Kanisa Katoliki lasema ndoa zitaendelea kufungishwa ila watahusika Wanandoa na Wasimamizi wanne tu

Hicho kituko ni kipi? Unachoambiwa kuhusu corona ni kwamba unawe mikono na usiwe kwenye msongamano wa watu wengi. Wakiwapo wasimamizi wanne tu kwenye kufunga ndoa, waoanaji wawili na wahudumu wa hapo kanisani, ina maana watakuwemo watu wachache tu kanisani, kiasi kwamba kutakuwepo na nafasi kati ya mtu na mtu; ambacho ndicho kitu kinacholengwa. Wewe usiyeona mantiki katika kuaswa unawe mikono na utumie sanitizer, tuambie tufanye nini, kitu ambacho kitakuwa si upuuzi?
 
Kanisa kuu duniani limeongea. Asante Sana Mh. Dr. Katibu Mkuu (PhD) kwa ufafanuzi huu. Maana michamgo ilizidi unashangaa pesa hii inakwemda wapi?
Mkuu umepanot hapo kwny michango tu
 
Kama mmezuia sherehe, bado kuna haja ya mamia kuwa kanisani kila jumapili?

Si vema kuendelea kusubiri serikali itoe tamko, nanyi toeni maamuzi kwa waamini wenu.
Mabenchi bado yamejazana, wanakwaya wanaendelea kupumuliana kwa kigezo cha kufundishana mazoezi achilia uimbaji kanisani. Ni vema litoke tamko kuwa watoto hapana, wazee hapana, wajawazito hapana, kwaya zisimame kwa sasa, awepo mmoja anayeongoza nyimbo then waumini kuitikia au kuimba mwenyewe.
Mic inaambukiza hivyo kutumia wengi haifai hivyo tofaut na mapadri ambao ni familia wengine ni mmoja tu aruhusiwe kusoma masomo, na matangazo.
Mita moja izingatiwe kweli ikiwezekana benchi moja livukwe kila baada ya kukaa benchi husika, wahudumu hasa dar kila kanisa wanunuliwe suits za kuzuia maambukizi na kupima joto la mwili.
Ministrant wapumzishwe kwa sasa au atumike mmoja( chetezo kinaweza punguzwa kwa sasa)

Sadaka, masunduku yawe wazi lkn watu wavae barakoa wote wanaoingia kanisani kasoro makundi yaliyopumzishwa.
 
Wamekusikia na mengi yamezingatiwa. Kwa mwendo huu wanandoa wataogopa hata kulala kitanda kimoja.
 
Kanisa kuu duniani limeongea. Asante Sana Mh. Dr. Katibu Mkuu (PhD) kwa ufafanuzi huu. Maana michamgo ilizidi unashangaa pesa hii inakwemda wapi?
Kwani sherehe za ndoa huwa zinasimamiwa na kanisa? Kanisa hufunga tu ndoa mambo ya sherehe hayahusu kanisa.Hilo.tamko la kuhusu sherehe kadandia kusiko kwake
 
Hivi yale mambo ya kwenda na washenga ukweni kutoa mahari nayo si ni aina ya mikusanyiko isio ya lazima...?
Hayo ni mambo binafsi hayahusiani na kanisa unataka kanisa litoe tamko?
 

Kuna uwezekano hii Corona itabadilisha kabisa taratibu za sherehe za ndoa mazimaaaaaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…