DOKEZO Karagwe: Watu wengi hawajaweza kuunganishiwa umeme kutokana na gharama ya kununua nguzo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Ukitaka kuunganishiwa umeme, unatakiwa kununua nguzo kwa gharama ya Shilingi 300,000 kwa kila nguzo. Ikiwa utahitaji nguzo zaidi, utalazimika kulipia kila nguzo kulingana na mahitaji. Gharama ya kuunganishiwa umeme ni Shilingi 150,000.

Kwa hiyo, kwa kiasi kikubwa, watu wengi hawajaweza kuunganishiwa umeme kutokana na gharama ya kununua nguzo kuwa sehemu ya mchakato huo.
 
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi.

Tafadhali fahamu kuwa nguzo ni mali ya TANESCO. Wakati wa kuomba kuunganishiwa huduma ya umeme, mteja hutozwa gharama kulingana na tathmini itakayofanywa na mtaalamu wa vipimo pamoja na vifaa vitakavyobainika kuhitajika.

Baada ya mteja kufanyiwa vipimo na kukamilisha malipo ya huduma, muda wa kuunganishiwa huduma huwekwa kulingana na umbali uliobainishwa na wataalamu wetu. Kwa kawaida, mteja aliye ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo huunganishiwa ndani ya siku 30, aliye ndani ya mita 60 ndani ya siku 60, na umbali unaozidi mita 60 unaweza kuchukua hadi siku 90.

Hata hivyo, si lazima mteja asubiri hadi kufikia siku hizo. Huduma inaweza kukamilishwa mapema kulingana na utaratibu wa kiofisi.

Asante. ^FL
 
Je bei aliyotaja ni sahihi? Kwa nguzo.
Asante
 
Je bei aliyotaja ni sahihi? Kwa nguzo.
Asante
Habari, ndugu mteja.

Hatuuzi nguzo, bali bei ni kutokana na tathmini kufanyika na watalamu wetu. Bei ni kama ifuatavyo:
  1. Gharama za kuunganisha umeme ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,
  2. Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,
  3. Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=
  4. Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,
  5. Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,
  6. Umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.
Bei pia huweza kubadilika kutokana na tathmini zingine kutoka kwa watalamu wa vipimo.

Asante. ^FL
 
Habari, ndugu mteja.

Tunaomba kesho, ufuatilie taarifa zetu kupitia mitandao yetu ya kijamii, kwani tunatarajia kuwa na taarifa kuhusu suala hili.

Asante. ^CM
Nilisikia kuna gunzo za mradi sijui mkifika watu 10 na pesa ya nguzo nguzo zinamwaga nyingi zaidi au inakuwaje kwa walio mbali na nguzo mfano kupata umeme mpaka nguzo tatu
 
Habari ya asubuhi, mteja wetu.

Katika Uunganishaji umeme serikali imefanya kazi kubwa kupunguza gharama kwa mteja ambaye eneo lake linahitaji nguzo moja hadi mbili zote bei yake ina ruzuku. Kwa eneo linalohitaji zaidi ya nguzo moja hapo kuna mambo ya kuangalia. Mfano eneo linaweza kuwa linahitaji kujenga laini mpya kabla ya kuunganisha wateja ndiyo hapo kauli yako ya mradi inapotokea.

Aidha,ujenzi wa laini hiyo unaweza kwenda sambamba na kuweka transifoma mpya.

Jambo la muhimu la kuzingatia, ili kujua mahitaji ya eneo lako lazima wataalam wa TANESCO wapime na kubaini mahitaji ya eneo husika.

Kutokana na eneo husika ndipo wanaweza kushauri kipi kifanyike na kwa wakati gani kinaweza kufanyika.

Asante. ^HN
 
Ukitaka kuunganishiwa umeme, unatakiwa kununua nguzo kwa gharama ya Shilingi 300,000 kwa kila nguzo. Ikiwa utahitaji nguzo zaidi, utalazimika kulipia kila nguzo kulingana na mahitaji. Gharama ya kuunganishiwa umeme ni Shilingi 150,000.

Kwa hiyo, kwa kiasi kikubwa, watu wengi hawajaweza kuunganishiwa umeme kutokana na gharama ya kununua nguzo kuwa sehemu ya mchakato huo.
Unaponunua sukari mwenye duka anakuwekea kwenye mfuko! Tanesco nao mfuko ni nguzo kwa mteja!! Kwa nini unanunua?
 
