Kanusho la kuwepo kwa Mayai ya Kuku kutoka nje ya Nchi yaliyosababisha kushuka kwa bei ya Mayai Nchini

Kanusho la kuwepo kwa Mayai ya Kuku kutoka nje ya Nchi yaliyosababisha kushuka kwa bei ya Mayai Nchini

WANAKANUSHA NINI wakati rais alienda kenya kufungua fursa, arusha kilombero yako kibao yanaingia kwa njia za panya.
Mkuu 'ANKOJEI'' hebu pata picha hii:

Mayai toka Kenya yauzwe Tanzania kwa bei ya chini zaidi kuliko yanayozalishwa nchini:

Hao wakenya wananunua malighafi ya kutengenezea chakula cha hao kuku, kama mashudu, mahindi toka hapa hapa Tanzania; halafu wapate gharama ya kusafirisha hadi huko kwao; walishe kuku wao na wasafirishe tena mayai kuyaleta hapa Tanzania wayauze kwa bei ya chini na bado wapate faida kuliko mzalishaji wa hapa hapa!

Hii picha ipo vizuri kweli, au kuna kitu hakionekani?

Kama ni kweli mayai toka Kenya yanauzwa hapa kwa bei ya chini zaidi, basi kuna umuhimu wa Wizara husika ilifanyie kazi jambo hilo, kwa sababu haieleweki kabisa kwa nini iwe hivyo.
 
Mkuu 'KeyserSoze', inawezekana kweli "unashindwa kuelewa", kwa mfugaji anayefuga kuku 100,000 huko Marekani, anavyoweza kumshinda mfugaji wetu hapa Tanzania mweye vikuku 1,000 kwa sababu haya mambo huyafahamu vizuri.

Hilo siyo kosa lako; kosa ni huko kudhani kwamba huyo wa kuku 1,000 ataweza kuhimili ushindani kwa mazingira ya hapa nyumbani.
Hayo Mayai yametoka Marekani ?

Kuweza kushinda kwenye world market inabidi hata huyo mwenye kuku mia au mia mbili aungane na wengine na kutengeneza umoja (Umoja ni nguvu) unadhani Kenya kila mtu anafuga mmoja mmoja ? Watu wanaungana na kutafuta masoko kwa pamoja...

Hili la kuzuia ili mwananchi atoe pesa mara mbili unasahau kwamba ile pesa ambayo angesave kwenye mayai angenunua tikitiki au mguu wa kuku hence kumsaidia yule mkulima wa tikiti au mguu wa kuku...

Bila kuungana na kununua vyakula kwa pamoja na kutafuta masoko kwa pamoja kila leo watakuwa wanalia bidhaa zisitoke nje (wanasahau hata tulio ndani hatuna buying power ya kutosha hence ni mwendo wa kuumizana na kutiana umasikini tu)
 
Hapa, sijui kama yanatoka Marekani au la, wewe unajuwa?

Kwani haiwezekani yakatoka Marekani, yakapitia Kenya na kuja kuuzwa hapa?

Hapana tena ya pili, kuhusu hilo la watu kuungana huko Kenya na kutafuta soko hapa Tanzania. Hilo nalijuwa wazi kwamba siyo hivyo. Ninawafahamu vizuri sana wafugaji wa Kenya, hawana tofauti yoyote na hawa wa hapa kwetu.

Kuhusu hilo la "kuzuia ili mwananchi atoe pesa mara mbili", binafsi siliangalii hivyo, na wala sidhani kwamba ndiyo matakwa ya wizara husika.

Nitakuelewa vizuri sana ukihimiza hiyo wizara au serikali iweke mipango bora kwa wafugaji wetu ili nao waweze kuzalisha kwa bei nafuu, hilo tungeelewana zaidi kuliko kushabikia wakulima wetu waondolewe kazini.

Hilo la "kuungana" siyo jambo baya, ni jambo jema sana, lakini sasa hivi halipo. Mpaka wafugaji wetu watakapoungana na kutafuta masoko kwa pamoja, kwa hali iliyoelezwa hapa hapatakuwepo na mkulima wa kuungana naye tena, kama serikali itajiondoa moja kwa moja kuwalinda hao wakulima na kuwaongoza katika kuunda umoja unaouzungumzia wewe.
 
Lisemwalo lipo...
Kuna kitu hakiko sawa kwenye hiyo taarifa ya wizara, kwani yapata wiki sasa bei ya mayai kwa dar imefikia 6500 kwa tray moja (bei ya jumla)toka 8000!! Mimi sioni tatizo kwani inaonekana kwa sasa mayai kutoka kenya yameanza kuingizwa nchini, na hata suala la vifaranga vya nyama, kipindi cha mwenda zake, alipiga marufuku kuingizwa kukawa na shida kweli ya vifaranga, kwani wazalishaji wa ndani wahatosherezi soko, wakaja na masharti kibao kuwa ili kupata vifaranga lazima vianzie 500, na ununue chakula kutoka kwao cha vifaranga hao 500!!!wenye mitaji ya kuunga ikawa balaa!!
 
Back
Top Bottom