Kaponea chupu chupu kugongwa na Koboko mkali

Kaponea chupu chupu kugongwa na Koboko mkali

Nasikia huyu nyoka ni kichaa hua anakukimbiza sasa hapo vipi mboni kaishia kujinyanyua tu?
Mambo ya kusikia mara nyingi huwa yameongezwa chumvi. Nyoka anapojinyanyua ili aone kwa macho yake hafifu, anuse kwa kutoa ulimi wake nje aweze kujua nini kinachojiri - ni adui au ni chakula/mawindo. Kama ni adui, nyoka anajificha chap' au anakimbia au kama ni karibu mno (taken by surprise) anajiweka tayari mkao wa kupambana. Kumbuka nyoka hana uwezo wa kuona mbali na hutegemea sana uwezo wake wa kusikia vibrations kwa kutumia tumbo lake.
 
Dah! Hilo li dubwana liko fasta sana, hapo angepanic tu ingekuwa habari nyingine.
Ni kweli kabisa. Inashauriwa uwe una kaa mbali na nyoka esp. wale wanaotema mate (spitting snakes) walau zaidi ya mita tatu kwa sababu uoni wa nyoka ni hafifu haoni vizuri umbali zaidi ya m3 na kwa hiyo hatoweza kukulenga shabaha kamili machoni au puani kwa mate yake.
 
Kumbe huwa haoni mbali vizuri?
 
Mhm kwel naogopa kinyonga mno , hakuna nyoka ananitisha.

Note, siwezi wala sipendi kitu kinaitwa uongo labda ukute ni wrong information tu.
kuna watu hawakuamini najua kwa hilo

lakini mimi pia huwa siogopi nyoka wala kinyonga wala wadudu wengine wengi

mimi ata kama nyoka ameingia ndani najua kakosea njia tu namtoa aendelee na mishe zake uko njee

ila sasa kuna kipindi cha mvua kwa mikoani kunakuwa na wadudu ukishawataa ndani wanaingia aiseh wananikosesha raha nakuwa very weak baada ya kuwaona

nawaogopa kichizi mpaka watu wanashangaa
 
WP_20240822_10_45_57_Pro.jpg
Mhm kwel naogopa kinyonga mno , hakuna nyoka ananitisha.

Note, siwezi wala sipendi kitu kinaitwa uongo labda ukute ni wrong information tu.

kweli kila mtu ana kitu anaogopa sana kuliko kawaida kuna watu wanaogopa sana nyuki lakini upande wangu

nawapenda sana huwa nawawekea asali waje angalau waje niwaone jinsi wanafanya kazi

basi nafurahi sana ila kuna jamaa wangu huwa hataki ata kumuona huyo mdudu
 
Kumbe huwa haoni mbali vizuri?
Ndiyo. Haoni mbali kwani kile kitendo cha kutambaa humnyima fursa ya kuyaona mazingira yanayomzunguka (poor vicinity augmentation) kwa mapana yake. Lakini pia macho yake yana layers mbili layer ya kwanza ungeweza kuifananisha na mtu aliyevaa miwani na layer ya pili ndo jicho halisi. Sasa endapo layer ya kwanza imechafuka kwa vumbi au uchafu mwingine au ni kwa uzee hapo vision yake inakuwa hafifu (blurred) kwani inasababisha au inaweka kiwingu dhidi ya ile layer ya pili (jicho halisi). Na kadri kitu kinavokuwa mbali ndo inakuwa shida kwake kukiona. Ila akijikoboa (kujitoa gamba), walau huwa anaweza kuona vizuri lakini hii ni kwa muda kidogo kwani kukua na kukomaa kunaendelea. ( ref.Growth and Aging)
 
Mhm kwel naogopa kinyonga mno , hakuna nyoka ananitisha.

Note, siwezi wala sipendi kitu kinaitwa uongo labda ukute ni wrong information tu.
UKWELI ni huu hapa kumhusu Kinyonga(Chamelion). Kinyonga HANA sumu yoyote.
Vitisho na mbwembwe zote za kinyonga ni ili adui asimsogelee na asimdhuru. Lakini waweza kumshika, kumnyanyua, kumruhusu atembee juu ya mwili wako e.g. kichwani, mgongoni n.k. na hatakudhuru kwa namna yoyote ile. Cha msingi tu ni wewe umpende na usimdhuru kwani hana madhara kwako.
 
kweli kila mtu ana kitu anaogopa sana kuliko kawaida kuna watu wanaogopa sana nyuki lakini upande wangu

nawapenda sana huwa nawawekea asali waje angalau waje niwaone jinsi wanafanya kazi

basi nafurahi sana ila kuna jamaa wangu huwa hataki ata kumuona huyo mdudu
Ni sahihi kabisa. Binadamu tunatofautiana katika mengi. Wapo baadhi ya watu waking'atwa na nyuki japo mmoja tu, anaweza kudhurika kiasi cha kuwa admitted hospitali ilhali wapo wengine hata nyuki kumi na tano yy anaona kawaida tu na anaendelea na mishe zake.
 
Kwa wa mjini hii kitu ni hatari mno , ila kwa sisi vijana tulio kulia manyara miaka ya 90 hivi vitu ni vya kawaida mno
Mimi nikiwa darasa la pili umanda huko tabora vijijin unasikia bimkubwa anaita we ujoka washa koroboi uingie ndani ukatoe linyoka limeingia saiv yasije kuzaliana na lile jingine lililongia jana
 
Kwa wa mjini hii kitu ni hatari mno , ila kwa sisi vijana tulio kulia manyara miaka ya 90 hivi vitu ni vya kawaida mno
Ila sio koboko mkuu. Mbona shemeji zangu wa Manyara wana akili na hekima, we mbona umekuwa kilaza na mjinga? Mbona sasa umekuwa mzabibu mwitu wakati ulikuwa mzabibu mzuri.

Usiwaige hawa akina Kiranga huku mtandaoni. Huyo ni msukuma na wasukuma wengi wanasumbuliwa na ushamba. Yupo mastate huko ila bado ana usukuma ndani yake. 😀😀😀😀

Karibu kwa Yesu tena, bado anakupenda shemeji yangu.
 
Asante
 
Back
Top Bottom