#COVID19 Kanisa Katoliki Arusha na uzembe kwenye Corona

#COVID19 Kanisa Katoliki Arusha na uzembe kwenye Corona

fisi 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
3,280
Reaction score
4,645
Nimesali leo Kanisa Katoliki Ngaranaro (kwa Babu) ibada ya misa ya kwanza. Nimesikitika sana hakuna tahadhari yoyote kuhusu corona hakuna hata tangazo zaidi ya vindoo vya maji ambavyo hakuna kuhimizwa watu kunawa.

Ibada ni ndefu bila sababu kuanzia saa 12.30 asubuhi mpaka saa 2.20 asubuhi almost 3 hours. Watu wamebanana na hata kwenda kutoa sadaka au kupokea wanabanana huku wanaimbiana midomoni. Sanitising kits hazina sanitizer yaani nimebonyeza mpaka mikono unauma nothing oozes out. Katika watu karibia 400 wenye barakoa nimehesabu hawafiki 45.

Mbali ya hapo nyimbo zipo nyingi mno yaani kila kipengele cha liturjia wanaimba unaona tu midomo inatoa Moshi na baridi hii. Hii ni hatari yaani Jimbo kuu hakuna mwongozo wa kuendesha ibada kwa tahadhari. Jimbo la Dar es Salaam muda wa ibada umepunguzwa to one hour na nyimbo 3 au nne tu za muhimu kuingia, sadaka kupokea na mwisho Basi zinatosha sio kumpigia Mungu makelele wakati wa hatari hivi.

Arusha Askofu na kamati za jimbo za afya wamelala sana andaeni mwongozo wa ibada za misa jumapili ziwe fupi si zaidi ya saa moja. na mzifuatilie. NI BORA KUWA NA IBADA ZA MISA 6 KULIKO KULUNDIKA WATU NDANI BILA TAHADHARI ZOZOTE.

Mkuu wa mkoa Arusha peleka vijana kwenye haya makanisa kama hawataki kuona tatizo. What is this we are already injured wengine hata marehemu wetu hatujawazika.

NGARENARO CATHOLIC.jpg
 
Kuna na wengine wanakimbiza mwenge huku. Wanasema wanashukuru kwa kuwa eti hawakufungiwa ndani wakati hawajui idadi kamili ya wahanga wa hatua hizo.

Inabidi kuelewa definition kamili ya neno "wendawazimu" kuweza kuzielezea hali kama hizi.
 
Usijaribu kukuza mambo, sema ulichokiona, wote kweli tunajua tuna wimbi la korona, na tunazingatia miongozo kutoka kwa wataalam wetu, sasa ya nini ukuze mambo (exaggerate)? Sasa ibada kutoka saa 12:30 mpaka saa 2:10 ndio masaa matatu? Kwa nini tusiwe wakweli?
 
Usijaribu kukuza mambo, sema ulichokiona, wote kweli tunajua tuna wimbi la korona, na tunazingatia miongozo kutoka kwa wataalam wetu, sasa ya nini ukuze mambo (exaggerate)? Sasa ibada kutoka saa 12:30 mpaka saa 2:10 ndio masaa matatu? Kwa nini tusiwe wakweli?

Nenda shule ujue maana ya almost. Wengine be objective mnajibu tuu bila kufikiri? Nisiende kanisani?& jinga nyie.
 
Hiyo mikoa ndio ina maambukizi zaidi lakini watu hawachoki kuishi kwa mazoea, kuvaa barakoa wameshindwa kabisa, japo hapo kwenye foleni sijui ya kutoka kwenye sadaka naona distance ya kutosha kati ya mtu mmoja na mwingine, tatizo wakienda kukaa wanabanana tu.
 
Halafu una gadhabu sana, kunywa maji.

UVIKO-19 haijaanza leo. Tumeishi nayo siku zote na hakuna madhara makubwa kihivyo.Wewe endelea kuchukua tahadhari, hakuna anayekukataza.

Ukisubiri waraka ndiyo uchukue tahadhari, then unasikitisha.
 
Nenda shule ujue maana ya almost. Wengine be objective mnajibu tuu bila kufikiri? Nisiende kanisani?& jinga nyie.
01 Hour 50 Minutes ni almost two hours, siyo three. Umesoma shule gani?
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Kuna Mungu gani RC zaburi 91 10
 
Wewe badala ya kuishangaa serikali kutokutoa muongozo wa maziko kwa watu wanaokufa kwa Corona unalishangaa kanisa ambalo limejitahidi kuweka vindoo vya maji?Is this fair?
 
Usitupange, usitutishe. Hata tukiumwa tukifa ni juu yetu angalia maisha yako. Tusichunguzane sili silali kwako. Au kuna gharama utaingiliwa nikifa. Chaooo
Ndugu ni haki yako kusema usemayo na ni huru kabisa!

Ila mpaka dhahama hii kutufikia sisi ni chain ndefu sana ugonjwa ulipita!! Kuna watu walisema hawajali hata kama watakufa bila kuelewa yeye akipata hata mwingine ambaye alitakiwa kumlinda naye anaambukizwa!

Huwezi jua wewe ni kijana na huna hofu maana kinga yako nzuri, ukamuambukiza mtu hata ambaye humjui akaenda kijijini akakutana na mzazi wako akamuambukiza!

Asipomuambukiza mzazi wako akamuambukiza mtu wako wa karibu mfano daktari ambaye siku zijazo ataokoa maisha yako au maisha ya mtoto wako au mume au mke wako, au mtu yeyote wa karibu na muhimu katika maisha yako!

Kwenye maisha tunategemeana as far upo duniani huwezi kusimama mwenyewe!

Unapomlinda jirani
 
Nenda shule ujue maana ya almost. Wengine be objective mnajibu tuu bila kufikiri? Nisiende kanisani?& jinga nyie.
Nitakusaidia, najuwa una tatizo. Huo muda uliotaja, toka ibada inaanza mpaka inaisha ni saa 1:50 (12:30 - 2:20), sasa hiyo ni almost 3 hours? Halafu unatukana kwa kujiona uko sahihi. Sasa nikupe shule; neno almost linatumika kwa kumaanisha: ilibakia kidogo tu kutimia kiasi fulani. Tukirudi kwenye muda uliosema hapo juu, basi angalau ungesema: almost 2 hours! Upo?
 
Umeenda kanisani kwa imani ipi mbona unakuwa Muoga unajuwa kuwa Yesu anaponya?.
Kuna neno gani gumu ambalo hawezi kulitenda

Hii ni ibada ya kwanza tangu Corona imeanza mpaka uanze kuwa na Wasiwasi.
 
Back
Top Bottom