Elections 2010 Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama

Elections 2010 Kanuni za Uchaguzi 2010 na mgogoro wa Sheria ya Gharama

Status
Not open for further replies.
Serikali yakiri hoja ya Dk. Slaa nzito

na Kulwa Karedia

SIKU moja baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk.
Willibrod Slaa, kudai Rais Jakaya Kikwete amepotoshwa kuhusu sheria ya gharama za uchaguzi, serikali imesema itaomba radhi na kurejesha muswada huo bungeni.

Akizungumza na Tanzania Daima jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali,
Jaji Frederick Werema alisema: "Kama kweli ikithibitika, tuko tayari kuomba msamaha na kurudisha bungeni suala hili ili lifanyiwe marekebisho… namhakikishia Dk. Slaa kuwa tutarudisha bungeni ili makosa hayo yaondolewe.

"Siamini na si dhani kama ni kweli, kwa sababu eneo hilo nakumbuka lilijadiliwa kwa kina mno, tena Dk. Slaa na John Cheyo (Mbunge wa Bariadi Mashariki) walitoa mchango mzuri uliozua mjadala mrefu na hatimaye tukafikia mwafaka."

Dk. Slaa alidai
Rais Kikwete amepotoshwa katika baadhi ya vipengele, kikiwamo kipengele kinachohusu uthitibishwaji wa wajumbe wanaounda timu za kampeni kwa ajili ya wagombea urais, wabunge na udiwani.

Alisema
Bunge halikukubaliana kuhusu kipengele hicho, wala hakimo katika kumbukumbu za Bunge; na kwamba kiliongezwa baadaye, kabla ya Rais Kikwete kusaini muswada huo kuwa sheria.

Hata hivyo, Jaji Werema alishtushwa na kauli ya Dk. Slaa, na kudokeza kwamba inawezekana hata mwanasiasa huyo hakukielewa vema kipengele hicho.

"Nimeshutushwa na kauli ya Dk. Slaa… wasaidizi wangu wameniambia haya mambo, saa sijui tatizo liko wapi… nafikiri anapaswa kuelimishwa tu.

"Tunajua sasa zipo kampeni, hivyo kila mtu anataka kufanya au kufuatilia kwa makini sheria hii, sasa namshauri
Dk. Slaa aisome kwa makini," alisema Jaji Werema.

Alisema kumbukumbu zinaonyesha kuwa wakati wa kujadili muswada huo kila kipengele kilipitiwa kwa umakini wa hali ya juu na kuridhiwa na wabunge.

"Nakumbuka katika kumbukumbu zangu wakati tunajadili muswada huu tulipitia kipengele kwa kipengele; sasa haya mengine yatakuwa yametoka wapi?" alihoji Jaji Werema.

Alisema kama kweli kutakuwa na baadhi ya vipengele ambavyo vitakuwa vimechomekwa kwenye sheria hiyo kinyemela, sheria hiyo inaweza kurudishwa bungeni kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho haraka.

Akizungumzia sheria hiyo, juzi Dk. Slaa alisema anashangazwa na kilichotokea Ikulu siku Rais Kikwete aliposaini sheria hiyo.

Dk. Slaa alisema atamchukulia hatua mtu aliyehusika kuongeza kipengele hicho bila idhini ya Bunge.
Katika kushangaa huko, Dk. Slaa alionyesha kitabu cha kumbukumbu za Bunge (Hansard), ambacho hakionyeshi viongozi wanaopaswa kufanya uhakiki wa timu za kampeni za wagombea.

"Katika sheria aliyosaini rais kuna
kifungu cha 7 (3), ambacho hakikuwepo kabisa kwenye muswada uliojadiliwa na kupitishwa bungeni, kwa kweli nimeshangazwa sana, kwa sababu rais amedanganywa," alisema Dk. Slaa.

Kabla ya kuzungumza na Jaji Werema, gazeti hili liliwasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu, ili atoe msimamo wa Ikulu.

