Kanuni mpya za TFF ni za ovyo kupindukia; wanaendesha mpira kishamba sana!

Yeah ushauri mzuri
 
Mfano Yanga inadhaminiwa na sportpesa, je inawezekana Diarra binafsi akaingia mkataba na betpower? Yanga watakubali?
Yanga na TFF lao moja......wananyanyasa wachezaji. Hawewezi kukubali. Inauma sana.
 
Mmh sidhani kama ndio muarobaini wa hilo tatizo
Wewe unashauri tufanyaje mkuu? Kwa kuwa sasa unaona TFF wameshindwa kuendesha mpira, mm naona ni wakati muafaka wa kuiuza TFF kwa waarabu kama tulivyofanya kwenye bandari. Hakuna namna nyingine zaidi ya hii mkuu.
 
Mdhamini mkuu lazima aheshimiwe ,kama CRDB wanapesa wangekuwa wadhamini wakuu....Conflict of interest zipo kila mahali hivyo lazima kulinda maslahi ya mdhamini mkuu...TFF wapo sawa.
Mkuu acha kukanyaga haki za wachezaji. Maisha yalivyokuwa magumu hivi wewe unataka wachezaji wakaibe? Waacheni wachezaji wavune hela za wadhamini. Roho mbaya hailipi.
 
Ndio hapo hata mimi nashangaa. Hawa TFF ni wapumbavu sana.
 
CRDB adhamini ligi nzima halafu NBC adhamini wachezaji maarufu kama wanne hivi
 
Mdhamini ndio kaamua hivo, hao kina CRDB kama wanalipenda soka la bongo mbona hawakuja kipindi ligi haina mdhamini? Kaingia NBC nao ndio wanajidai kujitangaza kupitia wachezaji
 
Hiyo ni ulaya kibongobongo haiwezekani labda baadae sana tukiwa tuna uhakika wa wadhamini lukuki
 
Hiyo ni ulaya kibongobongo haiwezekani labda baadae sana tukiwa tuna uhakika wa wadhamini lukuki
Sasa uchache wa wadhamini ndio uwe kisingizio cha kukandamiza haki za wachezaji? Hii nchi imerogwa sio bure.
 
Sasa uchache wa wadhamini ndio uwe kisingizio cha kukandamiza haki za wachezaji. Hii nchi imerogwa sio bure.
Yaap lazima iwe hivo, ulaya mdhamini ukileta sheria zako ngumu unasepa wanakuja wengine, sasa sisi yenyewe kumpata tuu mdhamini ilikua mbinde

Au mnataka turudi tena kule ambako ligi haina mdhamini muanze kuitusi tena TFF kushindwa kutafuta wadhamini.

Hao wachezaji hawajakatazwa kuwa na wadhamini binafsi, mradi tuu asiwe mshindani wa NBC kibiashara, hata ingekua ni wewe umemwaga pesa zako kama NBC usingekubali washindani wako watangazwe na wachezaji wanaocheza ligi unayoidhamini wewe, tuache kuwa wanafiq kama sisiem
 
Hapa ndipo penye tatizo mkuu. Badala TFF waangalie maslahi ya wachezaji, wanaangalia matumbo yao binafsi. Hii nchi ni ya kipumbavu sana.
 
Mkuu mbona katika ligi ya England benki ya Barclays inadhamini ligi kuu lakini benki ya Standard Chattered wanaidhamini Liverpool bila shida? Tuache kuendesha mpira kishamba.
 
Mkuu mbona katika ligi ya England benki ya Barclays inadhamini ligi kuu lakini benki ya Standard Chattered wanaidhamini Liverpool bila shida? Tuache kuendesha mpira kishamba.
Mkuu nimeeleza hapo tofauti yao na sisi, wao ushindani wa kudhamini ligi ni mkubwa wadhamini ni wengi hivo masharti hayawi magumu

Sisi wadhamini ni wakutafuta kwa tochi hivo wakiweka masharti magumu kama hayo inabidi tuu tukubali maana kupata mdhamini ni ngumu

Hii ni Tanzania sio England , wale wapo mbele miaka 100 kisoka
 
Unalalamika Bure Ila tafuta maarifa ya kibiashara utaelewa zaidi. Unahitaji elimu! Elimu! Elimu. Refer sportpesa na 1×bet caf champions league. Pia soma zaidi kanuni na taratibu za udhamini. Yapo mambo,ikiwa huna uelewa nayo ni vyema ukatafuta ufafanuzi kwa wanaojua....sio kujifanya unajua kumbe unajishishia credibility.
 
Iko hivi epl inadhaminiwa na barclays, Ila kila club kinatafuta mdhamini ambapo Liverpool walimpata standard chartered kama mdhamini mkuu.....hakuna mgongano wa maslahi hapo Ila ndani ya Liverpool ikitokea Kuna mchezaji anadhaminiwa na nmb ya huko basi itasababisha mgongano wa maslahi na hapo muamuzi ni kanuni Ila sio mihemko. Ni sawa na caf champions league ilivyokuwa inadhaminiwa na 1×bet then vilabu shiriki vinavyodhaminiwa na betting companies nyingne viliambiwa vitafute mdhamini mwingine ndo yanga akampata Haier na Simba akaandika visit Tanzania.
 
Kabisa
 
Ondoa neno kanuni za tff ni za ligi ni za ligi kuu zimepitishwa na wenye viti na viongozi wa juu wa vilabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…