Kapt. Mkuchika na Maagizo yake!


Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba sisi JF hatuna tofauti na hao waandishi wahabari, sisi iso waandishi wa habari, sisi ni wananchi tu toka njia nyingi za maisha tunaokuja kutoa maoni yetu tu, au? sio lazima tujje uandishi wa habari!
 

Sasa hapo ni tofauti Mwanakijiji,wataalamu wanasema in every professional there is a black sheep,sasa ni kazi ya hizo professional bodies kusimamia masuala mazima ya nidhamu na utendaji kazi unaofuata maadili.Hata hivyo kusema waandishi wasomee sidhani ni kuesema kuwa waliopo sasa ambao hawajasomea waache kuandika kama inavyotafsiriwa na wengi (na nafikiri hii ndio hofu) hapana, nadhani kusema hivyo ni kukosea.Elimu iwe pale watakao bahatika kuipata wataipata watakaoikkosa kwa sababu moja au nyingine wataikosa,na kuondoka kwa tabaka lile lisilosomea litatokana na industry yenyewe sio sheria,itakuwa tu ni survival of the fittest.Wee utaona tu automatically hufit kwenye mfumo utaamua tu mwenyewe kwenda kutafuta japo certificate, tofauti na wale correspondent wengine ambao sio waandishi ila wanatumia taaluma zao kama waandishi mf.katika safu za uchumi,sheria,kilimo nk,wenyewe kwa walivyo ni wataalamu wa fani hizo,wataendelea kutoa michango yao kwa kutegemea uhariri wa mhariri wa chombo husika,lakini wale wanaohitaji kuwa wana practice kama their main professional ni vema wakaipata hii elimu,maana mie nadhani itawasaidia zaidi kuliko kuwaharibia.
 

Unajua sifa ya kisomo ya mbunge ni kujua kusoma na kuandika tu wala katiba haisemi japo awe na elimu ya kidato cha nne au walau ajue kiingereza na kiswahili. Katika hili kwa kweli nakuungeni mkono kuwa tuanze na wabunge wenyewe kuhamasisha elimu kama kigezo cha ubunge,sio elimu ya juu sana hapana ni elimu ya kawaida tu kidato cha nne.Hii itasaidia uelewawao katika mambo mbalimbali pale bungeni,tusiishie kuwasema waandishi tu.
 
inanikera sana kuona watu wanakuwa na uelewa mdogo katika jambo hili. wengi wa watu wanaopinga hii hoja humu ni waandishi wa habaru makanjanja na nahisi mnapinga ili kulinda ajira zenu. mimi nawashauri muende shule kwanza. OK. siamini kama watu wenye akili wanaweza kusema kuwa degree haihitajiki kwenye uandishi wa habari. hamjui kuwa ktk shughuli hiyo kuna kanuni na sheria nyingi sana mnazotakiwa kuzifuata ili msikolaidi na sector zingine za kazi za watu waliowazunguka? ndo maana lazima muende shule mkapikike kwanza.mnaboa kishenzi hapa tz, na kuna siku mtaondoka wote waje waliosomea. the day is coming. mnatutia aibu sana. tunapenda na we wish kama waandishi wa habari wetu hapa bongo mngekuwa safi na fit kama waandishi wenzenu wa nchi zingine. mnatumiwa kama instruments za kulipiza visasi vya watu tu, mnanunulika sana, habari mnazotafuta ni zile ambazo hamjazitafuta, bali mmepigiwa simu na watu wakawawekea mafuta kwenye gari zenuna hela ya kula, ndo mnakuja kuzitoa na kumfagilia.

Lakini, wakati mwingine, ni tatizo la waajiri wenu, hawana hela ya kutosha kuwalipa qualified ones, so wanawachukua makanjanja tu alimradi mnaingiza vihela. najua kama akiajiri watu waliokolifai vizuri, mtaji unaweza ukaishamaana atawalipa hela kubwa.

tunachohitaji,kama habari inatolewa ya kiuchumi, mtu aliyesomea uchumi anaejua kuuelezea uchumi na akaenda kusomea uandishi pia. kama sheria hivyohivyo, kama any other social thing vivyohivyo. hatutaki mtu anaeleza vitu asivyovijua,ndo maana mnaongeza tu jazba kwa wananchi hata zisizohitajika.
 
