Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Mkuu wa Utawala na Fedha wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church - Ufufuo na Uzima, Askofu Baraka Thomas Tege amedai kuwa, tangu kanisa hilo lilipofungwa Juni 2, 2025 na hatimaye majengo ya yao kulindwa na Jeshi la Polisi nchi nzima, hakujawa na makabidhiano yoyote ya mali zikiwamo fedha za sadaka, vyombo vya muziki na samani.
Soma pia: Polisi wazingira kanisa la Gwajima
Katika video inayosambaa mitandaoni leo Juni 19, 2025, Askofu Tege amedai kuwa polisi wameweka makufuli yao kwenye milango ya makanisa hayo na kuwaondoa waliokuwa walinzi wa kanisa hilo.