Alisema hana jibu, akamshauri mwandishi wa habari hizi kuwasiliana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, kwa kuwa ndiyo inayohusika zaidi na suala hilo.

"Sina cha kujibu katika hili, nakuomba uwatafute watu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, hawa ndio wako kwenye nafasi ya kuzungumzia suala hili kwa kina," alisema Rweyemamu.

Source: Tanzania Daima
 
huyu werema ndo sifuri kabisa...Kama mmempotosha rais kwa nini usijiuzuru ,hakuna kurudisha suala bungeni ni kuwajibika tu hapo
 
Hili la mswaada kupitishwa alafu kusainiwa na Rais kwanza ndio unaanza kutengenezewa kanuni nadhani unatoa upenyo wa watu kuanza kutafsiri muswaada tofauti. Kama hamna watu makini kama Dr. Slaa wanaotaka kusoma na kujiridhisha kuona je Nukta na Koma zimekaa mahali pake basi watu mnakuwa mmekwisha
 
Mnhhhh............. kama ipo hivyo.....basi kuna mengi yamechomekwa kwenye sheria zetu..................NAYE HUYO ANAYESAINI.........HIVI HUWA ANAKUWA NA RIFERENSI GANI WAKATI WA KUSAINI KWAMBA ANACHOKISAINI NDO KILE KILICHOJADILIWA.........???
 
Hata wabunge wengi wakishajadiri huwa hawarudii kusoma kile kilichosainiwa na kupitishwa kuwa sheria ili wajiridhishe kama ndicho walichojadiri. Kuna wabunge wachache sana wanaotaka kujiridhisha na wanaoshika sheria iliyopitishwa kulinganisha na mswada alafu ukilinganisha na makubaliano ya wabunge. Mswaada ukiwa na kurasa zaidi ya 100 unataka moyo kupita vipengere vyote hivyo. Kwa wenye macho ya Ngumbaru kama mimi ndio natambua ipi ni PhD original na ipi ya kutengeneza kariakoo kwa Hp Lesser Jet
 
hapo patamu!!! Lets see where the saga will fall!!
 
anaposema sidhani...anamaanisha hata yeye hajasoma? sifuri kabisa.
Mi wananichosha sana hawa jamaa!
 
hapo patamu!!! Lets see where the saga will fall!!
Naona kama vile wanatutengenezea jambo la kutufikirisha ili tusahau skendo zao nyingineeeee....mweheeeeeeeee.........TZ...........likitoka hili linafuata hili.........
 
Tena Mhe Rais aliusaini kwa mbwebwe hadhalani kumbe anasaini madudu, i can imagine alivyofura!
 
Hii ni wazi kwamba dhuluma haitapita kirahisi wataumbuka na kulazimisha lakini ukweli uko wazi . Hivi akina Mwakyembe ambao ni wana sheria sawa na Slaa wako wapi ?
 
Dr. Slaa please kama unauhakika na hilo, nenda mahakamani. Tuko nyuma yako, hata gharama za kesi ni(tu)tachangia, naamini tuko wengi ambo tumechoka na kufanya wajinga.
Tafadhali lifikishe kwa Spika wa bunge rasmi na tusikie msimamo wake. Mahakamani ni lazima...huu ni uhaini.
TZPride,

Asante. Lakini sasa ndio naelewa jinsi watanzania wengi wanavyokuwa hawaelewi issues.

1) Swala siyo kwenda mahakamani, kwa sababu hata ukienda mahakamani, na ukashinda kitakachofanya mahakama ni kutua hukumu, Rulling,( uamuzi) kuwa jambo hilo lirejeshwe Bungeni, kwa sababu sheria ikiisha kutungwa haina namna ya kuiondoa isipokuwa kwa njia ya " Miscellaneous Amendment" au hata "amendment ya Sheria nzima. Kwa hili ni Miscellaneous amendment kwa sababu sehemu yenye mgogoro ni para mmoja tu yaani 7(3). Miscellaneous Amendment ni utaratibu unaotumika kufanyia marekbisho vipengele vya Sheria, (iwapo ni vichache au ni kimoja).

