Kanisa lamshinda Mc Pilipili

Kanisa lamshinda Mc Pilipili

Limemshindaje? Hajataka tu kufanikiwa.. hajataka kutafuta konekshen , akina mwamposa wamewwza sababu ya kua "connected" na "washika dau"
 
Hivi ndivyo anafunguka baba mchungaji wa Love Church Mc pilipili....

"Kanisa limenishinda, sasa hivi nahubiri mitandaoni pekee."

Anaendelea kufunguka Mc..

"Pale tulipokuwa tunakutana kila jumapili kwa ajili ya kufanya ibada hatukutani tena na badala yake nimebuni njia mpya ya kuhudumia watu kwa kutumia mitandao ya kijamii."

Kuhusu kuonekana akila bata club baba mchungaji amefunguka....

"Maneno yamekuwa mengi mimi kuonekana Club Element kwenye tukio la Haji Manara, kiukweli mimi nilienda pale kumsapot Manara na sikuangalia kama nipo club, biblia yenyewe haijatukataza kwenda club na kama Biblia ingekataza basi watu wasingekwenda hata Super Dome kufanya shughuli zao huko ".

Kuhusu kugombana na mke wake, baba mchungaji amefunguka....

" Ni kweli nimegombana na mke wangu na chanzo cha kugombana na mke wangu sio kuzaa na mwanaume mwingine kama watu wanavyosema, bali tumepishana kwa mambo yetu mengine na tunazungumza ili kuyamaliza".

Wana familia wa love church tujuane hapa tafadhari View attachment 2881414
😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom