Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Taarifa ya kanisa katoliki Jimbo la Bukoba ni kuwa wamekiri kumtambua Padre Elipidius Rwegoshora

Pia hatua waliyochukua ni kumsimamisha kutoa huduma mpaka swala (tuhuma) lake litakapo isha ndipo nao watachukua hatua zaidi kulingana na taratibu zao

Chanzo: Gazeti la kanisa (kiongozi) na Mwandishi Delpina Rubyema

View attachment 3022695
 
Mungu yupo ndani mwako,,,,kwenye hizi dini ndo walozi wengi wamejificha humo,,,,,na wanacheza sana na saikolojia za waumini wao, ukienda kichwakichwa unachezea ndoige za kutosha
Kweny dini kuna waganga wanaoseme wanatumia vitabu na kuna wavaa suti , wote wachawi wana nguvu za giza nyuma yake kupumbaza watu.
 
Kweny dini kuna waganga wanaoseme wanatumia vitabu na kuna wavaa suti , wote wachawi wana nguvu za giza nyuma yake kupumbaza watu.
Tatizo watu hawasomi wakaelewa na wanaosoma wakaelewa hua wanajitoa mapema baada ya kugundua hapa ninapigwa, Biblia ipo wazi kabisa wala haina konakona Ila washenzi wanatengeneza konakona zao kuwapiga watu kuna wapiga ramli waliovaa suti na Mkononi wameshika Bible na wanapaza sauti kuliita Jina la Yesu Mazabauni kwa sauti Kuu bila uoga na watu wanawaamini akasema "Watu wangu wanahangamia kwa kukosa maarifa" watu wanaokusanyika km makutamo Biblia hawaisomi wengi wao wale unaowaona wamekusanyika pale kwa fulani na kwingine Biblia hawaisomi Ila wanapenda kusomewa tuneno Neno na kuombewa wao wenyewe kuomba hawaombi Ila wanataka kuombewa sasa wale wapiga ramli chonganishi waliovaa suti wanajua jinsi ya kudeal nao lakini wengi hawaisomi Biblia na kuielewa wachache wanaoisoma na kuielewa uanza kwa kuhoji wengine huwazuia wasihoji Ila wanapoendelea kuhoji huambiwa watoke wakaanzishe cha kwao km wanaona kilichopo hakifai maana yake wengi wapo sababu wanahofia kufukuzwa lakini si kwamba wapo sababu wanapenda kuwepo
 
Kanisa Moja Takatifu La Mitume Duniani ( Katoliki) limemsimamisha Paroko Elpidius Rwegoshora anayetuhumiwa kuuwa Albino Ili haki itendeke kwa mamlaka za Dola kumchunguza kikamilifu

Source: Mwananchi

Nawatakieni Sabato Njema 😄
 
1. Kifo cha binti kimetuhuzunisha sana, kama dada wa Lazaro tunamlilia Mungu kama angelikuwepo haya yasingetokea. Katika mapungufu ya binadamu ndipo uwezo wa Mungu unadhihirika.
2. Padre anapaswa kuombewa na kuhurumiwa sana. Hatuna hakika sana padre alitoa ushauri upi?
3. Padre ni zao la jamii husika. Sio malaika ni binadamu kama sisi, hakushuka toka mbinguni. Jamii ndio inapaswa kusutwa kwa matukio kama haya!!!!! Watuhumiwa wako 9 lakini anashambuliwa mmoja hiyo nayo haiwezi kuwa sawa.
5. Tusali sana kuìombea roho ya marehemu na tumwombee sana padre, wakati huu wa kutengwa na kukataliwa!
6. Laiti jamii ingefahamu walau kidogo maisha ya mapadre. Hiyo ya kusimamishwa kutoa huduma peke yake ni adhabu kubwa kutolewa na askofu!
 
Hapa mada ya uraia haitakosa! Ila huyu padre itakuwa Askofu alishamchoka la sihivyo Kanisa lingekanusha tu na habari ingekuwa kwisha.(Kanisa katoliki lipo juu ya sheria)
Wanaoijua hii wanaelewa RomaLocutaCausaFistinaEst
Juu ya sheria zipi mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…