Kanuni za CAF Kuelekea nusu fainali

Kanuni za CAF Kuelekea nusu fainali

Yanga huwa wanajiaminisha sana ,tusubiri
 
Sasa hatuamini kiasi hiko kwamba tukose goli na alhly watoke droo?
Yaanii mshindwe kula Maini Bongo tuwaamini vipi kwenda kula Mfupa Egypt ilihali meno ni yale yale ?
 
Achakuwatisha wewe,hata wao wanayonafasi ya kushinda goli 2 kwa mtungi
Labda kama Simba wangemuazima Samson Mbangula mwamba anajua kupiga timu kubwa two goals bila majibu ukidhani anapiga kulia ye anaweka kushoto tena pale alipo kipa

Ila kolo haina namba 9 watafungaje sasa? Huko Cairo ni kichapo tu!

Bahati nzuri mechi itachezwa muda wa kula daku saa 5 usiku haitauma sana kukandwa tena maana wachache wataona, ukijilipua kwenda kibanda umiza ukirudi home geti limefungwa unarudi kibanda umiza kulala kwenye mabenchi!
 
Kanuni za CAF Kuelekea nusu fainali ;

◉ Hakuna dakika za nyongeza (Extra time) ikitokea timu zimetoka suluhu ndani ya dakika 90', mikwaju ya penati itaamua timu ipi isonge nusu fainali.

◉ Goli la ugenini litatumika ikitokea timu zimetoka sare. Aliyefunga goli ugenini ataenda nusu fainali.
Sawa mkuu
 
ya pili imekaa kishamba sana haifai na inatakiwa ifutwe.
Miaka ya 2020, nilikuwa nalipigia kelele away goal UEFA champions league,kwamba liondolewe,kanuni hiyo niliiona inamapungufu mengi sana kwa soka la kisasa.

Kuna wadau walikuwa wananipinga sana,,Ukisikiliza hoja zao ni za kusikitisha,Ati wawazidi wazungu wewe..?? & tulia wewe Mtu wa dunia ya tatu...!!

Hatimaye UEFA champions league waliondoa kanuni hiyo Msimu wa 2021/22.

Linapokuja suala la kubadili na kurekebisha Sheria na kununi za Mpira wa miguu na ungana kwa aslimia nyingi na Mzee Arsene Wenger.

Kanuni na Sheria zimewekwa na watu na zinaweza kubadilishwa au kuondolewa na watu vile vile,Mazingira na nyakati hubadilika.

Caf/Africa Sheria na kanuni nyingi zinamatobotobo kibao,mapungufu sana..na hizo nyingi huwapa sana faida watu wa kaskazini..

Sasa kuzibadilisha ,kuziondoa,kuziboresha yataka moyo na ujasiri,,

Wacha Tumtazame kwa makini Motsepe kama Ndie.

Naunga mkono goli la ugenini kuondolewa.
 
Naombeni elimu kwa matokeo haya itakuwaje ?

Mamelodi 0 - 0 Yanga ??
Mamelodi 1 - 0 Yanga ??
Mamelodi 2 - 0 Yanga ??
Mamelodi 2 - 1 Yanga ??
Mamelodi 3 - 0 Yanga ??
 
Back
Top Bottom