Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Kansa ya matiti inammaliza mke wangu nikiwa nashuhudia, sina la kufanya. Sijui kama naweza kusahau hili

Ñaweza Sema ,ukweli ambao si mzuri kuusikia,
Mtayarishe mkeo kiroho.....wekeza nguvu nyingi kuponya roho yake I mean Muandae,ni ngumu ilà ni muhimu mweke karibu na Mungu kama kuna mila maagano ,dhambidhambi na mambo mengine ya ushirikiana na mambo ya ajabu Acha,
Amrudie Mungu ......aweza ponya roho yake asije akatwseka dunia na motoni.
# ni muhimu kuliko kuwekeza duniani.
Mtafute kiongozi wa kiroho eg tumia redio upendo
  • aungame
  • ajitayarishe KWA wakati wowote
 
Maumivu yakawa makali kiasi sindano za maumivu zikawa hazisaidii ikabidi awe anagewa cookies zenye bangi ndiyo anapoa baadaye dozi ya cookies ikazidishwa.

Tiba mbadala haikujaribiwa
Daaah aisee mpaka cookies za bangi?

Maimivu yalitokana na upasuaji ni kawaida saratani kuwa na maumivu?
 
Mkuu tafuta mtumishi wa kweli wa Mungu aweze kuombea hilo tatizo.Yasio wezekana kwa Mwanadamu Kwa Mungu yanawezekana bado ana nafasi ya kuishi.
Tuingie kwenye imani maana tumeshuhudia watu wakipona magonjwa makubwa na kama hayo na yale sio mazingaombwe.
Sawa kama
 
Mkuu pole kw ame wako kuumwa na maradhi ya Sratani ya maziwa aka Breast Cancer nitafute mimi kwa wakati wako ili nipate kumtibia mke wako.Kwani kutumia CHEMOTHERAPY kutammaliza mke wako taratibu atakwenda zake duniani kwani hiyo CHEMOTHERAPY haitibu Maradhi ya Cancer ya aina yoyote ile kwani CHEMOTHERAPY inauwa Cells zilizo hai na cells zilizo kufa kwa hiyo sio rahisi CHEMOTHERAPY kumponyesha mke wako unapoteza pesa zako bure hapo.

''Chemotherapy is an approach that destroy the Cells.
Chemotherapy doesn't distinguish between good cells and bad
cells. It destroys cells. It's an ACID Approach. -Dr.Sebi.
''Chemotherapy ni mbinu inayoharibu Seli.
Chemotherapy haitofautishi kati ya seli nzuri na mbaya
seli. Inaharibu seli zote. Ni Mbinu ya ACID. -Dkt.Sebi.
Ahsante sana dr, nikutafute kwa njia gani niweze kukupata
 
Pole sana mkuu, nakutumia inbox namba ya Mama mmoja yupo Morogoro, Mwinjilisti...... Mama yetu alikuwa na shida ya miguu lakini baada ya kumfahamu huyu mama,dawa siku ya kwanza tu.....mama anataka kuanza kucheza rede,anadawa za aina nyingi inawezekana akakusaidia pia
Mkuu hapa mpaka nimetabasamu kwakweli? Hivyo alipona kabisa?

Nitumie nitamtafuta . Nitafanya kila niambiwalo maana sijui msaada utatoka wapi
 
Nina thread ya kumpoteza kaka yangu mpendwa humu, Dr, christopher Kilongola wengi wanamfahamu, aliwahi saidia member watatu humu kwa tatizo kama lako, ila hatukujua kumbe yeye pia alikua muathirika wa cancer, na kusaidiwa watu ilikua ni research yake ili ajiponye, badluck alitutoka last 3 years.
Ndugu, kutana na madaktari, talk to them the world, nenda pale muhimbili, nenda pale ocean road, wapo vijana wanapambana na haya mambo, wanaweza kuwa na kitu, actually issue yako is too sensitive ila kutana na doctor, si kwa appointment ya matibabu, kutana nao ongea nao kama familia. Watakupa kitu,
Nimepoteza kaka na babu kwasababu ya magonjwa hatari kama ya mkeo, ila brother wangu did something yeye kama daktari, naamini yupo mtu sahihi na si dawa za kienyeji.
Mkeo ataishi usijali.
 
Pole sana mkuu
Chukua huu ishauri utanishukuru
Chukua majana ya stafeli changanya na maji masafi lita5 na majani yajae ndoo ndogo ya lita 10. Maji yachemshe hadi yawe ya moto then chukua hayo maji nusu lita saga na majani yamejaa chupa ya blender hadi majani na maji yaishe. Yaache yapoe mdogo mdogo masaa 12. Xhuja them mgonjwa yawe ndo maji yake ya kunywa. Unaweza kuongeza limao kuweka ladha na kamwe usiongeze kitu kingine ila kama ladha itakushinda basi ongeza tunda lenyewe ondoa tu mbegu blend ba maganda yake
Tumia hadi utakapopata nafuu
Ni ushauri nzuri kuhusu anticancer property ya soursop leaves ila concentration ni kubwa hiyo Kwanza atapata maumivu ya tumbo na inaweza mletea shida katika figo baada ya kutumia muda mrefu.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
yapata miaka miwili imepita tangu mke wangu alipogundulika ana saratani ya matiti, tulianza dozi ya CHEMOTHERAPY pale GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL ifakara, tulipatiwa jumla ya mizunguko 8 ya CHEMO, hali ilionekana kuwa nzuri ila ndani ya muda mfupi sana uvimbe ulianza tena.

Baada ya kuona uvimbe umeanza upya tulihamia dodoma BENJAMIN MKAPA napo tulipatiwa chemo 4 kisha ukafanyika upasuaji ili kuondoa titi lililo athirika na saratani, upasuaji amefanya mwezi wa 4 mwaka huu.

Baada ya upasuaji hali ilionekana kama ipo vizuri, ila baada ya miezi ipatayo mi 3 mgonjwa ameanza kusumbuliwa tena.
Anasumbuliwa na;
MAUMIVU MAKALI SANA MAHALA ALIPOFANYIWA UPASUAJI
KIDONDA KISICHO PONA (kilianza kidogo sana, kama kiji upele, hatimae kikakua. Hakionyeshi dalili ya kupona.

Najua yote ni mipango ya mungu, ila sina matumaini kama mke wangu anaweza kupona kwa sasa.

KUNA MTU ASHAWAHI KUUGUZA MGONJWA WA SARATANI naomba ushuhuda ambao unaweza nisaidia cha kufanya.

KAMA KUNA DAWA ZA TIBA MBADALA ULITUMIA ZIKASAIDIA, NAOMBA MSAADA PIA.

Kwa sasa mgonjwa yupo tu nyumbani tunasubiri neema ya Mungu

Ushauri wowote pia napokea.
Pole sana mkuu, Neema ya mungu na iwe pamoja nawe,

Pia mola akutie wepesi, kwa haya unayoyapitia ndugu.
 
Back
Top Bottom