Ukristo ambao mwanzilishi wake ni Yesu Kristo ulianza miaka mingi sana kabla ya kanisa katoliki kwaiyo nakuhakikishia kuwa kanisa katoliki sio mama wa ukristo,halafu Mtibeli,Biblia imeweka wazi kuwa Dunia hii au anayetawala ulimwengu kwasasa ni Ibili si shetani na ndiosababu ya matatizo yote unayoyaona ikiwemo vita,majanga ya asili,njaa n.k,,soma1Yohana5:19"Tunajua tunatokana na Mungu,lakini ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu".Kwaiyo hizi serikali zote unazoziana zipo chini ya shetani,ndiyosababu katika Yale majaribu ya shetani kwa Yesu,alimwambia endapo utanfanyia tendo la Ibada nitakupa falme zote na utukufu wazo(Mathayo4:8,9"Tena Ibilisi akampeleka Yesu kwenye mlima mrefu sana,akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wazo.9 Naye akamwambia nitakupa vitu hivi vyote ukianguka chini na kunifanyia tendo la Ibada),kwaiyo mkristo hauwezi kuwa mwanasiasa,lakini unapaswa kuheshimu mamlaka katika baadhi ya mambo kama kulipa Kodi maana ndio zinafanya tupate huduma mbalimbali kama raia,unankumbuka hata Yesu alikuwa analipa Kodi,lakini pale tu serikali inapokuagiza kufanya kitu kinyume na mapenzi ya Mungu haupaswi kukubali,soma Matendo5:29"Petro na wale mitume wengine wakajibu"Lazima tumtii Mungu kuwa mtawala badala ya wanadamu".Hata maandiko yanasema tunapaswa kuziheshimu mamlaka,soma Waroma/Warumi13:1-7. NOTE Hata hao wasabato wakiikosoa serikali hakuna watakachobadilisha kwasababu mtawala mkuu wa hii serikali ni Shetani na yeye hawatakii wanadamu mema,kwahiyo kuliko kuanza kuikosoa serikali ni bora wawe busy na kazi waliyoachiwa na Yesu Kristo ambalo ndio jukumu la wakristo wa kweli yani waeneze ujumbe wa Mungu kwa watu mbalimbali,soma Mathayo28:19,20"Basi,nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote,mkiwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu,20 na kuwafundisha kushika mambo yote niliyowaamuru.Na tazama! mimi nipo pamoja nanyi siku zote mpaka umalizio wa mfumo wa mambo". Hata Yesu alipokuwa anaishi Israeli,raia walikuwa wanakandamizwa vibaya mno na serikali yao ya wakoloni yani Waroma(Rumi empire), lakini jambo kuu ilikuwa ni kutangaza ufalme wa Mungu na sio kuzungumza siasa,matatizo ya wanadamu yatatatuliwa na ufalme wa Mungu tu na sio serikali za kibinadamu zilizo chini ya shetani, ndiosababu katika Sala ya mfano Yesu aliomba "Ufalme wako na uje duniani kama mbinguni" ngoja niishie hapa