Habari ndugu mteja,
tafadhali tunapenda kukufahamisha kuwa TANESCO hatuuzi nguzo bali tunatoa huduma ya kuunganisha umeme kulingana na mahitaji na umbali uliopo baina ya mteja na miundombinu yetu.^HN
 
Wakiunganisha hata kama ni mbali, baada ya mda ile faida inafidia nguzo! Nguzo ni BURE. Kuna wakati waziri mmoja aligusia hilo ila immediately akapewa "speed governer".
 
Habari ndugu mteja, asante kwa kuwasiliana nasi.

Tafadhali fahamu kuwa nguzo ni mali ya TANESCO. Wakati wa kuomba kuunganishiwa huduma ya umeme, mteja hutozwa gharama kulingana na tathmini itakayofanywa na mtaalamu wa vipimo pamoja na vifaa vitakavyobainika kuhitajika.

Baada ya mteja kufanyiwa vipimo na kukamilisha malipo ya huduma, muda wa kuunganishiwa huduma huwekwa kulingana na umbali uliobainishwa na wataalamu wetu. Kwa kawaida, mteja aliye ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo huunganishiwa ndani ya siku 30, aliye ndani ya mita 60 ndani ya siku 60, na umbali unaozidi mita 60 unaweza kuchukua hadi siku 90.

Hata hivyo, si lazima mteja asubiri hadi kufikia siku hizo. Huduma inaweza kukamilishwa mapema kulingana na utaratibu wa kiofisi.

Asante. ^FL
Acha uongo wewe admin. Nguzo tunauziwa laki tano wewe unasema siyo mali ya mteja
 
Acha upumbavu wewe admin. Nguzo tunauziwa laki tano wewe unasema siyo mali ya mteja
Ndio, ndugu mteja. Sio mali ya mteja kwa maana katika kuunganishwa, kuna gharama zingine zinazingatiwa katika zoezi la kuunganisha umeme ndo maana sio nguzo tu inaletwa, bali na vifaa vingine.

Asante. ^HN
 
Nimelipa 600,000+ recently, kilichonishangaza ni Tanesco kuweka nguzo ndani ya kiwanja(kuna mawe ya upimaji yanaonekana). Mimi sitahamgaika kuwatafuta ila hio nguzo yenu mtaikuta ndani ya fence yangu.
 
Wakiunganisha hata kama ni mbali, baada ya mda ile faida inafidia nguzo! Nguzo ni BURE. Kuna wakati waziri mmoja aligusia hilo ila immediately akapewa "speed governer".
Habari, ndugu mteja.

Ndo maana tumesema kua nguzo ni mali ya TANESCO na hua gharama zikitozwa ni kutokana na huduma inayotelewa ya kumuunganishia mteja na huduma ya umeme.

Asante. ^HN.
 
Nimelipa 600,000+ recently, kilichonishangaza ni Tanesco kuweka nguzo ndani ya kiwanja(kuna mawe ya upimaji yanaonekana). Mimi sitahamgaika kuwatafuta ila hio nguzo yenu mtaikuta ndani ya fence yangu.
Habari, ndugu mteja. Asante kwa kuwasiliana nasi.

Pole sana kwa changamoto hii, na tunakushukuru kwa kutufikishia taarifa. Tafadhali tutumie mtaa/kijiji, kata, wilaya, mkoa pamoja na namba yako ya simu, ili tuweze kufanya ufuatiliaji na kukupatia msaada unaohitajika.

Unaweza kututumia taarifa zako kupitia inbox yetu. Tutahakikisha suala lako linafanyiwa ufuatiliaji kwa haraka.

Piga 180.

Ni chap watakuwa hapo kuihamisha.

Ikiwa ndani ya fensi yako nafikiri wewe ndiye unahatarisha usalama wako,wale vijana huwa vibarua tu wala hawana cha kupoteza.
 
Habari, ndugu mteja. Asante kwa kuwasiliana nasi.

Pole sana kwa changamoto hii, na tunakushukuru kwa kutufikishia taarifa. Tafadhali tutumie mtaa/kijiji, kata, wilaya, mkoa pamoja na namba yako ya simu, ili tuweze kufanya ufuatiliaji na kukupatia msaada unaohitajika.

Unaweza kututumia taarifa zako kupitia inbox yetu. Tutahakikisha suala lako linafanyiwa ufuatiliaji kwa haraka.

Asante. ^HN
Kwa umbali wa mita 500 njia moja gharama imekaaje.?

kwa sehemu za vijijini (same). Mlisema mradi wa REA nafuu lakn nimefatilia naambiwa nguzo tano 1.5 Million apo bado gharama nyingine.

Ni sahihi ?
 
Back
Top Bottom