Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Kanisa haliipongezi serikali, sijawahi kusikia wakikaa vikao vya kuipongeza serikali. Ila lina wajibu wa kuiombea serikali na kukemea dhambk na nadhani wanafanya hivyo...
Huwezi kuponga dhambi kama kanisa kama unashindwa kuikosoa serikali pale anapokosea huo ni Unafiki na uoga.
 
Unajua maana ya neno kanisa??
Kanisa maana yake ni walioitwa watoke.
Yesu alikuwa nakanisa lake dogo la watu 12
Mwanzo.
Ama ulitaka liwe ni jengo ili ulitambue kuwa ni kanisa

Kanisa lazima liwe jengo hiyo ndio maana yake ya msingi, hizo maana zingine za ziada ni nyongeza tuu
 
Huwezi kuponga dhambi kama kanisa kama unashindwa kuikosoa serikali pale anapokosea huo ni Unafiki na uoga.
Kanisa litaikosoa serikali pale inapoenda kinyume na neno.
Na sio kinyume na katiba
Katiba imeundwa na wanadamu inakosewa.
Ila neno ni la Mungu halikosewi
Kanisa haliwezi kushikilia msingi wa mwanadamu.
Kwakuwa sio yakini.
Ila msingi wa neno la Mungu
Sasa kanisa linakosoa mikataba,mara sijui linadai maji,mara shule, mara bandari.
Upuuzi kw kanisa
 
Kanisa lazima liwe jengo hiyo ndio maana yake ya msingi, hizo maana zingine za ziada ni nyongeza tuu
Unaona sasa ulivyokariri.
Kwamba kanisa ni jengo?
Kama kanisa ni jengo basi hata waislamu na wapagani wanayo tena mazuri tuu
Kanisa ni nini ?
 
Huwezi kuponga dhambi kama kanisa kama unashindwa kuikosoa serikali pale anapokosea huo ni Unafiki na uoga.
Kazi ya kanisa sio kuikosoa serikali, nenda kasome miongozo ya kanisa lako. Hatutaki kanisa liende kinyume na misingi yake.

Nakuunga mkono kwenye issue ya kuponda imani zingine, kujiona kwamba wao(wasabato)ni special kuliko, ndio waliochaguliwa etc ila swala la kuikosoa serikali haijawahi kuwa kazi ya serikali.
 
Viongozi wakuu wa sabato ni ccm .sasa wataikosoaje ccm? Ukiangali trend utaona jinsi wanavoisifia ccm na kuwaalika viongozi wa ccm kwa ajili ya matamko au kuwasafishia mambo yao..

Mbona hata hizo dini zingine kuna ccm lakini wakiona serikali imekosea wanakosoa?
 

Wasabato hawataki waumini wajihusishe na siasa na uongozi wa nchi,hii imani ya ajabu kweli,wao wakiamka na wakilala ni alama ya mnyama na ukatoliki,hovyo kabisa.

Bila kusahau Catholic ndio kanisa mama la ukristo duniani.
 
Miongozo hiyo imewekwa na wanadamu ambao ndio hao nasema wamegeuka Machawa.

Kusema kanisa lisiikosoe serikali au viongozi wa serikali wakikosea wakati manabii na viongozi wa kiimani karibia wote waliokosa serikali mpaka wengine kuwekwa jela ni kwenda kinyume na Biblia.

Muongozo mkuu wa Wasabato ni Biblia. Na biblia inataka Watu wakemee maovu ikiwemo ya Wanasiasa.

Yohana mbatizaji unamjua?
Isaya
Nehemiah
Musa
Yona
Yeremia
Wote hao waliikosoa serikali
 
Wasabato hawataki waumini wajihusishe na siasa na uongozi wa nchi,hii imani ya ajabu kweli,wao wakiamka na wakilala ni alama ya mnyama na ukatoliki,hovyo kabisa.

Bila kusahau Catholic ndio kanisa mama la ukristo duniani.

Hapa ndio kuna kukwama
 
Ndugu, vijikanisa vidogo vidogo visivyo na mifumo hasa hivi vya kipentekoste ni tatizo, bila kuisifia CCM wanaweza kujikuta wanakosa leseni za biashara zao, nukuu yaliyomkuta Mbarikiwa na kanisa lake kwa kusimamia haki. Kumbuka yaliyomkuta Kakobe baada ya kuihoji CCM, kumbuka yaliyotaka kumkuta mtumishi Mwingira aliposema Lissu hakamatiki ni sauti kutoka mbinguni tuifuate..

Kongole kwa kanisa katoliki kukupita maskofu wenu TEC, nyie ni vinara wa haki - wengine si kwamba hawataki wanataka ila wanaogopa tonge litadondoka.
 

Utapiganiaje Haki bila kujihusisha na siasa, hapo ndio uje na Facts?
Sasa like na sifa zitanisaidia nini Mimi?

Alafu kama wewe ni Msabato basi umenianbusha sana. Nilitegemea uje kwa hoja ili hata wasiowasabato wakisoma washawishike na hoja zako.
Sasa kama yesu hakuingia kwenye siasa Unafikiri kilichomfanya asulubiwe ni nini? Embu tumia akili hata kidogo.
 

Kifungu gani kimeitaja katoliki kama kahaba mkuu.
 
Soma
Luka 13:31-32
mafarisayo walimuambia ondoka hapa Herode anataka kukuua

Sasa hapo Yesu alijihusishaje na siasa?

Hofu ya Herode ilikuwa ni Yesu kuitwa mfalme wakati huo huo Herode naye alikuwa ni mfalme

Hata kama ni wewe mtu ukiona anataka kuchukua cheo chako utafanyaje
 
Yaani ulichokiandika ni sawa na kusema Chadema hawakemei dhambi au kuhubiri injili kama wenzao wa NCCR na UDP ambao nimekuwa nawasikia wakifanya hivyo na kazi yao Chadema ni kuponda CCM

Wasabato waamini dhehebu lao ni la kweli.na kwenye kweli kuna Haki.
Swali linakuja, kwa nini hawakemei uovu ambao unafanywa na serikali?
Huo ndio msingi wa swali.

Ukasema kunachangamoto ya kusali jumamosi, sawà!
Sasa tuambie utapataje haki ya kusali jumamosi na utaomba haki hiyo kwa namna ipi ikiwa unaamini utawala wa dunia ni washetani? Kwamba unamuona Shetani haki ya kumuabudu Mungu wako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…