Jamani, nimeonelea niongee kidogo. hapa tunatakiwa kuongea mambo yatakayookoa heshima ya waandishi wetu iliyoporomoka kitaifana kimataifa tayari. kwa mtazamo wangu, nafikiri, kama vile nchi zingine zinavyofanya, ili mtu awe mwandishi wa habari mzuri, lazima awe amesoma taaluma mbili. ya kwanza ni ile ya specialization yake, na ya pili ni ile ya uandishi wa habari.mfano, kama mtu ni reporter wa uchumi, lazima asomee uchumi na baadae akasome uandishi. ndo ataongea kitu anachokijua akiwa guided by the principles za uandishi alizosomea. kama mtu anaripoti vitu vinavyohusu sheria, asomee sheria kwanza halafu ndo aende akasomee uandishi wa habari, atakuwa anakijua anachoongea na atakieleza kwetu wasikilizaji vizuri. akiwa reporter wa mambo ya social, aende akasome socialogy pale na baadae akasomee uandishi. vivyohivyo kwa mainjinia wetu na matechnitian n.k. huu ni mfano mzuri.

Tatizo ni kwamba, vyombo vyetu vya habari havina uwezo mkubwa kuajiri watu wa namna hiyo kwasababu watahitaji kulipwa hela kubwa sana kwa elimu hiyo. mimi nimesomea sheria jamani, ukisema nireport mambo ya kiuchumi siyajui, ila kama kuna sehemu sheria imevunjwa, ukinituma niripoti mwenyewe utapenda na utaelewa, society itaelewa kabisa.

pia waandishi wetu waliowengi hawafanyi utafiti, wanaandika tu kitu wanachosikia. hebu angalia Tido mhando alivyotia aibu juzi, Ze komedi ndo wameishitaki Tbc, sio eatv, lakini yeye kwasababu amesikia kwenye magazeti,bila hata kufanya utafiti, tayari amesharipoti kwenye media...hahaha.

kwa mtindo huu, mtawatia waajiri wenu kwenye hasara, mtapigwa faini sana za defamation,na kesi zenu huwa ni za kuomba hela nyingi. mtu unamchafulia jina anakwambia umlipe bilioni tano, sasa si ndo kufilisika hivyo? hamkuona aibu sana siku sumaye alipopata million mia moja kama fidia juzi tu pale, na akawaaibisha kuwa, hizo hela hazili ila anaenda kuwapa watu wanaosomea uandishi ili wawe waandishi wazuri? hakuna kitu kinaitwa kipaji kwenye uandishi, wala kwenye utaalamu wowote, ndo maana watu tunaenda shule, ingekuwa hivyo, tusingekuwa tunaenda skuli wazee. waandishi wetu wanatia aibu sana jamani.
 
hahaha, umesema kweli. nakuunga mkono asilimia mia moja, people like JERI MURO hatuwahitaji hapa tz, wanatuaibisha. waende shule tena au wahame taaluma wakawe waalimu labda, ila sio waandishi wa habari. good job.
 
Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba sisi JF hatuna tofauti na hao waandishi wahabari, sisi iso waandishi wa habari, sisi ni wananchi tu toka njia nyingi za maisha tunaokuja kutoa maoni yetu tu, au? sio lazima tujje uandishi wa habari!

FMES,

Basically what I am saying is if we are to hold anyone accountable, we need to hold ourelves accountable.

Ninachoongelea ni uandishikuandika si uandishi wa journalism.

Ukiangalia habari za Tanzania na waandishi wa habari (journalists) kuna makosa mengi sana katika kazi zao. Grammatic errors, lack of facts even flow of news.

Infact independent individuals wanaoandika makala huwa na mpango mzuri sana wa makala na maoni wanayoandika, lakini ukifungua IPP, Tanzania Daima, Uhuru, Daily News unakutana na habari ambazo hazijahakikiwa (edit).

Pamoja na uhuru wetu hapa wa kutoa maoni na ni wazi kuwa sisi si Waandishi wa Habari (journalists), lakini kanuni zakuandika (writting) hatuko exempted kisa tuko JF.

Tunapoanza kuwa na double standards katika maisha na kazi zetu, tunafungulia sanduku la kukosa kuwajibika.

Ni sawa na mtu ambaye akiwa kazini, akienda msalani hasafishi mikono kisa yupo kazini, lakini akirudi nyumbani anasafisha na kusugu ahata akienda kukojoa.

