Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Kanisa la Wasabato Mnapaswa Mkosoe maovu ya serikali zaidi kuliko kukosoa wenzenu wa Roman Catholic

Hapa tunaongelea siasa za CCM na CHADEMA na ACT, sio hizo za nyumbani sijui uchaguzi wa KKKT,

Viongozi wa dini wabaki kurekebisha watu waishi kadri apendavyo Mungu ila sio kuingilia siasa za nchi, mwanzoni tutaona raha, ila m nakuambia itafika stage watakuwa na nguvu sana halafu wataanza kuipora madaraka serikali hususani dini zenye wafuasi wengi,

Itakuwa ukienda kinyume na RC au Waisalam bas hutoboi kwenye siasa, itakuwa full kuwalamba nyao watu wa dini,

Sasa hapo ndio itakuwa mwisho wa demokrasia
Na ndio maana wewe hujaelewa, nilikuonya toka mwanzo labda hukumuelewa mtoa mada.

Ni wapi mtoa mada ameandika kuhusu ACT na CCM ?

Kwahiyo huko kanisani kwenu viongozi mnawapataje ?

Yule mtume wa 12 baada ya Yuda kufa alipatikanaje ?
 
Mungu hajawahi kubariki siasa
Na wala hatakaa awahi
Siasa ni michezo michafu yote.
Uongo,fitina na uzushi,mauaji na kila baya unalilojua.
Siasa iporadhi ikubali uchafu wajinsia moja na mengineyo .
Mungu kamwee hatakaa ajiingize
Na wala kanisa la kweli la Mungu halitakaa kamwee lijihusishe.
Kwanza kanisa la kweli linachefukwa na siasa
Viongozi kanisani kwenu mnawapataje?
 
Huyu wa ushoga ama.
Huyu Francis anaingiaje kwenye urithi wa kanisa la Mungu ilhali yeye ni mpagani??
Amerithi vipi?
Mnarithishana aaf mnasema ni Mungu alimchagua kwa moshi mweupe??
ELLEN G WHITE ndio mwanzilishi wa kanisa la wasabato
 
Ukristo ambao mwanzilishi wake ni Yesu Kristo ulianza miaka mingi sana kabla ya kanisa katoliki kwaiyo nakuhakikishia kuwa kanisa katoliki sio mama wa ukristo,halafu Mtibeli,Biblia imeweka wazi kuwa Dunia hii au anayetawala ulimwengu kwasasa ni Ibili si shetani na ndiosababu ya matatizo yote unayoyaona ikiwemo vita,majanga ya asili,njaa n.k,,soma1Yohana5:19"Tunajua tunatokana na Mungu,lakini ulimwengu mzima unakaa katika nguvu za yule mwovu".Kwaiyo hizi serikali zote unazoziana zipo chini ya shetani,ndiyosababu katika Yale majaribu ya shetani kwa Yesu,alimwambia endapo utanfanyia tendo la Ibada nitakupa falme zote na utukufu wazo(Mathayo4:8,9"Tena Ibilisi akampeleka Yesu kwenye mlima mrefu sana,akamwonyesha falme zote za ulimwengu na utukufu wazo.9 Naye akamwambia nitakupa vitu hivi vyote ukianguka chini na kunifanyia tendo la Ibada),kwaiyo mkristo hauwezi kuwa mwanasiasa,lakini unapaswa kuheshimu mamlaka katika baadhi ya mambo kama kulipa Kodi maana ndio zinafanya tupate huduma mbalimbali kama raia,unankumbuka hata Yesu alikuwa analipa Kodi,lakini pale tu serikali inapokuagiza kufanya kitu kinyume na mapenzi ya Mungu haupaswi kukubali,soma Matendo5:29"Petro na wale mitume wengine wakajibu"Lazima tumtii Mungu kuwa mtawala badala ya wanadamu".Hata maandiko yanasema tunapaswa kuziheshimu mamlaka,soma Waroma/Warumi13:1-7. NOTE Hata hao wasabato wakiikosoa serikali hakuna watakachobadilisha kwasababu mtawala mkuu wa hii serikali ni Shetani na yeye hawatakii wanadamu mema,kwahiyo kuliko kuanza kuikosoa serikali ni bora wawe busy na kazi waliyoachiwa na Yesu Kristo ambalo ndio jukumu la wakristo wa kweli yani waeneze ujumbe wa Mungu kwa watu mbalimbali,soma Mathayo28:19,20"Basi,nendeni mkafanye wanafunzi kutoka kwa watu wa mataifa yote,mkiwabatiza katika jina la Baba na la Mwana na la roho takatifu,20 na kuwafundisha kushika mambo yote niliyowaamuru.Na tazama! mimi nipo pamoja nanyi siku zote mpaka umalizio wa mfumo wa mambo". Hata Yesu alipokuwa anaishi Israeli,raia walikuwa wanakandamizwa vibaya mno na serikali yao ya wakoloni yani Waroma(Rumi empire), lakini jambo kuu ilikuwa ni kutangaza ufalme wa Mungu na sio kuzungumza siasa,matatizo ya wanadamu yatatatuliwa na ufalme wa Mungu tu na sio serikali za kibinadamu zilizo chini ya shetani, ndiosababu katika Sala ya mfano Yesu aliomba "Ufalme wako na uje duniani kama mbinguni" ngoja niishie hapa
 
