Kanzu ni vazi amazing, basi tu...

Kanzu ni vazi amazing, basi tu...

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Leo nimegundua napenda sana mwanaume akivaa kanzu. Kanzu ina usexiness fulani hivi sijui kwa sababu asili yangu ni Pwani.

IMG_3623.JPG

Kanzu nyeupee halafu awe ananukiaaaaa...na makobazi fulani. Huwa napenda sana Ijumaa nikiwa Kariakoo nikipishana na waislamu na kanzu zao manukato kama yote.

Ila kanzu uwe na “swagg” or else utaonekana kama pipa.

IMG_3624.JPG

Ladies, ni mimi tu nina maruhani na kanzu au kuna wenzangu huko?

IMG_3620.JPG

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
[emoji23][emoji23][emoji23]kweli mwingine anaweza kua kama pipa kama hiyo picha inavyojieleza.

Mimi kanzu hapana
Huyajuwi mambo.

Mwanamme kanzu.
Swali lililonijia kichwani kimasihara..., tofauti ya kanzu na dera ni nini? Ukiachilia tofauti ya majina....

Hayo mavazi ni maalum au mahsusi kwa......
Diraa ni vazi la kuvaa nyumbani kwa mwanamke si la kutokea kama wafanyavyo kwetu, Tanzania.

Kanzu ni vazi la mwanamme la kiheshima, zipo kanzu za kutokea na zipo kanzu za kutokea na hata akienda karibu karibu na nyumbani basi anavaa hizo tu zinafaa.

Sijawahi kutoka nje ya mlango wa nyumbani kwangu na diraa. Tena napenda zaidi kuvaa kanzu za mume wangu, zile za nyumbani za cotton nikiwa nyumbani.

Tanzania utakuta mwanamke kavaa diraa au kikoi ndiyo eti nguo ya kutokea. Khaa! Majanga.
 
Sasa sisi tunaovaa jeans kila siku msibani tutavaa nini madam kama sio diraa?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Sasa sisi tunaovaa jeans kila siku msibani tutavaa nini madam kama sio diraa?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Kuna kaftan, kuna Punjabi dress, kuna marob (robe), kuna magauni (gowns), kuna jilbab, kuna khanga na vitenge unaweza kubuni mishono yenye staha na "comfort' kuna mitandio aina mbali mbali.

Zote hizo zipo "design" nyingi tu na zinapendeza kuliko madiraa.

Hayo ma "jeans" yenyewe mnayovaa siku hizi yanabana mpaka pumzi haitoki, ukilivua sehemu si harufu hiyo ya jasho imechanganyika na ya mashuzi, na nyie mmo tu, wanawake kwa wanaume. Khaa! Inahusu nini?
 
Jasho linategemea na aina ya mwili. i rarely sweat kwakweli.

Nashukuru kwa somo ngoja nikagoogle nijielimishe kuhusu hizo aina za nguo
 
Hili vazi nilijua ni la waislam tu ila kuna wahaya walikuja kuoa kwetu na wote walikuwa wamevaa kanzu na koti na wote ni wakristo nilishindwa kuelewa kuna uhusiano gani kwa wahaya na hili vazi
 
Mkuu hilo vazi ni tamaduni/vazi la waarabu,sio kwamba linavaliwa na dini fulani tuu,yeyote anaweza kuvaa haina shida,tatizo watu wamekariri.
 
Uganda pia hulitumia kwa wanaume wanao oa.

Back
Top Bottom