Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha Padre Rwegoshora kufuatia tuhuma za kuhusika mauaji ya Asimwe Novath

Kwani si Yuko mahabusu? Hata asingesimamishwa,angeendeleaje kutoa huduma?

Mara ya mwisho kutoa huduma ni lini?
Nazani wengi walimkataa kuwa sio padre, hakuna cheo cha msaidizi, msaidizi sio lazima awe Padre

Maelezo yalikuwa mengi sana kuonesha kukinzana na taarifa za polisi

Sasa kama taasisi anayoifanyia kazi imekubali uwepo wake na kuna machapicho yake na huduma anazotoa ni wazi taarifa ya jeshi ilikuwa sahihi

Pia tusi sahau ata ktk vyombo vya imani kuna vyombo pia vya nchi, dola inamkono mrefu
 
Hapa mada ya uraia haitakosa! Ila huyu padre itakuwa Askofu alishamchoka la sihivyo Kanisa lingekanusha tu na habari ingekuwa kwisha.(Kanisa katoliki lipo juu ya sheria)
Wanaoijua hii wanaelewa RomaLocutaCausaFistinaEst
Acha upotoshaji huo.
Mamlaka za uchunguzi zimemtuhumu huyo Padre kwa vigezo vyao, iwe kweli au laah Kanisa haliwezi kuingilia kukanusha au kukubali. Kanisa lingekanusha lingekuwa linazuia Polisi kufanya kazi yao ya uchunguzi, pia lingeingia kwenye migogoro isiyo na ulazima na jeshi la Polisi.
Baada ya kutuhumiwa, Kanisa limetoa ushirikiano kwa kumsimamisha Padre huyo kutoa huduma. Mengine yote, iwe kweli au isiwe kweli itajulikana Mahakamani.
 
Sahihi kabisa, wametoa ushirikiano na kuondoa taharuki
 
Hawa ndo wale usipoenda kwenye jumuiya na kutoa michango wanatoa povu kama lote,,,,halafu mwisho wa siku wanachokutishia ni misa siku ukifa,,,,kudadeki kama kufa kwenyewe ndo unakuja kufanyiwa misa na paroko kama huyu bora tu tusielewane kila mtu aendelee na formula zake,,,,,,,kanisani tunakuja na sadaka tunatoa ile tu ya kwenye misa mengine kila mtu na 50 zake
Ujinga huu ndo ulinifanya kaa mbali na kanisa hili, kuna ubabaishaji wa ajabu sana msione wapo ndani ya majoho. Hakuna raha za dunia wazizofanya labda wale wa zamani ila sio hawa G - z
 
Kumbe ni kweli? Nilitaka kushangaa, Polisi wamethubutu vipi kukurupuka kumtaja Parko msaidizi bila ushahidi..!

Wale mliokuwa mnasema paroko hawezi kuthuhumiwa nyoosheni mikono juu
[/QUOTE.Paroko si malaika ni binadamu wa kawaida tu anayeweza kupotoka shetani akimuingia. Kwa ujumla mapadri na watu wa aina hiyo wenye mifano ya utaua si watakatifu ila wanapewa utukufu wa bure
 
Tangu nikiwa mtoto mdogo nilikuwa nashangaa kuona padri anakunywa pombe, tena pombe za kienyeji kama mtukuru na komoni, pombe ya uwele na mahindi. Mshangao zaidi anavuta tumbaku kwa kutumia kiko/mtemba. Ni baada ya kutoka kuendesha ibada ya misa tena padri mwenyewe ni mzungu. Nilishangaa sana mtu wa mungu anatumia vilevi
 
Hizo hatua zaidi za kikanisa zitakazochukuliwa baada ya tuhuma zake kuisha ni zipi? Na kwann wanahakika kwamba tuhuma zake zitaisha? Wasilete umaalumu kwenye Sheria za nchi na Uhai wa mtoto mdogo wa miaka miwili. Tena aliyekuwa akipambana na Maisha ya ulemavu wa ngozi.
Kama wao wana umaalumu sana wange simamia Maadili na Mienendo ya watu wao.
 
Wamuulize huyo padre alitaka akafanyie nini hivyo viungo vya malaika.
 
Hapa mada ya uraia haitakosa! Ila huyu padre itakuwa Askofu alishamchoka la sihivyo Kanisa lingekanusha tu na habari ingekuwa kwisha.(Kanisa katoliki lipo juu ya sheria)
Wanaoijua hii wanaelewa RomaLocutaCausaFistinaEst
Umesharudi Jumuiya au bado?
 
Hizo hatua zaidi za kikanisa zitakazochukuliwa baada ya tuhuma zake kuisha ni zipi? Na kwann wanahakika kwamba tuhuma zake zitaisha? Wasilete umaalumu kwenye Sheria za nchi na Uhai wa mtoto mdogo wa miaka miwili. Tena aliyekuwa akipambana na Maisha ya ulemavu wa ngozi.
Kama wao wana umaalumu sana wange simamia Maadili na Mienendo ya watu wao.
Umesharudi Jumuiya asubuhi hii?
 
Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji Padri, Elipidius Rwegoshora kufuatia tuhuma zinazomkabili za kuhusika katika mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Asimwe Novart.

Askofu wa Jimbo Katoliki Bukoba, Jovitus Mwijage ametangaza uamuzi huo kupitia gazeti la Kiongozi linalotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), toleo lake la Juni 21 -27, 2024

Gazeti hilo limemnukuu Askofu Mwijage akikiri kuwa mtuhumiwa ni padri wa jimbo lake na amemsimamisha kutoa huduma zote za kichungaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Tunahuzunishwa na taarifa ya mauaji ya Asimwe, kwani sisi kama Kanisa Katoliki ni walinzi wa kwanza wa uhai wa wanadamu. Tunaiombea familia yake na kuiombea roho yake ipate pumzio la amani mbinguni.

“Hata hivyo, tumesikia taarifa ya watuhumiwa na mmojawapo akiwa ni Padri Rwegoshora. Ni kweli padri huyo ni wa jimbo Katoliki Bukoba na tumechua uamuazi wa kumsimamisha kutoa huduma zote za kichugaji mpaka hapo suala lake litakaposhughulikiwa na vyombo vya sheria.

“Baada ya vyombo vya sheria kumaliza kazi yake, ndipo taratibu nyingine za kanisa zitafuata,” amesema Askofu Mwijage.

Asimwe menye umri wa miaka miwili na nusu alinyakuliwa mikononi mwa mama yake na watu wasiojulikana Mei 30, 2024 katika Kijiji cha Bulamula, Muleba mkoani Kagera.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma
Ndio huyo kwenye picha kumbe
 
Hizo hatua zaidi za kikanisa zitakazochukuliwa baada ya tuhuma zake kuisha ni zipi? Na kwann wanahakika kwamba tuhuma zake zitaisha? Wasilete umaalumu kwenye Sheria za nchi na Uhai wa mtoto mdogo wa miaka miwili. Tena aliyekuwa akipambana na Maisha ya ulemavu wa ngozi.
Kama wao wana umaalumu sana wange simamia Maadili na Mienendo ya watu wao.
Sasa wewe hapa hoja yako ni nini? Huu ni utaratibu wa kanisa katoliki kumsimamisha mtumishi wake kutoa huduma (hata kama ni mtumishi ambaye siyo padre) katika mazingira kama haya. Hata serikali humsimamisha kazi mtumishi wake akiwa na tuhuma za kijinai na hata za madai. Padre ni mtumishi wa kanisa kama alivyo mtumishi wa serikali.
Nalipongeza jeshi la polisi kwa hatua hii. However our Police Force should be converted into a Police Service for obvious reasons.
 
Back
Top Bottom