Kama tunataka quality ya fani ya habari Tanzania ikue na kuheshimika, ni wajibu wetu sisi kabla hatujawapigia kelele waandishi wa habari, kuwa ni watu wa ovyo na hawana mpango mzuri au hawajui kuandika, tujiulize, je sisi tunafuata hizo kanuni tunazotaka watu wengine wafuate?

Aidha kuna tofauti kati ya kuandika makala kutumia maoni ya anayeandika na kuandika kitu kuwa ni factual bila kuwa na proof.

Mfano mzuri nitautumia ni wakati ule kijana JMushi alipotangazia umma kuwa ana proof kuwa Daudi Ballali ni Daudi Kinyaga na wanapelekeana message za simu. It was stated as a fact, but proofof matter is that JMushi stumbled on a searchengine that he did not comprehend how it works and declare to public his findings.

Sasa kama angekuwa ni mwandishi wa habari wa gazeti (journalist) na mhariri wake akaridhia kuwa kila kitu ni mswano bila kuhakiki na ku check facts na kugundua makosa, then gazeti kama lingechapisha hiyo habari kuwa Ballali ni Muganda, lingeaibika wakati ukweli ulipotokea.

Ndiyo maana kuna maneno mawili ambayo ni kinga nzuri yanapaswa kutumika wakati wa kuandika kitu ambacho kinaonekana kuwa ni factual. Maneno "inasemekana" "inasadikiwa", hata ukiongeza "tuhumiwa", haya yanampa kinga yule anayeandika habari ambayo inaonekana kuwa ni factual, lakini anayeandika (iwe journalist au Rev. Kishoka) hana uhakika au hana ushahidi kamili wa anachoandika.

Sasa tactic hii inatumika kama chumvi au chambo ili kusaidia kupatikana kwa proof na hivyo jambo libadilike kuwa factual.

Nafikiri nimeeleweka.
 
vipi kwa issue ya kuhoji mtu laivu halafu unabolonga kama Jeri muro?,sisi hatuna haja ya kujiuliza kama tunazo hizo ethics na taaluma za uandishi wa habari kwasababu sisi hatufanyi kazi hizo, tuna taaluma zingine. isipokuwa kwa uelewa wetu na jinsi tunavyolinganishana waandishi wa nchi za wenzao, tunaona wanabolonga halafu wanaboa.media inaajikuta inaangukia sehemu ya kuwafagilia watu binafsi au kuwaumiza watu pasipo sababu ya kufanya hivyo. mchungaji wewe vipi tena.
 

Rev ninakuskia sana, lakini bado niansema hivi, sio wote hapa waliokwenda formal shule kwa kuongelea shule, na haipaswi kuwa a must kuwa member hapa, waandishi wa habari ni pro na ni kazi yao,

Hapa watu utnaandika kwa uwezo mbali mbali, na kwa nafasi mbali kuna ambao wanalipia mtandao kwa hiyo wanakuwa na haraka kuwahi time ya heal zao hawawezi kuandika inavyotakiwa, kuna wanaoiba mitandao kazini, kuna wanoazima mitandao ya watu, kuna ambao wamejisomesha wenyewe, kuna kila aina ya watu hapa na kuandika, sasa hivi ninapoandika nipo safarini na sina muda mrefu sana kwa hiyo ninajaribu kuandika fast as I can sasa siwezi kaundika kama inavyoatkiwa, that is my point,

Hoja kwamba na sisi lazima tuwe kama waandishi, binafsi siioni kuwa na nguvu sana, ni wajibu wetu kama wananchi kuwa-hlod responsible waandishi wetu, na ndio hasa nia na madhumuni ya wengi wetu kuwepo hapa, ni kurekebisha habari, lakini uandishi sio lazima sana cha muhimu mimi nilifikiri kuwa ni hoja tu, yaani hapa JF,

Lakini wajibu wetu kuwa-hold responsible waandishi wakiandika habari mbovu, lakini kuandika kwa umakini hapana hilo hatuliwezi kwa wananchi wote, cha muhimu ni hoja nzito na ndio hasa zilizotupelekea kufungiwa wakati ule, ilikuwa ni hoja nzito sio uandishi, au?
 
The need to have a free press, which includes a press with no artificial barriers on entrance to it's corps, is paramount and supersedes the concerns about quality of journalism. Standards can be enforced on an ad hoc basis, this will still guarantee quality journalism without sacrificing freedom and innovation.

