Kanye West aanzisha Biblia yake, ajiita Mungu

Kanye West aanzisha Biblia yake, ajiita Mungu

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,580
Reaction score
1,987
Mwanamuziki wa kufokafoka wa Marekani, Kanye West ameibadilisha biblia inayotumiwa na Wakristo kwa kuweka jina lake badala ya Mungu.

My take: Utajiri ukizidi ni shida
===================

aaa-kanye-horz.jpg


Kanye West Hujulikana sana kwa maringo yake,lakini kwa kweli Kanye West asingekufuru na kujitambulisha kama mungu katika biblia hiyo.

Kitabu hicho kitukufu kimebadilishwa na kuwa Biblia ya sasa kwa jina ''Yeezus'' na amini usiamini kila neno la Mungu katika kitabu hicho limeondolewa na badala yake msanii huyo wa muziki wa kufoka foka ameweka jina lake.

Kulingana na gazeti la The Independence nchini Uingereza,kitabu hicho kinasema kuwa katika kizazi hiki ,Kanye West ndio mkubwa na vilevile kiongozi wa kidini


Kitabu hicho kinaongezea kwamba ''katika utangulizi wetu tunamsherehekea Kanye West na vile alivyotufanyia katika maisha yetu''

Kanye West na mkewe Kim Kardashian Ijapokuwa Kanye hajatoa tamko lolote kuhusu wadhfa huo aliojipatia,amekuwa akijifananisha na Mungu hapo mbeleni.

''Mungu alinichagua mie,alinitengezea njia.Mimi ni chombo cha mungu'',alisema mwaka 2009.

''Lakini kinachoniudhi maishani mwangu ni kwamba sitawahi kujiona nikicheza muziki moja kwa moja''.,aliongezea.

Wasanii wengine waliofananishwa na Yeezy ni Marilyn Monroe na Michael Jackson. chanzo.BBC

Pesa ukiwa nazo nyingi haya ndio Matokeo ya kukufuru Kanye West moto wa jahanamu utakuhusu kesho.



Chanzo: BBC Swahili
 
Binadamu anguko lake li karibu kabisa...huwezi fanya kufuru kubwa namna hii... Ila fimbo ya Mungu itafanya kazi; Yaani Kanye aliumba mbingu na nchi? Akasema kuwe na jua na kila kitu kikawa?
Money is the source of all evils indeed
 
Hakunaga binadamu ninayemchukia hapa duniani kama kanye West!
 
Uchizi na umburula uko wa aina nyingi,hapo sio Kanye ila Kanyea!
 
"so y'all better quit playing with god"
Listen I am a god by kanye west
 
dah kila mtu ana dhambi zake ila hakuna dhambi mbaya kama hii. Jamaa sasa kavuka mipaka na kanisa kaanzisha Mungu atamfundisha ---- huyu.
 
Kwanza, Kanye yuko hivyo alivyo toka kitambo, hoe'ing 4 attention kwa namna yoyote. Hajaanza leo kujifanananisha na Mungu.

Pili, Hii mnavyo-panic hapa na kuupa muda wenu upuuzi wake, ndio ushindi kwake, kifupi y'all dancing to his tune.

Tatu na muhimu, kwani Mungu wako wa kawaida kiasi gani, mpaka hata taahira akijilinganisha nae au kumkashifu unapagawa?

Kifupi Kanye na wanaomtumia wanacheza na akili zenu, ukifungua macho hizi issue unaziona na hazikusumbui.
 
Back
Top Bottom