Dogoli kinyamkela
JF-Expert Member
- Nov 21, 2024
- 2,858
- 5,123
KANUNI YA CHANZO NA MATOKEO (THE LAW OF CAUSE & EFFECTS)
Ameandika Dr. dogoli kinyamkela 💀☠️
Kanuni hii ndio huitwa 'karma' na Wahindi.
Wakristo huiita "kanuni ya kupanda na
kuvuna".
Wanasema "apandacho mtu ndicho atakachovuna".
Kanuni hii inasema kwamba kile unachokitenda kwa watu wengine baadaye hurudi kwako kikiwa na nguvu zaidi kama matokeo ya matendo yako.
Kwa hiyo kama uliumiza mtu, baadaye maumivu hayo hayo lazima yatakurudia na kama ulimtendea mema mtu, huo wema utakurudia
maradufu. Haiepukiki.
Hivi mnajua ni kwa nini nguvu (nishati) ikienda lazima irudi tena?
Ni kwa sababu nguvu husafiri katika mwendo uzani,
kama tunavyoona bembea!
Ni sifa ya nguvu/ nishati.
Ukimsukuma mtu kwenye bembea, tarajia
kwamba ataenda na kisha atarudi, ndivyo ilivyo pia kanuni hii; ndivyo mwendo uzani ulivyo.
Kanuni hii unaweza ukaitumia kwa faida yako au kwa hasara yako pia (ni uamuzi wako tu)
Utakapomfanyia mtu kitu cha kuumiza, ile nguvu yako automatically itaenda, kisha ita-hit kwenye mwili wake wa hisia (emotional body) na huyo mtu ataumia sana; lakini yale maumivu
atakayoumia yatajikusanya kisha yataanza safari ya kurudi yalikotokea.
Kwa hiyo kila tendo ni nguvu, msisahau hilo.
Kama kuna tendo lolote umewahi kufanya, liwe
jema au baya, ni wazi utakuwa umeshapokea matokeo yake na kama bado hujapokea, basi ni
suala la muda, utapokea tu, fanya tu kujiandaa kwa sababu hii ni Kanuni, iko hivyo.
Niwape mfano kidogo wa haraka haraka, ni tukio la hivi karibuni.
Nikiwa mkoa fulani hivi majuzi kwa ajili ya semina fulani, nilikutana na 'mentor' wangu kwenye masuala fulani fulani, nikampatia pesa kidogo, shilingi laki tatu kama dhabihu ya kuendelea kujiambatanisha naye (uwa nafanya hivyo mara nyingi)
Ile nimemaliza kumkabidhi na akanibariki kwa matamshi ya kinywa chake, dakika kama 10 hivi, mfuasi wangu mmoja, anayeishi London, akanitumia dola 100!
Jioni ya siku ile nikalipia watu 5 ili walale kwenye Guest House, (shilingi elfu 75 tu) hawakuwa na pesa na walikuja kuhudhuria ile semina kwa mara ya kwanza.
Usiku nikapokea shilingi laki 2 kutoka kwa mwanafunzi wangu mmoja ambaye alisema nitafute lodge nzuri ya kulala kwa siku 2!
Unaona hayo maneno???!
Ni kupanda na kuvuna, kupanda na kuvuna!
Nimetoa mfano wa hivi karibuni, kwa sababu mimi sana sana nimejifunza kupanda na kuvuna lakini zaidi sana kwenye eneo la fedha; ndio maana sina mahitaji madogo madogo ya kifedha.
Nikitaka fedha ya haraka haraka, najua cha kufanya, natumia the law of cause and effects (among others); yaani nasababisha hela inifuate, napanda mbegu, kisha navuna baada ya muda mfupi, wa kati au muda mrefu kutegemeana na mahitaji yangu!
Kama mtu hana utamaduni wa kupanda mbegu iitwayo pesa, mahali sahihi (kwenye udongo mzuri), asitarajie kupokea pesa kwa njia rahisi kama ilivyo kwetu sisi.
Nizidi kuwasisitiza sana ndugu zangu, ukiamua kuumiza watu utavuna maumivu ya kukutosha.
Ukiamua kuwapa raha watu utavuna raha kama kawaida, tena kwa kipimo cha kujaa na kusukwasukwa!
Kwa hiyo uamuzi ni wako.
Kuna watu wengi wanateseka bila kujua ni kwa nini wanateseka na wafanyeje ili kutoka kwenye wingu hilo.
Ukifuatilia utagundua mateso wanayopitia baadhi ya watu ni kwa sababu hawajui kanuni hii vile inavyofanya kazi.
