Kanisa la KKKT kashfa ya ubaguzi ndani yake

Haya mambo ya ubaguzi yanazidi kushamiri tangu wamisionari waache kutoa misaada. Huu mtindo haupo kkkt tu hata makanisa mengine upo, kama huna hela utaibika huku umevaa suti na tai. Jumapili moja niliingia kwenye kanisa moja kusali, mchungaji akaanza kupanga safu za kukaa kwenye viti akianza na wenye laki tano, wenye laki nne, tatu, mbili, laki moja, elfu hamsini na kundi la mwisho ikawa ni wenye chini ya elfu hamsini. Kwa kweli nilijisikia vibaya watu kuwekwa kwenye madaraja ya utoaji waziwazi. Huu mtindo wa kuchangia michango kwa mpangilio huo hadharani ni kutweza heshima za watu kifedha. Mchango ulikuwa ni ununuzi wa gari la shule kubwa aina coaster. Ina maana kanisani wataenda wenye fedha tu. Kujikuta unaangukia kundi la wenye hela kidogo huku ukiwa unaonekana unazo hii ni aibu na fedheha. Utakosa ushawishi kama huna fedha hekima yako itadharauliwa na haitathaminiwa
 
Kanisa la CHADEMA hilo. Hivyo ubaguzi kwao ni kawaida. KKKT bila hela usiende. Lakini Katoliki nako bado mambo ni yaleyale.... akifa tajiri atazikwa na Askofu huku akisaidiwa na mapadre kadhaa.. ila akifa kapuku atazikwa na katekista. Yaani full ubaguzi. Ukiwa na hela ndani ya RC utakaa meza moja na askofu mkipiga mvinyo. Dini pekee angalau wanajitahidi kwenda sawa na dini inavyotaka ni uislamu. Hawa jamaa wako vizuri. Kweye ibada wote mnakaa chini huku mmevua viatu. Pia vaz lao la kanzu linasaidia sana kuficha matabaka. Madhehebu mengi ya kikristo kuna ubaguzi mno. Hayo ya kilokole ndo balaa zaidi.
 
Mtajuana wenyewee wafia Dini, na hizo Dini zenu.
Poleeeni sanaa
 
Ukiwa na pesa huko kanisani utawekwa siti ya mbele [emoji1]

Ova
 
Af wanachukulia kawaida
 
Acha tupewe heshima zetu tuwe kama ushuhuda kwa wengine kuwa Mungu anatenda.
 
Kama huna hela hata ndugu zako hawakuthamini dawa ni kujikubali tu
 
 
Tupo katika ulimwengu wa kibepari no money no acceptance no recognitions hii sio KKT ,RC,Muslim, sio Pentecostal churches, watch tower not SDA ni janga La kijamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…