Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Upo irrational sana!
 
Daah pole sana, nyie hamkufanya upasuaji?

Vipi hali yake kwa sasa? Chemo na mionzi zimemchosha zaidi au angalau amepata ahueni?

Pole sana ndugu daah
 
Unaonaje ungempa muongozo wa suluhisho badala ya kumbeza? Kumbuka huyu mwenzetu ana wakati mgumu kuliko unavyoweza kufikiria
Yaani mtu mwingine hajui wakati mwingine km huna cha kuandika ni hekima kunyamaza.
Mwenzetu anapitia magumu,ni wakati wa kumpatia msaada pale iwezekanapo,mtu anacheka.
 
Huyo mkeo anapona ndani ya MIEZI MITATU TU.

Ukiachana na wale MAKANJANJA wanaokuuzia MAKEMIKALI na MACHANJO anapona haswa na anakuwa SWALAMA WASWALAMANTA.

Unachotakiwa ni kuwa na AKILI TIMAMU tu, na kujiamini.
Mtoa mada angekutilia maanani akaachana na wategemea miujiza angevuna kitu cha maana sana kwako
 
Sawa mkuu
 
Pole sana mkuu MWENYEZI MUNGU asaidie, mama yangu alifariki na kansa ya titi mwaka 2013, alikuwa kashafanyiwa operesheni ndo maisha mkuu tutafanyaje!?
Apumzike kwa amani mama. Ina maana baada ya upasuaji aliendelea kuumwa eneo hilo?

Nauliza ili nipate uzoefu wako na mginjwa wa aina hii
 
Daah pole sana, nyie hamkufanya upasuaji?

Vipi hali yake kwa sasa? Chemo na mionzi zimemchosha zaidi au angalau amepata ahueni?

Pole sana ndugu daah
Mgonjwa aligoma kufanya upasuaji. Hali yake sio nzuri sana Wala mbaya sana, Kwa Sasa anasumbuliwa na kifua kubana maana Kuna dalili Kansa inasambaa kwenye mapafu hii kutokana na vipimo vya hospital.
Anapata maumivu ya mifupa na ganzi.

Miozi ilienda kutonesha kidonda kikazidi kuwa kikubwa ila baada ya kumaliza ndio kikaanza kufunga taratibu.
 
Pole Sana uchungu unao pata ni mkubwa mno

Ila Acha nikushaur kitu

Mpe furaha mkeo muda wote na mwambie Kila muda kuwa unampenda na umeridhika na Hali yake usimbeze ,usimkaripie wala kumdhihaki kivyovyote vile..

Usiache kumwambia kwamba haya yote ni majaribio ya Mungu na baada ya dhiki faraja

Usionyeshe Una huzuni Sana kwa Hali yake

Vivyo hivyo muombeni Mungu katika Kila Hali

Nimeumia mno pole Sana mkuu

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Endapo hatopona utamlipa fidia ya kumpotezea muda kwenye hayo matibabu yako? Tuacheni masikhara au kuleta biashara kwenye afya za watu, wewe ungekuwa na uwezo huo wa kutibu Cancer wala usingekuwa na muda wa kushinda humu jamvini kuwinda watu wa kuwatibu, watu wangekufuata wenyewe na usingekuwa na muda kabisa maana hata wateja wangekuzidia, pengine hata serikali ingekuwezesha ili uweze kusaidia wengi.


Acheni janjajanja yenu kwenye matatizo ya watu tafadhali.
 
Daah it's not fair

Sent from my SM-A047F using JamiiForums mobile app
 
Apumzike kwa amani mama. Ina maana baada ya upasuaji aliendelea kuumwa eneo hilo?

Nauliza ili nipate uzoefu wako na mginjwa wa aina hii
Alikuwa dar es saalam mkuu alipofanyiwa operesheni alikuwa anachomwa miozi pale muhimbili, mkuu sikuwa karibu nae mi nilikuwa mkoani huku, tulikuwa tunapewa tu taarifa ya hali yake, kuamkia jumapili alifariki akiwa amelala tu kitandani Nyumbani kimya milele, ndo hivyo tu
 
Pole sana ndugu ,pole mno.
Mwenyezi Mungu ampe nguvu ya kuvumilia maumivu, ampe subira na tumaini.
Kuna wakati mwanadamu anafika kikomo kwa namna ya ubinadamu na hapo ndipo Mungu hushika nafasi ,Mungu yupo na yupo kwa wote, wote wenye heri na wenye Shari.
Yupo kwa kila mwenye haja nae, hajifichi wala hayupo mbali sana kwa yoyote aliweka nia ya dhati kumhitaji.

Wakati huu mkiwa mnapitia changamoto hio na maumivu hayo makali na kukata tamaa ndio Mungu hushika nafasi yake.

Ili kukutana na Mungu kwanza kuweni na amani, msilitazame sana hilo tatizo bali muoneni Mungu katika hilo tatizo, mshuhudieni Mungu kwenye hilo tatizo.

Jitahidini sana mfanya ibada na matendo mema na kuwasaidia wengine wenye hali kama ya kwenu, wapeni moyo wenye hali mfano wa ya kwenu, waombeeni wengine walio kama nyie, toeni sadaka za shukurani kwa wenye mahitaji maalumu, tembeleeni wagonjwa, tembeleeni wafungwa tembeleeni wazee na wenye namna yoyote ya udhaifu wanahitaji faraja na tumaini.
Ikiwa mtajaliwa kufanya hivyo itawajieni amani, itawajieni furaha na tumaini, hamtayazama tena tatizo la mke wako kama hapo awali.

Amini kaka nakushuhudia mke wako atapona , kupona kusikotazamiwa wala kudhaniwa .

Binafsi nakuombeeni katika nia zangu hakika nitawaweka nanyi, mwenyezi Mungu yupo na ataonekana kweli katika maisha yenu.
 
Pole sana mkuu. Ni mtihani,kaza moyo.

Uliwahi ulizia kuhusu Butaro Cancer Center of Excellence? Ni kituo cha wamarekani,kipo Rwanda. Nimeonapo watu wengi wa nchi mbali mbali za Africa, sikufatilia kujua ila huenda wakawa na advanced technology kupunguza maumivu. Kupona sizungumzii.

Mgonjwa tuliewahi kuwa nae alitoboka shavu, ila mpaka anakufa, maumivu hayakuwa makali.

Labda ujaribu kufatilia uone kama watakuwa na la ziada
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…