Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Chukua tahadhari wewe, watu kufa Marekani na wapi sijui si sababu au justification ya wewe kufa pia, acha ujinga
 
Kwanini wasifunge kabisa makanisa ili tuone kweli wako serious kuliko hii ya kuallamika tu?
Hivi yule wa Kagera aliyefunga kanisa una mkumbuka? Baada ya kufunga kanisa aliishi kwa amani mbele ya Hawa wachumia tumbo wa CCM?
 
Imetokea hivyo Kwa mama yangu na Mzee wangu, wote sasa wakonyumbani na wanaendelea na maisha, lkn kilichosababisha ni Yale maneno ya faraja,
Umemweleza rais wako kwamba ni kweli corona ipo?

Umemweleza pia kwamba ilibidi uwapeleke wazazi wako hospitali na hukuishia kuwafukizia tu nyumbani?

Umemweleza rais wako kwamba ni kweli hofu/uoga ni kitu kibaya sana, sio katika mambo ya magonjwa tu bali hata katika mambo mengine yanayotokea huko mitaani na hata kwenye siasa?
Hili ni janga, na kila mtu anajua Hilo, lakini katikati ya janga kama hili ikikosekana faraja linakuwa janga kubwa zaidi.
Ulimweleza rais wako juu ya hii faraja unayoizungumzia hapa, ili na yeye awe na moyo wa faraja kwa raia anaowaongoza?
 
Povu lote hili ni kwa sababu tu padri kasema corona ipo na imeua watumishi wake kibao? Ama unachuki nyingine na padri wetu
 
Utatuzi unaanza kwa kukubali tatizo lipo na kutoa data.

Huko kote ulikotaja wamekubali tatizo lipo na wametoa data.

Tanzania serikali haitaki kutoa data, hili ni tatizo, ndiyo maana makanisa yanaanza kuona bora yatoe data zao.

Ushaelewa somo?
Nafikiri hayo makanisa kama wako serious wangefunga kabisa ibada mpaka gonjwa lipite
 
Ee mwenyezi Mungu mtenda miujiza nakuomba unichukulie huyu mwanasiasa anayewadanganya wananchi kuwa hakuna janga huku wanaendelea kufa tu.UU
Mchukue hata akawe mfagia choo huko.
Amen.
Mungu mwenye haki akuchukue PINC upesi tena kwa corona ya ajabu ajabu; na kumlinda Rais wetu Mhe.Dkt.John J.P. Magufuli kinyume na dua zenu.
 
Hii nchi, unaweza ukasikia yale ya Open University..., Taasisi na Wadau wenzake kuita Kikao na kumwambia aombe msamaha wa kutoa hizi Takwimu...
Hakupaswa kutoa hizi takwimu, siyo wajibu wake, amesababisha hofu na taharuki isiyo na sababu! Ashitakiwe kwa mujibu wa Sheria ya takwimu!! Yeye angetahadharisha tu! Hawa maaskofu na mapadri wakiheshimiwa wasidhani kuwa wako juu ya Sheria!!
 
Hivi yule wa kagera aliyefunga kanisa una mkumbuka? Baada ya kufunga kanisa aliishi kwa amani mbele ya Hawa wachumia tumbo wa ccm?
Sasa alifanywa nini? Hakuna mtu alimbughudhi, tena alikuja kufungua hayo makanisa mwenyewe bila kulazimishwa na mtu na hata kwenye mikusanyiko ya maelfu ya watu kwenye mikutano ya Lisu wakiwa hawajavaa barakoa akawa anaenda.
 
Sasa alifanywa nini? Hakuna mtu alimbughudhi, tena alikuja kufungua hayo makanisa mwenyewe bila kulazimishwa na mtu na hata kwenye mikusanyiko ya maelfu ya watu kwenye mikutano ya Lisu wakiwa hawajavaa barakoa akawa anaenda.
Hujui ulisemalo,Kama watu wanadhalilishwa hadharani huko sirini so ndo kwenye shida kabisa?
 
Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu awajibike na atumie uwezo wake kufikiri.
Nadhani hawa hawataki kutumia dawa za asili kwa dhana ya kishirikina wanaimani na dawa za wazungu tu.
 
Reactions: Ame
Marekani wamekufa watu nusu milioni. Vipi kule nako ukweli ukoje?
Bila kuchukua tahadhari na kufuata ushauri wa maafisa wa afya,kama sisi idadi ya vifo mpaka sasa ingekuwa maradufu.

Na tatizo la Corona lilisabishwa na dharau za kichwamaji Trump mwanzoni alichukulia maambukizi ya Corona kwa kejeli na dharau,makosa yaliyoigharimu pia nchi ya Italia.
 
Eeenh Heee.

Hii nayo itakuwa aina fulani ya taaluma.

Watu wataanza kujipatia kipato kwa mgongo wa corona..., ushaliwazia hili kwa utulivu mkuu 'Sky'!
 
Hakupaswa kutoa hizi takwimu, siyo wajibu wake, amesababisha hofu na taharuki isiyo na sababu! Ashitakiwe kwa mujibu wa Sheria ya takwimu!! Yeye angetahadharisha tu! Hawa maaskofu na mapadri wakiheshimiwa wasidhani kuwa wako juu ya Sheria!!
Shule ulienda kufanya ko nini ?! Kama Padri amezungumzia kanisa lake . Siyo takwimu za nchi kama Tz . Hivi ukiwa mfuasi wa u dictator na u communist lazima uwe hamnazo ?!

Hakuna sheria inayomzuia kuzungumzia watu walio chini yake. By the way u communist & u dictator haujawahi kuitoa nchi yeyoe mrisi [emoji107]. mbingunikwetu
 
Mbona sisi tuliendelea na maisha ila hatujafa kwa malaki?
 
Kama kweli wanajali wasimamishe mikutaniko ya jumuiya. Kitubio kitafutiwe aina nyingine ya kuungama

Misa zipunguzwe au zisimame kwa muda kuepusha kusambaa kwa ugonjwa
Ningemwelewa huyo m-tec kama angetoa tamko la kufungwa kwa ibada zote kanisa katoliki tanzania; na kuhakikisha sheria, kanuni na taratibu wanafuata kivitendo na kuacha kupayukapayuka kwenye vyombo vya habari na mitandao ya jamii kushindana muumini wake hadharani!
 
Pale Vatcan wamekufa wangapi?
Hadi leo Vatican hakuna mtu aliyepoteza maisha tangu Corona ibishe hodi pale.
Takwimu zinaonyesha kuwa walikuwa na maambukizi ya watu 27 wakapona 15 na 12 bado hawajapona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…