Einstein failed in school, if the scientific institutions and administration of the Annalen der Physik, leading German Phyusics Journal circa 1905 was as rigid as Mkuchika in accepting papers for publication, we probably would have been delayed the opus that is "The Theory of Relativity" by several years if not decades because Einstein did not have the required scientific credentials.But they looked at the paper, not the person.

The Theory of Relativity turned out to be arguably the most important Physical Theory of the last century, informing engineers on rocket trajectile, astronomers and cosmologist on the motions of the celestial bodies, and engineers on the calculus of Global Positionisng Systems.

And still some people want to entertain some form of medieval guilds!
 

Well, how come you borrowed a page from Mkuchika's playbook then:
Then unakuta muandishi aliyesomea Ilala School of Journalism ambaye haujui mlango wa library una rangi gani, ana quote sensationally, then unamkuta airhead mmoja huko Zenj kama Shamhuna, anamburuza huyu mama naye kwenye mijadala ya local politics.

Explain why I shouldn't call you Mkuchika's poodle, Mr. Cosmologist.
 

Kuhani said

Well, how come you borrowed a page from Mkuchika's playbook then:

Implying I got the below from Mkuchika's book

Then unakuta muandishi aliyesomea Ilala School of Journalism ambaye haujui mlango wa library una rangi gani, ana quote sensationally, then unamkuta airhead mmoja huko Zenj kama Shamhuna, anamburuza huyu mama naye kwenye mijadala ya local politics.

Kuhani akatukana

Explain why I shouldn't call you Mkuchika's poodle, Mr. Cosmologist.

That the complexity of my analysis is certain to baffle you to the point of insulting my mental capacities with the above unflatterring distinction is of no surprise to me, knowing well your capacities or quite likely lack of.

Instead of being enraged at the mere entertainment, if not outright suggestion, of that unwarranted but perfectly explainable betrayal of apparent slightness -for the real slightness is not of my character, to the contrary, of your reasoning and comprehension- I will take the challenge of trying to explain the apparent, albeit nonexistent wave particle duality like contradiction.

There is a valid concern about the quality of journalism in our country, anybody disputing this ought to have his head examined.So anybody taking issue with the quality of journalism is justified.That includes me in that supposedly self contadicting post.

As I explained in an earlier post, given that there are some genuine concerns about the quality and standards of journalism in Tanzania, freedom of the press takes a more important place than the effort for a more educated/ regulated fleet of journalists. As such if given the choice of a mix of quality and shoddy journalism that is afforded freedom and a super educated ultra-modern intellectual journalist's club, which is overregulated and only play fiddle to the government's tune,I would settle for the first one, knowing that issues of quality and standards can be settled on an ad hoc basis, by ways of fines, readership involvement, litigation and even self education.

So you can see there is no contradiction at all, a person can very well believe that Tanzania's journalism stinks but still not agree with Mr. Mkuchika's proposal for an overregulated and therefore stifled press.

Murphy said everything appears be be much easier that it really is, your analysis of my analysis included.I guess my analysis of your analysis of my analysis included as well, time will tell.
 

Pundit nae anasema ametoa point ati....hahaha. Pundit, wewe mtu wa aina gani....
 
Nakubaliana na wewe . Nafikiri umeongea ukweli (Truth). Nao ndio kikorombwezo muhimu cha Uandishi wa Habari.
 
Pundit nae anasema ametoa point ati....hahaha. Pundit, wewe mtu wa aina gani....

Sasa wewe unaye dispute point usiyoionyesha, na bila wala kuonyesha counter argument yako ndiye utakuwa "mtu wa aina gani" hapa for sure. regardless ya point yangu.

Watu wanajua kuji shoot themselves sijawahi kuona.
 
Nakubaliana na wewe . Nafikiri umeongea ukweli (Truth). Nao ndio kikorombwezo muhimu cha Uandishi wa Habari.

Ukweli ni kwamba, ingawa kuna concerns genuine kuhusu quality na standards za uandishi (hili halibishiki, anayebisha mwehu) kuna jambo lingine ambalo ni muhimu zaidi ya standards za uandishi ambalo tukiruhusu wanasiasa wenye ambitions na nia za kisiasa ku control nani anaandika na nani hawezi kuandika, tutakuwa tunarudi nyuma, hili linahusu uhuru wa kujieleza na uhuru wa vyombo vya habari.

