LOTH HEMA
JF-Expert Member
- Dec 6, 2015
- 18,611
- 27,615
Haya mambo ya ubaguzi yanazidi kushamiri tangu wamisionari waache kutoa misaada. Huu mtindo haupo kkkt tu hata makanisa mengine upo, kama huna hela utaibika huku umevaa suti na tai. Jumapili moja niliingia kwenye kanisa moja kusali, mchungaji akaanza kupanga safu za kukaa kwenye viti akianza na wenye laki tano, wenye laki nne, tatu, mbili, laki moja, elfu hamsini na kundi la mwisho ikawa ni wenye chini ya elfu hamsini. Kwa kweli nilijisikia vibaya watu kuwekwa kwenye madaraja ya utoaji waziwazi. Huu mtindo wa kuchangia michango kwa mpangilio huo hadharani ni kutweza heshima za watu kifedha. Mchango ulikuwa ni ununuzi wa gari la shule kubwa aina coaster. Ina maana kanisani wataenda wenye fedha tu. Kujikuta unaangukia kundi la wenye hela kidogo huku ukiwa unaonekana unazo hii ni aibu na fedheha. Utakosa ushawishi kama huna fedha hekima yako itadharauliwa na haitathaminiwa