Kanisa kazi yake ni kueneza ujumbe wa Mwenyezi Mungu na kujenga upendo na jamii bora.
Siasa ni kazi ya wananchi wenyewe na wawakilishi wao.
 
Wakati Mungu ni mtawala wa Israel unajua aliongoza vita ngapi?
 
Mtibeli umejidhalilisha kwa uelewa wako duni. Kanisa sio chama cha siasa kianze kulumbana na wanasiasa. Malengo ya kuanzishwa kanisa ni ya kiroho na sio siasa. Hiyo kazi kuna wahusika wake ambao tunawalipa kupitia ruzuku ili waifanye yaani vyama vya siasa. Na sio lazima wanachofanya KKKT kifanywe na SDA. Wasabato wako sahihi kabisa kuishi kwenye kanuni zao za kiimani walizojiwekea.

Ninakuunga mkono unavyosema SDA waache kuwashambulia wakatoliki kwa maneno ya hovyo. Huwa inaleta ukakasi sana kusikiliza shombo zinazorushwa na wasabato kwa wakatoliki. Wanachofanya sio sawa kabisa.
 
KANISA LA WASABATO MNAPASWA MKOSOE MAOVU YA SERIKALI ZAIDI KULIKO KUKOSOA WENZENU WA ROMAN CATHOLIC.

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mimi nimezaliwa kwenye Usabato, nimekua na kulelewa kwenye Usabato. Kimsingi Mimi ni Msabato ingawaje ni Mtibeli kiasili. Yaani tuseme ni Mtibeli aliyezaliwa katika Dhehebu la kisabato. Sasa sisi Watibeli ni Watu wa kusema ukweli hata kama unatugusa wenyewe. Hatunaga ushabiki.

Licha ya Wasabato wengi kubobea katika Mafundisho ya biblia na dini yao lakini wanaupungufu mkubwa wa kuisema Kweli hasa linapokuja suala la siasa, utawala na serikali.

Ni ngumu sana kusikia Kanisa la Sabato likikemea maovu ya Serikali. Kwa upande wangu sijawahi kusikia. Ila wakati huohuo ni rahisi kusikia kanisa la Wasabato wakiipongeza serikali na kuiombea. Hapa ndipo Watibeli tunapoona kuna tatizo fulani la Unafiki.

Wasabato wamefundishwa kutojihusisha na siasa. Kanisa pia moja ya sera zake ni kutojihusisha na siasa.

lakini Wasabato ni mabingwa duniani wa kukosoa dini zingine hasahasa Ukatoliki ambao ndio Mama wa Ukristo. Hata biblia inayotumika ni Wakatoliki walioiratibu na kuipanga. Ukisema bila ukatoliki hakuna biblia utakuwa upo sahihi kwa sababu Biblia ilikusanywa na wakatoliki. Nisitoke nje ya mada, na wala Wakatoliki wasidhani nawatetea hapa.

Hakuna kanisa lolote au dini yoyote itakayokuwa ya haki na sahihi zaidi ya ile inayotetea haki na kuikosoa serikali. Hakuna dini wala dhehebu hilo.

