishika vilivyo lakini cha ajabu sikuweza kuhimiri jaribu hilo, nilijikuta namrukia huyo binti kitandani kwake na kumvua kufuli kama nafukuzwa vile ambapo alinipokea kwa mikono miwili na kwa bahati mbaya tukafahamiana
Tuliendelea kufahamiana wiki tatu zote za project

Ndipo tukiwa Dar akaja kuniambia ni mjamzito mwezi mmoja baadae, nikamwambia mimi ni mume wa mtu atafute utaratibu mwingine, akaniambia hamna tabu atasafiri kwenda Arusha kwa boyfriend wake akamwonjeshe halafu amsakizie akasema kwa Wachaga wanavyopenda watoto asingeruka, ila akaniambia kwa option hiyo mimi sina changu hapo na nisije kudai mtoto mbele ya safari nikakubali pia. Nilikubali kupoteza damu yangu kwa sababu nilijiuliza ntamwambia nini mke wangu siku akijua nina mtoto pembeni niliempata baada ya ndoa?

Hofu hii imetokana na ukweli kwamba mke wangu alinikuta kanisani nikiwa na mazingira magumu sana, akanipenda na akaamua kunisitiri, sikua hata na mahari ya kupeleka kwao, yeye wife ndo alinipa mahari ya kupeleka kwa wazee wake.Hata gharama za ndoa na harusi ni yeye ndo alinipa, alianza kazi siku nyingi na ana biashara kadhaa hivyo yupo vizuri.Baada ya ndoa alinitafutia kazi kwa magumashi na kufosi sana, sikua na vigezo stahiki, nilikua na cheti cha form six ambacho nilifanya vibaya, nilipata principle pass moja maana mzee wangu ndo alikua amefariki wiki hiyo ya mitihani ya mwisho, mke wangu alinilipia kozi jioni ya diploma nilishamaliza, ndo wife akakipeleka cheti kwa baba yake mkubwa ambae ndie hr wangu na kuchomekwa kwa file langu

Yule binti niliezaa nae nilikua nimeshasahau suala lake siku nyingi, nilijua alishambambika yule Mchaga wake siku nyingi maana binti mwenyewe aliacha kazi mda sana, hatukuwahi kuwa na mawasiliano hadi alipoibuka January mwaka huyu akinitisha nimtumie hela la sivyo atamleta mtoto, nikimuuliza kuhusu Mchaga ananiuliza mtoto ni Wa Mchaga au wako?
Nikawa simuelewi kwa kweli

Sijui amepajuaje kwangu, nimestukia tu huyu hapa na mtoto siku ya jumapili iliyopita Muda ya saa nane mchana, kagonga Getimsichana wa kazi kaenda kufungua, almanusura nizimie kwa mshtuko, mzazi mwenzangu akiwa na mtoto mkononi akafika na kumbwaga mlangoni ni mtoto wa miaka mitatu kwenda minne, akaanza kunipaka mbele ya mke wangu na kudai ameniletea nilee mimi na wife na akaondoka zake.

Mke wangu alianza kulia na kuniambia maneno makali sana, akaniambia nibebe mzigo wangu niondoke nao. Nikampigia simu yule binti nikambeleza tuonane usiku huo huo maana tayari ilishafika usiku hapo, nilizunguka na mtoto hadi alipokubali tuonane saa nne usiku baada ya kumwambia nina laki 3 mfukoni aje achukue, akaja nikampa hiyo laki 3 akamchukua mtoto akaondoka huku akinimbia "" usinichezee mimi"" .Tangu siku hiyo wife ananitazama tu hanisalimii wala nn, wala hatuongei kabisa. Nimemlilia na kumshika miguuni lakini hakunijali.

Sasa sijajua kama ndoa bado ipo kwa hali hii. Yeyote mwenye suluhisho nahitaji msaada wa haraka, akina na mama humu ndani nifanye nn katika hali kama hii ili huyu mwenzenu aweze kunisamehe.Yaani amefura hata kumuongelesha naogopa, hata ile nafasi ya kujitetea ameshindwa kunipa. Au niondoke tu pale nyumbani na mabegi yangu nikaanze moja?

Your help is highly needed

Wenu mtiifu

Mimi na mke wangu tuna watoto wawili
Jambo muhimu ni kumuomba radhi mkeo,na husisha wazee wake,wazee wa kanisa na msingi omba radhi,na utubu huku unalia na kutambaa chini na kugaragara,atakusamehe tu
 
Back
Top Bottom