Unakuta ni wao
walioyatengeneza hayo mateso.
Swali ni "Je, unatokaje kwenye maumivu yaliyoletwa na karma mbaya?"
How to dissolve your bad karmas?
Je, kuna hali unapitia kwenye maisha na ukiifuatilia unagundua ni wewe uliyeisababisha kutokana na utendaji kazi wa kanuni hii ya chanzo na matokeo?
Kwa mfano, uliwahi kumfanyia jambo baya mtu au watu, lakini ulishasahau kwa sababu ilikuwa ni huko nyuma, miaka ya zamani, ila ukifikiria kwa muda unakumbuka?
Hebu jipe muda kufikiria.
Ukigundua kuna 'bad karma' unalipia, ufanye jambo ili kuipunguza nguvu.
Karma haiondolewi kwa kukemea.
Karma haiondolewi kwa kusali.
Unakuta mlokole kwa jina la Yesu, kwa jina la Yesu,
ninavunja, ninasambaratisha nk nk nk.
Karma haijui upuuzi wako huo, wewe umetenda, lipa,
simple.
Ni hivi, karma ni nishati, ni energy na unajua kabisa "Energy can neither be created nor destroyed, but can be transformed."
Therefore, Karma should
only be paid!
Sasa jinsi ya ku transform ndio muhimu.
Kuna njia mbili tu za kukabiliana na karma.
Njia ya kwanza ni SUFFERING. Kama uliumiza mtu, akaumia sana kihisia au kimwili, wewe utalazimika kupitia maumivu yale yale mara tatu zaidi kwa sababu sasa ni zamu yako.
Unalipia bad karma by suffering!
Suffering ni yale mateso au magumu unayopitia, we unaita changamoto!
Hiyo ndiyo njia ya kwanza ya kupunguza bad karma.
Suffering! Suffering! Suffering!
Njia ya pili ya kulipa NI KWA KUTOA SERVICE.
Service ni huduma ya bure.
Service ni
njia ya pili ya kutatua karma mbaya.
Service unaweza kuiita huduma kwa jamii (Charity)
Mifano yake ni kama kuhudumia wagonjwa, kuokoa uhai wa mtu au kiumbe chochote nk.
Unajua kuokoa uhai ni kama msaada kwa mgonjwa ambaye hakuwa na mtu wa kumsaidia, hivyo
angekufa.
Mnakumbuka mfano wa Msamaria mwema?
Nyingine ni msaada kwa fukara ambaye
angekufa kwa njaa.
Lakini uzito wa karma mbaya unatakiwa uendane na uzito wa karma nzuri.
Sio una zigo zito la bad karmas unafanya service ndogo ndogo, haitaendana na kwa sababu hiyo haitawezekana ku-dissolve
karma husika.
Mfano mwingine wa kupunguza effects za bad karma ni kufundisha.
Kufundisha inakuwa ni service kwa sababu maarifa yanaponya, yanauisha.
Kwa mfano nakufundisha wewe jinsi ya kujiponya cancer, unaenda ku apply steps unapona kabisa.
Kwa hiyo mimi nakuwa nimekusaidia wewe kuokoa uhai wako.
Au nakufundisha jinsi ya kuyasikiliza machale yako, unafanyia kazi na kujiokoa na ajari ya mauti.
Hapo nakuwa nimeokoa uhai wako kupitia service ya teaching.
Binafsi uwa natumia pia mbinu ya 'service' ku-dissolve bad karma, maana hakuna asiye na karma, iwe ni kwenye kizazi hiki au kilichopita, maana kila mmoja wetu aliyepo hapa duniani sio mgeni,
tumewahi kuishi kwenye generations mbalimbali zilizopita huko.
Kuna mengi tuliharibu,
tulikosea; sasa tumerudi kulipa.
Lazima tuchague tunalipa kwa njia gani; kwa njia ya suffering au service.
Sasa binafsi mimi nimechagua kulipa kwa kufanya service.
Nafanya Charity mara kadhaa, walau mara moja kwa wiki.
Pia natumia utaratibu wa kutoa offer kwenye services zangu zote kama njia ya ku-dissolve karma.
Mfano, kama Pete yenye Jiwe fulani bei yake halisi ni laki 7, nikakupa kwa laki nne na nusu, basi ile 250,000/- inayopungua, nakuwa nimeitoa kwako kama service au Charity.
Nafikiri sasa tumeelewana.
Tujitahidi sana kuwekeza kwenye matendo mema kwa jamii ili yatusaidie kupunguza bad karmas zetu.
Ahsanteni kwa kunielewa.