Kaponea chupu chupu kugongwa na Koboko mkali

Kaponea chupu chupu kugongwa na Koboko mkali

Black-Mamba-Dendroaspis-polylepis-from-near-Durban-KZN.-Copyright-Johan-Marais-40.1-768x1152.jpg

Koboko huwa hana utani.
 
Mkuu Koboko hana mazoea ni kiumbe hatari.
Ni kweli kabisa mkuu ila tumeishi na watu wa maeneo ya urambo sehemu moja kama unaenda kaliua kuna watu hawana uoga kabisa.

Sasa nilishindwa kujua ni madawa au kwasababu wengine madogo tu miaka kama 12, wanakupa maelekezo wapi utampata mida gani anapendelea kutembea na namna gani anakamtwa kwa biashara na wazee wa mitishamba.

Kitu kilicho nifanya nikaja kuamini baada ya kuanza kufatilia kipindi cha Simon channel ya National Geographic Wild namna anavyomkamata na tahadhari kubwa sana anazochukua kumkabili hadi kumkamata.

(Very interesting bush kule anachomewa dawa tu analegea mlevi akasomeee wabongo kwa vitu hivyo mmh 🙌🙌) Nilidata.
 
Nilichogundua kuhusu hawa Viumbe ni kwamba mchana wa jua kali ndio wanakuwa wakali sana ni vigumu kusikia kuwa Koboko kamgonga Mtu usiku.
 
Nilichogundua kuhusu hawa Viumbe ni kwamba mchana wa jua kali ndio wanakuwa wakali sana ni vigumu kusikia kuwa Koboko kamgonga Mtu usiku.
Na wazee (expert wa pori) wanakwambia pia usiku mara nyingi anajishtukia kwasababu kuna viumbe wengine nao wanamtegemea kama msosi.

Ila ninachomkubali ni kwamba ana tabia ya ustarabu mmekutana mazingira hujamuona anakupotezea na mishe zako, siyo nyoka aina ya swila atataka mpaka msumbuane mmoja amkatae mwenzake mtikasane walau kidogo.
 
Nilikutana na Swila mmoja mkubwa Mweusi katikati ya Katavi karibu na pale alipotupwa Sativa ilikuwa 2013 yule Swila akagoma kutoka Barabani ikanibidi nisimame nikazima Gari ndio akaondoka.

Alikuwa mkubwa kuliko huyu.
004127-3.jpg
 
Mimi na nyoka ni vitu viwili tofauti kabisa, nakiri kuwa kama mwanamke pindi nikimuona nyoka, nawachukia na kuwaogopa
Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo 2000's tulikuwa tunaishi mazingira ambayo nyumba ilikuwa mstari wa mwisho karibu kabisa na mlima yani mwanzo kabisa wa kuanza kupandwa huo mlima kwahiyo kuna msitu na mawe yenye kutengeneza mapango kulikuwa na project ya kutotolesha vifaranga.

Kwahiyo mara nyingi sana kesi ya kutembelewa na kenge na nyoka ilikuwa kawaida sana, siku moja majira kama ya 12 na nusu tukiwa viwanjani huko vijana kama kawaida nyumbani pale alibaki mama na watoto Sasa akiwa anapika jikoni (mazingira ya kota nadhani unaelewa) anatoka kufata kitu ndani anakuta swila mkubwa sana nyuma yake alianguka pale pale kwa presha bahati ni kwamba hakuangukia moto wala lile dude alikumdhuru likakimbilia ndani.

Kwahiyo kuna kijana wa kuhudumia mifugo ndiyo kwenda kutoa taarifa kwa wazee waliokuwa zamu muda huo getini walienda wawili tu swila akasanda tunarudi tunakuta watu kibao nyumbani ndiyo kupewa huo mkasa hapo bi mkubwa bado HOI.!

HUYO SWILA UKIMUONA unajisemea tu kwa yeye ana haki ya kuzimia.
 
Huyu Mwanamama wa Kinaijeria mwenye Travel Blogger anayoenda kwa Jina la Go.Ebaide anazunguka Afrika kwa kutumia Pikipiki na sasa yuko Tanzania wakati akitokea Kigoma kuelekea Mpanda amekoswakoswa kugongwa na Koboko mwenye hasira sana aisee!!..

Anabahati sana aisee!!!...

View: https://youtu.be/vNfcf5-FX5Q?si=cNb8ezJGtIsQJvNC

View: https://youtu.be/_i0ABGNY-_k?si=tSKOniq_7KCAEqDD

Ngoja kwanza, kwanza hatujaendelea naomba tujadili hili:
1. Kuna Basi moja nimeliona la rangi ya buluu Limeandikwa Mashujaa Football Club. Hivi Mashujaa kumbe wana basi zuri
2. Ni aina gani ya Lenzi anayotumia huyo mwanamama, maana naona inabendisha watu/vitu balaa!!
 
Back
Top Bottom