Manabii wote, mitume wote, Makuhani wote, Waamuzi wote walijihusisha na siasa hasa pale mambo yanapoenda Mrama au viongozi wa kisiasa wanapogeuka wadhalimu au kutenda maovu.

Yesu mwenyewe ambaye ndio msingi wa ukristo aliikosoa serikali na vyombo vya Dola.

Sasa iweje Wasabato wanajitoa katika wajibu huo.

Utatakaje Haki bila kujiingiza kwenye siasa ? How?

Yaani uwaambie waumini wako waache dhambi wakati msingi wa dhambi unabebwa na siasa.

Waumini watashikaje amri za Mungu bila kukemea viongozi wao wa kisiasa? how?

Amri kama ya kufanya kazi ambayo ni moja ya amri za Mungu, Muumini anafanya kazi kwenye serikali yenye mazingira ya mengi ya rushwa, wizi, ufisadi, dhulma alafu muda huohuo Kanisa halikemei serikali ikiwa na baadhi ya viongozi madhalimu, hivi kweli inakuja Akilini?

Unasema lengo la kanisa ni uinjilishaji,haya utafanyaje uinjilishaji kwa Watu na jamii inayodhulumiwa?
Badala ya kusaidiana na jamii kukabiliana na baadhi ya viongozi madhalimu ninyi mnawatia moyo wakijinga kuwa ati tumaini lipo wakifika Mbinguni kwani duniani kuna dhiki.

Wasabato tumekuwa kama Wamishenari walioungana na makoloni kututawala na kulainisha mioyo yetu kwa aya za kuokoteza.

Tumekuwa Machawa wa Watawala.

Haya mnahubiri neno la kweli, lakini kweli gani yenye mipaka? Kweli inayohusu Watu duni, dhalili, Waumini wasio na Mamlaka ndio kweli?

Kweli inayowaogopa Watawala na serikali? Hiyo ni kweli gani hiyo?

Tumekalia Sabato
Alama ya mnyama!
Sijui Papa!

Kama mnashindwa kuikosoa serikali mnayoiona mtawezana na Mambo ya Mnyama au huyo Papa kweli?

Tuacheni kuwa Machawa wa serikali!

Mbona Wakatoliki na Walutheri mabaraza yao kila mara hutoa matamko ya kukosa serikali pale wanapoona unakosea?

Dini ya kweli ni ile inayopigania Haki. Na huwezi pigania haki bila kuigusa siasa na serikali kwa sababu hao ndio wanahusika na mambo ya kutoa Haki.

Tusiwapotoshe waumini kuwa ati ufalme wa duniani hatuhusiani nao ilhali ibiblia iko wazi kuwa sisi ni Watu wa duniani na asilimia mia moja tunautawala huku duniani. Huko mbinguni sio kwetu na hata biblia yenyewe inakiri hilo. Ndio maana hata tukienda huko kama biblia isemavyo hatutakaa milele isipokuwa miaka elfu tuu.

Acha nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
hao pamoja na mashahidi wa yehova ni sawa tu na wanawake wanasubiri wanaume tuwapambanie wao waje wale kwenye sahani.
 
Kanisa litawasahihisha kila mtu anapoenda nje ya neno

Herode alikemewa kwkauchukua mke wa mtu,

Yohana aliuwawa sinkwa sababu ya kumkosoa herode ila yule mwanamke alimwambia binti yake achague kichwa cha yohana.

Sio kwenda kupiga kelel za maji,ama umeme ama bara bara.

Io sio kazi ya kanisa
Utumbo kbsa
 
Siku hizi wasabato wanakunywa soda na chai za majani ya chai ,kahawa[emoji1]

Ova
 
lakini Wasabato ni mabingwa duniani wa kukosoa dini zingine hasahasa Ukatoliki ambao ndio Mama wa Ukristo. Hata biblia inayotumika ni Wakatoliki walioiratibu na kuipanga. Ukisema bila ukatoliki hakuna biblia utakuwa upo sahihi kwa sababu Biblia ilikusanywa na wakatoliki. Nisitoke nje ya mada, na wala Wakatoliki wasidhani nawatetea hapa.
Wanasema Papa ni yule mnyama mwenye namba 666
 
Back
Top Bottom