2) Katika hatua ya sasa, mahakama siyo siyo suala la urgency iwapo tunataka uchaguzi wa 2010 usiathirike na kipengele hiki. Mahakama ina utaratibu wake, ambao hata ukipeleka under certificate of urgency, utaenda kwa utaratibu wake kama ilivyo swala la " Mgombea Binafsi" wote mnajua lilianza lini, na hata baada ya Mahakaa Kuu kuamua bado linasuasa, na sasa ndio tunasubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufaa, tarehe 8 April, 2010 nadhani kama sijakosea na au haitabadilika. Hivyo Bunge la April, yaani mkutano wa 19 ndio wa mwisho unaojadili miswada ya Serikali. Bunge la June-Julai linajadili tu Bajeti ya Serikali ( au mswada utakaoletwa naSerikali chini ya Hati ya dhararua kama ipo). Hivyo, nafasi pekee ya kawaida ni Bunge la April, ndio maana ninasukumu Serikali itakiwe as a matter of urgency kuleta Miscellaneous Amendment hiyo Bunge la April, yaani Wiki mbili zijazo.

3) Watanzania wafahamu pia ukiingia mahakamani umeihalalishia Serikali iliyochomeka hoja hiyo, kama ilifanywa kwa hila au makusudi, isilete Miscellaneous Amendment kwa kuwa suala litakuwa mahakamani. Swala lililoko mahakamani haliwezi kujadiliwa Bungeni and vice Versa( in most cases japo kuna exception hapa). Hivyo suala la kwenda mahakamani ambayo hujui litaisha lini sio priority kama kuitaka Serikali ilete irejeshe hiyo hoja haraka Bungeni.

4) Swala la mahakamani ni kutaka aliyehusika na kuchomeka kifungu hicho ambacho kinaweza kuwa Forgery afikishwe mahakamani, au basi kuchukuliwa hata hatua za kinidhamu. Hizi ni hatua zinazoweza kwenda kwa mkondo wake, hata baada ya amendment kufanyika. Nadhani sasa hoja inaeleweka vizuri. Naomba radhi kama nimetoa kwa kirefu lakini niliona elimu ya jinsi Bunge linavyofanya kazi ni muhimu ili wote tuweze kushiriki katika mjadala tukiwa na level mmoja.
 
Kuna kitu hapa wanakificha kabisa ila kama ndio sheria imepitishwa kama hivi basi kunapaswa Watanzania wote wajulishwe kabisa
 
Slaa huwa haropoki!
Waberoya,

Thanks. Nadhani sitaki kujisifu, lakini huwa ninajitahidi kufanya Research ya kutosha kabla ya kutoka Tamko. Inawezekana kabisa Tamko ninalotoa lisiwe kamili kabisa kila wakati kwa sababu mbalimbali. Lakini katika hili sina mashaka na utafiti wangu. Ndio maana nilichukua nyaraka zote husika na nikazilinganisha. Hakuna namna jambo lolote likaingia kwenye Sheria kama " angalau hata wazo hilo" halijawasilishwa na kujadiliwa na Bunge. Ni kwa maana hiyo, in the Interest of transparency na ukweli, ninawatumia hapa Barua niliyoandika kwa Spika wa Bunge. Ninafanya hivi kwa sababu zifuatazo;-

i) Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa ninamheshimu sana, jana katika Taarifa ya Habari ya TBC1 (TV) alinukuliwa kuwa " hakuna udanganyifu, na kuwa hakuna kipengele kilichoingizwa bila kupitia Bunge". Kwa Bahati mbaya, inaelekea dhahiri Spika wangu hakufanya utafiti wowote, na ninathubutu kutumia neno "alikurupuka kujibu hoja aliyoulizwa na mwandishi wa habari bila kufanya utafiti".

ii) Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kama alivyonukuliwa na Gazeti la Tanzania Daima, pia "alikurupuka", lakini angalau alikuwa mnyofu kuonyesha katika maelezo yake kuwa hajasoma wala hajafanya utafiti wowote yeye binafsi, bali alielezwa na vijana" wataalamu wake".

