Kanisa la Gwajima ladai Polisi wameshikilia mali zao bila makabidhiano

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Your browser is not able to display this video.

Mkuu wa Utawala na Fedha wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania Church - Ufufuo na Uzima, Askofu Baraka Thomas Tege amedai kuwa, tangu kanisa hilo lilipofungwa Juni 2, 2025 na hatimaye majengo ya yao kulindwa na Jeshi la Polisi nchi nzima, hakujawa na makabidhiano yoyote ya mali zikiwamo fedha za sadaka, vyombo vya muziki na samani.

Soma pia: Polisi wazingira kanisa la Gwajima

Katika video inayosambaa mitandaoni leo Juni 19, 2025, Askofu Tege amedai kuwa polisi wameweka makufuli yao kwenye milango ya makanisa hayo na kuwaondoa waliokuwa walinzi wa kanisa hilo.
 
Muliro na majambazi wenzake wameshagawana nyara tayari
 
Kwa kuwa muelekeo wa hii kesi wanaenda kushinda waweke ushahidi uionashaka kwamba walikuwa wamehifadhi mali huko ndani na hawajazikuta .
Waje wafungue kesi ya madai
 
Gwajima huwaibia mazwazwa wacha naye aibiwe aonje joto ya jiwe kama jusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…