PostGE2025 Kanisa Katoliki limetoa maagizo ya tangazo la misa ya kuwaombea watu waliouawa 29 Oktoba 2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Misa nchi zima, Kanisa limeagiza Kesho watangaziwe kwenye jumuiya ndogo ndogo, jumapili tutangaze kanisani, na wiki yote inayofuata Itakuwa ya kutangaziana.

======

Mwadhama Kardinali,

Wahashamu Maaskofu Wakuu,

Wahashamu Maaskofu.

Bwana Awape Amani!

YAH: WITO WA KUADHIMISHA MISA TAKATIFU KWA NIA YA KUOMBEA MAREHEMU NA WAATHIRIKA WA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU SIKU YA TAREHE 29 ОКТОВА 2025​

Kwa moyo wa kichungaji na kwa kutambua wajibu wetu wa kuliongoza Taifa la Mungu katika ukweli, haki upendo na mwanga wa Injili. Kwa barua hii nawaalika kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuliombea Taifa letu la Tanzania na sisi wenyewe. Katika kutimiza mwaka. moja tangu uchaguzi wa mwaka jana, tunakumbuka baadhi ya watu wetu kuumizwa, kupotea na hata kuuawa. Hali hiyo ya maumivu na msiba bado ipo kati ya watu wetu.

Katika mazingira haya, tunaitwa kusimama pamoja kama jumuiya ya waamini, tukimkabidhi Mwenyezi Mungu mwenye huruma Taifa letu, viongozi na watu wake. Tukiomba umoja, upendo, ukweli, mshikamano ambavyo ni matunda ya haki na amani. Kwa sauti ya upole, unyenyekevu, unyofu na majuto tuombe faraja kwa wanaolia, tumaini kwa waliokata tamaa, imani kwa wenye mahangaiko, haki na ukweli kwa waliopotea, busara kwa wasioelewa, uponyaji kwa wenye majeraha na upendo kwa wenye chuki. Pia huruma ya Mungu kwa wale waliotangulia mbele ya yake.

Tunaomba Misa Takatifu ziadhimishwe kwa nia hizo; walioumizwa, kupotea, kuuawa na kuliombea Taifa letu. Tunashauri Misa hiyo ifanyike katika Parokia, vituo vya sala na Taasisi za Kanisa kadiri iwezekanavyo siku ya Alhamisi 29 Oktoba 2026. Misa inaweza kufanyika asubuhi muda wa kawaida, au muda wowote unaofaa. Masomo ya siku au ya kuchagua yanaweza kutumika kwenye Misa hiyo.

Tukizidi kuliombea Taifa letu, naendelea kumshukuru Mungu kwa kila moja wenu kwa upendo, uelewa, ushirikiano na majitoleo yenu yasiyokoma.

Soma Pia: Makanisa ya CCT kuwakumbuka waliouawa, kumwaga damu Oktoba 29, 2025

Katika utumishi, upendo na ukweli,

+ Wolfgang Pisa, OFMCap

Askofu wa Lindi na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC)
1003455132.jpg
 
View attachment 3697014
Kanisa la Mungu.
 
ok.
sawa na ibada ifanyike kwa amani.

msisahau pia kuwaombea na wale wote walio athirika baada ya dhuluma za kingono kama vile kupigwa mimba na kulawitiwa na mapadre na viongozi mbalimbali wa kanisa dunia kote na Mungu wa huruma awajaalie faraja ya amani mioyoni mwao na itapendeza zaidi 🐒
Tutajumlisha maombi hadi waliolawitiwa na vyombo vya Dola.
 
Back
Top Bottom