Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba sisi JF hatuna tofauti na hao waandishi wahabari, sisi iso waandishi wa habari, sisi ni wananchi tu toka njia nyingi za maisha tunaokuja kutoa maoni yetu tu, au? sio lazima tujje uandishi wa habari!
FMES,
Basically what I am saying is if we are to hold anyone accountable, we need to hold ourelves accountable.
Ninachoongelea ni uandishikuandika si uandishi wa journalism.
Ukiangalia habari za Tanzania na waandishi wa habari (journalists) kuna makosa mengi sana katika kazi zao. Grammatic errors, lack of facts even flow of news.
Infact independent individuals wanaoandika makala huwa na mpango mzuri sana wa makala na maoni wanayoandika, lakini ukifungua IPP, Tanzania Daima, Uhuru, Daily News unakutana na habari ambazo hazijahakikiwa (edit).
Pamoja na uhuru wetu hapa wa kutoa maoni na ni wazi kuwa sisi si Waandishi wa Habari (journalists), lakini kanuni zakuandika (writting) hatuko exempted kisa tuko JF.
Tunapoanza kuwa na double standards katika maisha na kazi zetu, tunafungulia sanduku la kukosa kuwajibika.
Ni sawa na mtu ambaye akiwa kazini, akienda msalani hasafishi mikono kisa yupo kazini, lakini akirudi nyumbani anasafisha na kusugu ahata akienda kukojoa.
Kama tunataka quality ya fani ya habari Tanzania ikue na kuheshimika, ni wajibu wetu sisi kabla hatujawapigia kelele waandishi wa habari, kuwa ni watu wa ovyo na hawana mpango mzuri au hawajui kuandika, tujiulize, je sisi tunafuata hizo kanuni tunazotaka watu wengine wafuate?
Aidha kuna tofauti kati ya kuandika makala kutumia maoni ya anayeandika na kuandika kitu kuwa ni factual bila kuwa na proof.
Mfano mzuri nitautumia ni wakati ule kijana JMushi alipotangazia umma kuwa ana proof kuwa Daudi Ballali ni Daudi Kinyaga na wanapelekeana message za simu. It was stated as a fact, but proofof matter is that JMushi stumbled on a searchengine that he did not comprehend how it works and declare to public his findings.
Sasa kama angekuwa ni mwandishi wa habari wa gazeti (journalist) na mhariri wake akaridhia kuwa kila kitu ni mswano bila kuhakiki na ku check facts na kugundua makosa, then gazeti kama lingechapisha hiyo habari kuwa Ballali ni Muganda, lingeaibika wakati ukweli ulipotokea.
Ndiyo maana kuna maneno mawili ambayo ni kinga nzuri yanapaswa kutumika wakati wa kuandika kitu ambacho kinaonekana kuwa ni factual. Maneno "inasemekana" "inasadikiwa", hata ukiongeza "tuhumiwa", haya yanampa kinga yule anayeandika habari ambayo inaonekana kuwa ni factual, lakini anayeandika (iwe journalist au Rev. Kishoka) hana uhakika au hana ushahidi kamili wa anachoandika.
Sasa tactic hii inatumika kama chumvi au chambo ili kusaidia kupatikana kwa proof na hivyo jambo libadilike kuwa factual.
Nafikiri nimeeleweka.