Lets say kuna mtu anaweza kuhamasisha watu kama anavyofanya Mwanakijiji hapa, ana uchambuzi mzuri, ana sources nzuri, ana passion na uandishi, kajisomea mwenyewe na mambo anayajua kuliko hata hao waliosomea rasmi.Kwa sababu huyu bibi anayajua sana haya mambo, na ana mvuto sana anaandika katika lugha iliyo "accessible" kwa wananchi, anakwenda straight to the point bila ya meanders za kisomi, watu wanampenda sana na anaweza kuhamasihsa jamii vizuri sana.

Wakina Mkuchika wanamsikia anatajwa tajwa, mara hili mara lile, hawapendi, wanaona tutamsimamishaje huyu bibi? Wanasema hebu mtafuteni tuangalie elimu yake.Kama hana degree ya uandishi tunampiga marufuku kuandika. Wanakuta kweli hana degree, amekuwa "home schooled", wanampiga tight na unakuwa mwisho wa habari.

Hiki ndicho mnataka? mnajua wakipitisha haya mambo ya "hakuna kuandika mpaka uwe na degree/ certificate" deeper implication ni nini? Hii haina maana kuwa gazeti haliwezi kuwa na anonymous contributors/ reporters? Kwamba itabidi kila makala iwe na jina? Kwamba itabidi ndiyo uwe mwisho wa M. M Mwanakijiji na wenzake kama yeye wanaotumia pen name kuandikia magazeti ya Tanzania? Manake kama objective ni kuhakikisha kila anayeandika ana degree au certificate ya uandishi, si itabidi ujue mwandishi wa kila makala ni nani ili kusudi pasiwe na faker asiye na degree/ certificate akaandika? Otherwise whats the point? How can this be enforced?

Je mnaelewa ukubwa wa hili jambo ninaloongelea?

Siyo kwamba natetea waandishi vihiyo, waandishi vhiyo hata mimi wananikera sana, ila naelewa kuwa hili swala linaingia katika freedom of speech and freedom of press.Linawakuta unfavorably siyo tu vihiyo, bali hata ma intellectuals wenye misimamo mikali lakini wanaotaka privacy ya anonymity.

I am not sure if you can see where I am coming from.
 
Date::8/4/2008
Waziri apiga marufuku wimbo wa taifa katika simu
Na Clara Alphonce
Mwananchi

WAZIRI wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika amepiga marufuku wananchi kuweka wimbo wa taifa katika simu zao za mkononi.

Mkuchika alisema kufanya hivyo ni kuudhalilisha wimbo wa taifa pamoja na nchi kwa ujumla kwani inapaswa kuheshimiwa mahali popote .

''Unakuta mtu ameweka wimbo wa taifa kwenye simu yake ya mkononi halafu anapopigiwa ama yuko kwenye ulevi au mahali kwingine ambako wimbo huo hauhitajiki, hakika tunaokosesha heshima kama wimbo unaowakilisha utaifa wetu,'' alisema.

Aliongeza kuwa nyimbo nyingine zinazosifu Tanzania zinaruhusiwa kutumika kwenye simu, lakini sio wimbo wa taifa.

Alisema pia kuwa wizara yake inaandaa utaratibu wa kupitia sheria zetu iliiweze kuruhusu wananchi wote kutumia bendera ya taifa kama zilivyo nchi nyingine.

Waziri huyo aliyasema hayo wakati akikabidhi bendera ya taifa kwa timu ya Olimpiki inayoondoka leo mchana kwenda Beijing, China.

Mkuchika aliwapa wanamichezo hao salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye ameitakia timu hiyo kila la heri na kuitaka ihakikishe inarudi na medali na pia kuwa na nidhamu kwa muda wote watakapo kuwa huko.

Timu hiyo inaondoka na wanamichezo 10 wakiwemo wanariadha nane na waogeleaji wawili, akiwamo Mkuchika.
 
Hivi bado tunayo timu itakayotuwakilisha katika Olimpiki au ni watalii tu?
 
Mimi nilisema huyu bwana Chekist Gestapo watu wakasema ooh, anataka waandishi wa habari waende shule, sijui professional.

Na bado, atawakagua watu mpaka chupi kama wamefua.
 
Actually mimi naona kuwa na ringtone ya Mungu Ibariki ni moja ya njia za kuonyesha uzalendo wako kwa nchi yako. Lakini hili lijamaa halioni hilo.....jamaa shamba kweli yaani....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…