Iwapo Mhe. Spika na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa Serikali wangelifanya utafiti niliofanya, kulinganisha nyaraka zote husika, basi angeligundua kuwa "mjadala pekee uliokuwepo Bungeni" ambao AG ametaja waliosika akinitaja na mimi ulihusu tu, swala aliloleta Mhe. Andrew Chenge, kuwa baada ya neno "Voter" lililotwa katka Schedule of Amendment iliyoletwa na Serikali inayoanzisha kifungu kipya cha 7(2) yaongezwe maneno "including food, ...." haya yote yalikuwa yanahusu gharama za Makundi ya Sanaa yatakayokuwa yanatumika na mgombea. Makundi ya Sanaa ni kitu tofauti kabisa na "campaign Team".

Katika mjadala huo uliochukua muda mrefu, na hatimaye kuhitimisha na Mwenyekiti wa "Kamati ya Bunge Zima" ambaye siku hiyo alikuwa Mhe. Naibu Spika, hakuna popote swala la " Approving Athority" limesemwa, wala kujadiliwa, wala kuamuliwa na Bunge.

Ndiyo maana ninasisitiza Mhe. Spika na Mhe. Mwanasheria Mkuu, ni vizuri tu wakawa waungwana, na ukweli ukasemwa, ili hatua stahiki ikachukuliwa kulinda Demokrasia. Ah, wakiamua kutumia mabavu, vyombo vingine vitafanya maamuzi, na wakati huo historia itawahukumu, tatizo ni kuwa tu iwapo watachagua njia hiyo, Demokrasia itakuwa imeathirika kwa "Timu za Kampeni kuthibitishwa (approved na watu wasio husika, tenda watendaji wa Serikali ambao siku zote wamelalamikiwa kuiegemea Chama Tawala).

Naambatanisha Barua iliyoenda kwa Spika kwa rejea ya kila mmoja wa wana JF.(naona nimeshinda kutuma) nitaituma separately
 
Kweli Slaa ameonesha umakini katika ufuatiliaji,Nafikiri kwa kipindi hiki hakuna kiongozi mwenye kiwango kama chake,yawezekana wapo baadhi ya viongozi wameliona hilo lakini wamekuwa waoga kusema.Kama suala hilo ni la kweli,basi Rais atakuwa amedanganywa mengi.
 
Asante kwa kutuelimisha kuhusu procedure za bunge na kwa nini suala hili si la kukimbilia mahakamani nakutakia kazi njema
 
Hii sheria haina budi kuangalia tena na kufanyiwa mabadiliko yanayohitajika; vinginevyo itakapoanza kuuma ndiyo watu wataanza kujipanga nyuma kutaka mabadiliko. Itakuwa ni kisingizio cha kutaka uchaguzi uahirishwe.
 
huyu werema ndo sifuri kabisa...Kama mmempotosha rais kwa nini usijiuzuru ,hakuna kurudisha suala bungeni ni kuwajibika tu hapo
Kama tungekuwa na mila kama hiyo nchi yetu ingeendelea sana. Bahati mbaya hata Raisi hatamshauri hivyo! Badala yake humkumbatia!!
 
Dr. Slaa,

Fanyeni petition Uchaguzi Mkuu uahirishwe hata ikiwezekana ufanyike December au Sheria hii mpya isitumike kabisa mwaka huu, na ianze kupitiwa upya na kufanyiwa kazi.

Je Bunge na Bungeni hamuwezi kupiga kura kusitisha muswaada huu kuwa Sheria?

Naunga mkono hoja...The best way ni kuahirishwa kwa uchaguzi ili mambo yakae sawa kwanza.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom